Matatizo mbalimbali ya kindoa na majibu yake. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo mbalimbali ya kindoa na majibu yake.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bujibuji, Jan 18, 2012.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,436
  Likes Received: 22,349
  Trophy Points: 280
  Kwenye ndoa kuna matatizo mengi sana yanayotukuta eitha sisi wenyewe, marafiki zetu, ndugu zetu na watu mbalimbali. Tunayasikia matatizo hayo kila siku kwenye mazungumzo tunayoyafanya, kupitia magazeti ya udaku na vyanzo vingine mbalimbali.
  Kupitia uzi huu, tutaweza kuweka matatizo ya kindoa kisha tuone nini linaweza kuwa suluhisho kwa tatizo hilo.

  TATIZO:-
  Mdada maarufu anajielezea. "Mimi nimeolewa miaka miwili na nimebahatika kupata mtoto mmoja kwenye ndoa yangu.
  Mume wangu anautumia muda wake mwingi nje ya nchi ambako anasakata soka la kulipwa.
  Tatizo langu ni kwamba, mume wangu awapo mbali huwa ninamkumbuka sana na ninatamani aje niwe naye, lakini akija ninamchukia, namfanyia visa na kumtukana na kumvunjia heshima mbele ya watu.
  Je nimerogwa? Nifanyeje ili niidumishe ndoa yangu?

  Wana JF hebu tuchangiane mawazo ili kumnusuru mrembo huyu na ndoa yake.
   
 2. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  :A S 465:Kulogwa tena!!! Hilo nalo neno,ngoja nikapate msunguti nitarudi na shemeji aseme!!!
   
 3. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,348
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Jamani huyo anayezuga kurogwa ili aachane na mumewe si ndio yule Irene WOWOWO?
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,436
  Likes Received: 22,349
  Trophy Points: 280
  Aende akafanyiwe maombi, pia apunguze mahusiano nje ya ndoa, maana hayo ndiyo yanayomfanya amchukie mumwe wake kila ajapo bongo.
   
 5. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,348
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Ukisha yazoea maisha ya kuruka njia, maisha ya ndoa utayawezea wapi?Aombe tu talaka yake, arudi kwenye soko lake rasmi, awaombe pia radhi wateja wake kwa kuwacheleweshea huduma kipindi alichokuwa ndoani.
   
 6. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hana kurogwa wala nini wakuroge kwalipi? ebu tuliza mapepe umetaka kwani ulikua hujui kama kuolewa sio lelemama?
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mh jamani majaribu mengine ni mazito.
  Buji mwambie binti huyu asali sana. Aiweke ndoa yake kwenye maombi kwani inawezekana ni mambo ya ushirikina. Huwenda mumewe ana kimada sehemu nyingine ambacho kimemtengenezea mazingira ya kutoelewana na mkewe au yeye mdada ana kibanda chake ambacho kinamharibia kwa mumewe au wote ni wasafi lakini yupo asotaka wawe pamoja.
   
 8. M

  MUMY A JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 234
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya matatizo mengine jaman......kazi!!!
   
Loading...