Matapeli wapya

Matapeli wapya

abunerimgaya

Member
Joined
Nov 13, 2012
Posts
78
Reaction score
15
TAHADHARI MATAPELI WAJA NA
NJIA MPYA SASA
Kuna dada mmoja anasoma chuo
buguruni na pia ni mfanyakazi
hivyo jioni akitoka kazini ndipo
huenda shule.Sasa akiwa njiani
kuelekea chuo akapigiwa simu na
mtu asiyemfahamu
akajitambulisha kwamba yeye ni
daktari wa lugaro hosp na
kumuulizia habari za mwanae
ambae alishawahi kwenda
kumtibu pale na chakushangaza
zaidi akataja mpaka aina na rangi
ya nguo aliyovaa siku ile
alipokwenda hapo hospitali na
yote yalikuwa kweli. Na zaidi
akamwambia najua sasa hivi
unaelekea chuo buguruni na
kweli ilikuwa hivyo, lakini
mwishoni akamweleza kwamba
kuna mambo anataka kujua kujua
kuhusu hicho chuo hivyo nae
anaelekea huko hivyo akifika tu
atamtafuta. Kwa muda wote huo
huyo dada hakuweza kabisa
kumkumbuka ila akajipa moyo
kwamba yamkini huyo mtu
atakuwa anamfahamu vizuri.
Baada ya kutoka chuo akiwa na
wenzake watatu akawa
anawasimulia habari za huyo mtu
ndipo simu yake ikaita,kupokea
yule mtu akamwambia nakuona
uko na wenzio wawili mnavuka
barabara na kumueleza jinsi
alivyovaa sasa wenzie wakasema
huyo mtu anakufahamu
haiwezekani hapa tupo watatu
kweli na ameweza kukutambua.
Kisha huyo mtu akamwelekeza
mahali alipo ambapo haikuwa
mbali na barabara.
Lakini alipomtazama
hakumfahamu kabisa, basi
akampa mkono kumsalimia,
baada ya hapo hakujitambua na
zaidi alijikuta yuko maeneo ya
chuo kikuu cha DSM akiwa hoi.
Kuangalia simu na kila kitu chake
kilikuwa salama na hakufanyiwa
kitu chochote, kwa bahati
kulikuwa kuna ndugu yake
anasoma chuo hivyo
akawasiliana nae ili kupata
msaada ikabidi awahishwe
mwananyamala hosp lakini
ikaonekana sumu iliyotumika ni
kali na dawa yake wanayo
regency hosp,hivyo
akawahishwa regency na kupata
matibabu.
Baada ya ufahamu kumrudia
akakuta mtu huyo kachukua pesa
zote kwenye mpesa,tigo pesa na
bank (NMB na CRDB) kiasi cha
milioni 3, hivyo inawezekana
walipompa sumu alitaja password
pasipo kujijua.
Na bank walipotazama kwenye
ATM Camera waliona picha ya
huyo mtu na yeye alimkumbuka
vizuri, lakini polisi Kijitonyama
wakakiri kwamba kesi hizo sasa
hivi zimetokea mara nyingi na
huo mtandao ni mkubwa,
walipoenda kwenye usajili wa
simu walikuta ni huyo huyo na
jina lake ndilo alilojitambulis
ha.Ingawa polisi wameshindwa
kumkamata.
Akiwa kituo cha polisi mara huyo
mtu akampigia simu akimwambia
‘’kumbe wewe ni muoga sana
tutakurudishia pesa zako’’. Sasa
kumbe wanachofanya
wanakuambia’’ tutafutie mtu
ambae unahisi ana pesa kuliko
hizi halafu tukifanikiwa
tutarudisha pesa zako’’ hivyo
inawezekana nae kuna mtu
anaemjua alifanyiwa hivyo
akaamua kumtaja yeye.
- HIVYO NI KUOMBA MUNGU NA
KUWA WAANGALIFU
 
aise huu ni wizi wa hali ya juu sana kama mtu hujapata kisa kama hiki huwezi kujua kinachoendela asante kaka kwa taarifa
 
Labda uwe Mossad ndiyo unaweza kukabiliana na uhalifu wa aina hiyo.
 
na huwezi kukwepa coz kuna nguvu fulani wanaitumia
yatupasa kumuomba Mungu.
 
Duh!! Hao jamaa ni noma, tujiadhari na wa2 wanao piga cmu za kizushi kama hizo, hakuna kushobokea wa2 2co wafahamu.
 
Back
Top Bottom