Matarajio ya mzazi anapomsomesha mtoto ni yapi hasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matarajio ya mzazi anapomsomesha mtoto ni yapi hasa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mwiyuzi, Sep 19, 2012.

 1. Mwiyuzi

  Mwiyuzi JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 861
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 80
  Habari zenu wanajamvi,

  Katika familia yetu mimi ndo nilifanikiwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu, wengine waliishia std 7 na wengine form four, japo kwa sasa wengine ni wajasiriamali na wengine ni ma day worker viwandani.

  Nilimaliza chuo na kukaa muda mrefu bila ajira, lakini nikabahatika kupata kazi ya tempo ambayo ni ya miez mitano. Baada ya kupata kazi nilimpatia mama hela kama zawadi akashukuru, baada ya mwezi akaniomba nimkopeshe laki moja ili alipe deni kwani anadaiwa, nikaamua nimpatie hiyo laki moja bila kumkopesha, Baada ya miezi kama miwili akaniambia nitoe mchango kwa aliyekuwa rafiki yangu wa primary aliyekuwa akitarajia kufunga ndoa, nilikataa kutoa huo mchango kwani mtoto wa shangazi yangu alikuwa akihitaji ada kwa ajili ya kwenda shule, kwa hiyo nikampatia kiasi yule wakusoma, mama akaniambia kuwa kama nimeshindwa kutoa mchango wa harusi ya yule rafiki basi nimchangie hela ya zawadi atakayoitoa kwani huyo rafiki huwa anamsalimia vizuri...kusema ukweli sikumpatia hiyo hela.

  Juzi kanipib nikapiga akaniambia nimpunguzie vocha, nikampunguzia vocha ya elfu tano lakini nikashangaa kuona kimya wakati vocha imeenda, kumpigia simu akasema kuwa hakurespond kwani alijua niko kanisani lakini kabla sijakata simu akasema kuwa sakafu ya nyumba yetu imebomoka na rangi ya nyumba imepauka so inabidi nigharimie.

  Sasa mimi nikajiuliza kwamba hivi huyu mama kwa nini hataki kuelewa kuwa kazi niliyonayo ni tempo tu? Mshahara wangu ni mdogo lakini anademand kiasi hiki...hivi anataka mimi nifanyeje? Na kwa nini asiwaambie pia kaka zangu na dada ili nao wachangie kwa kuwa mimi bado sijasettle kimaisha? Je anafanya hivi kwa sababu mimi peke yangu ndo niliyesoma kwenye familia?

  Kwa kweli simuelewi mama yangu! Manake nimeona kuwa ukiwa umesoma kwenye familia ndo unakuwa kwenye wakati mgumu wa kulaumiwa kupita wote...kwani ukimpatia mtu leo hela anakushukuru kwa mikono miwili lakini siku ukimwambia sina utasikia lawama kibao! Hivi na wazazi wengine wako hivi?
   
 2. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Hizo ni challange za maisha tu! Itakuwa mama yako ana high expectations na wewe, ndo maana anaamini kuwa wewe ndo utamtoa! La msingi endelea tu kufight tu utapata kazi nzuri, na hela zitatosha kumtimizia Bi Mkubwa wako! We uspanick wala kukwazika nenda nae taratibu si unajua tena bi mkubwa itakuwa kazoea enzi zile wasomii wana maana sana katika jamii, na wanaheshimika sana! We mwambie mimi uwezo wangu ni kukupa kiasi flani kwa mwezi, then Bi Mkubwa amua mwenyewe ukitumieje, tukiachana hapa mpaka mwisho wa mwezi
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ushauri wa hapo juu ni mzuri sana.
  Nami naongezea kuwa kwavile wewe ni msomi, organize nduguzo hao ili muanzishe kitu kama fund ya kumwezesha mama. Kila mtu atamke kiasi atakachomudu kutoa per month, then mama atajipangia mwenyewe namna ya kuitumia, ili mradi asionekane msumbufu kwako!
  Mama Theresa wa Calcutta alisema kuwa hakuna Tajiri asiyehitaji chochote, wala HAKUNA MASIKINI ASIYEWEZA KUTOA CHOCHOTE!
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Pole sana
  sometimes wazazi hupenda kutesa 'watoto wanaowapenda zaidi'
  bila kujua....

  ndo ukubwa huo....nenda nae taratibu tu
   
 5. Root

  Root JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,264
  Likes Received: 12,985
  Trophy Points: 280
  Bora wewe Mama tu vipi kama ndugu zako wote wangekuwa wakikutegemea?
  Anza kujituma ili upate hela zaidi
   
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mwiyuzi Pole sana... Tukiwa tunakua hua mara nyingi kama watoto tunaamini kuwa wazazi wetu wapo exceptional kuliko wanadamu wengine, na sometimes kua hawana kasoro. Ambayo mara nyingi sio kweli.

  Wazazi tumetofautiana, na kila mmoja hum treat mtoto wake (kwa kujitegemea kwake) tofauti na wengine. La muhimu ni kua ni muhimu sana kumpa heshima yake mzazi lakini pia inabidi umjue mzazi wako na kumsoma. Ukisha jua hulka yake ni rahsi kuenda nae sambamba. Huyo mama yako ni moja ya wale wenye kati ya hizi tabia...


  1. Anaona kua pale mtoto wake apatapo kazi ndio chanzo cha pesa kwa shida yoyote ile... Hii haitakuja kuisha hadi uweze i control namna gani unaweza iepuka.
  2. Ana amini kuwa once mtu yeyote yule awapo msomi (na hii ni wengi) basi anakuwa kila mara ana pesa (naona tokana na imani ya kuamini kuwa wasomi wote wanazo, yaani haiingii akilini kuwa huwezi kuwa na pesa). Kwa hili inabidi pia umuweke sawa na kumuelewesha huku ukimpa matumaini kuwa ukiwa sawa mwenyewe atafurahia.
  3. Anaona ni wajibu wako, na hupaswi kukataa... Kuwa yeye kakulea na kukufikisha hapo ulipo (in a way she is right), na kama kashikilia hili inabidi uwe makini sana jinsi ya kumuelewesha akaelewa na kutokwazika. Mie naamini sana katika radhi ya mzazi.. Jitahidi tu usifike mahala ukagombana naye.


  Kwa mtazamo wangu the best way ni kukaa na kuongea nae kwa kujadili, upole na upendo kuwa bado haupo sawa na kwamba hata hivo utajitahidi walau kumpatia kiasi fulani cha pesa kwa mwezi mara moja ama mbili. Kwamba ukisha mpa hizo pesa msijuane... (labda dharula za msingi) Hii labda yaweza siadia wewe na yeye pia kuwa na amani... La muhimu kuliko yooote kumbuka ni mama yako na upo responsible kwake, tafuta tu njia ya kusema muivane huku ukimsaidia sababu usipoangalia utakuja mchukia... Which will be a disaster!
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Mwiyuzi

  Mwiyuzi JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 861
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 80

  asante sana kwa ushauri...itabidi nifanye hivyo
   
 9. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  lara 1 umezungumza vyema, utafikiri si yule wa kufunguka aka mcharuko tunayemfahamu!
  By the way ishu zako na Boss wako zimeishia wapi?!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  mshukuru mungu mzazi wako, mama kabisa yupo hai na yupo karibu na wewe, mama anakupenda may be kutokana na usikivu wako na juhudi zako ktk maisha, siyo rahisi mama kupenda watoto wote kutokana na tabia za watoto kuwa tofauti, kwa hiyo ukiwa nayo mpe kwa moyo mkunjufu utabarikiwa kabisa nani kama mama? Changamoto kama hii me pia ninayo lakini mama ni mwelewa anajua nikiwa nazo lazima nitoe matumizi ya nyumbani, nikiwa kimya najua mwanangu hana pesa kwani ananipenda na siku zote ananiombea nifanikiwe zaidi mpaka kesho nipo tayari kumpigania mama kwani mama ni mama***love your mum, and you will be blessed 4rever***********
   
 11. Spinster

  Spinster JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 393
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  yan mi nashangaa kwa kwel..npo chuo wazaz wang wanasema ukimaliza nkipata hakuna kuhama nyumban..wala hawak kuckia naolewa bila kupata kaz ..hv jaman kaz c majariwa so hata nikae miaka20 bila kupata kaz nciolewa ...na matarajio yao ni kwamba nkiolewa ctowalipa fadhira..
  ukwel watt wa mkulima tunasomeshwa ili tusaidie familia zetu..tena kwa lazma co hiari...utackia tucnge kusomesha tungekua na nyumba na magar sahv..
   
 12. s

  sindo Senior Member

  #12
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hiyo ni challenge, umemshauri vizuri
   
 13. s

  sindo Senior Member

  #13
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ila sio siri, hiyo ya wazazi noma, experience yangu ni mbaya sio nzuri kabisa,
  Maana kila issue wewe ndio wa kusolve, pesa utaoata waoi hakuna ajuaye mama anakuwa mkali balaa, Lazima utoe pesa na usipotoa hamuelewani. Pata shida inayohitaji uwepo tu wa ndugu uone! na akija anakuwambia mpe nauli sijui hilo mnalionaje jamani
   
 14. s

  sindo Senior Member

  #14
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Muda mwingi hupati sapoti sanasana lawama tu kila ukitoa inaonekana kidogo,
  Yaani hapo mimi sisemi nakwazika ile kinoma
   
 15. s

  sindo Senior Member

  #15
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Niliuguliwa nikawa natumia elfu 45 kila siku na mgonjwa anajua, hapo akija mtu kumuona, mgonjwa anakuuliza umeshampatia nauli. Imagine nauli ya kurudia na aliyokujia inabidi umpatie. Hapo angalia unavyokwazika. Hapo wengine ndio kama maisha yetu. Demand nyingi mpaka unakimbia
   
 16. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Hahaaaa! Mimi mama ushauri umesahau!!!! (NANI KANUNA????) Bosi yupo bado anajilia vya bure! Mission ya bosi Nimeiabort nimeona iatanicost economically!!! We fikiria nikitoka nae hapo hata akinipunguzia OT siwez kulalamika manake ndo mtu wangu hivo! Watu wakimsema me ndo niumie badala ya kuongezea midongo! Hapo akiamua anakuomba uje jmosi bila OT! Akuuuuuu! hiyo itakuwainvestment ZEMBE. Amakweli PENZI KITOVU CHA UZEMBE!!!!!!
   
 17. Fund

  Fund Member

  #17
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  POle sana Mkuu,but jambo moja ni kwamba,tafuta pesa umfungulie biashara ili awe anapata pesa humo,hayo ni ya kawaida mkuu
   
 18. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Dah, napata picha ukija kuoa itakuwaje? My boyfriend alikuwa na tatizo kama hilo, yeye mamayake alikuwa akija home anamwambie siondoki hadi unipe one million! Kwa vile jamaa alilelewa na mama basi anajikamua hadi anampa mama 1 m, halafu anapigaje miayo??Be very careful na hayo masuala otherwise utayumba sana kiuchumi na hata kisaikolojia utaathirika. All in all mama ni mama, do the best you can to satisfy her whenever you get a chance ila kama ataendelea kuwa so demanding kaa nae na mueleweshe I believe atakuelewa tena do that as soon as possible before you get married!
   
 19. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Ungeendelea tu, huwezi kujua labda ungepata ka-promotion!:redface:
  Probably na visafari vya hapa na pale mkiwa naye, na kujikuta unajipatia per diem za bure na raha za bure, LOL!
   
 20. K

  KENET JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 259
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kama uwezo wako kwa siku unapata zaidi ya milioni moja.Kwani kumpa mama yako milioni moja kuna tatizo gani.Mama hawezi kumdai mwanae milioni moja kama hajui uwezo wake.
   
Loading...