Matapeli wana akili sana; Huko Mwanza, mteja amekwenda depot ya bia na kuweka oda, akapewa akaunti

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
1,333
MATAPELI WANA AKILI SANA...
Huko Mwanza, mteja amekwenda DEPOT ya bia na kuweka ODA, akapewa akaunti namba ili akalipie fedha benki, karejea saa 11.30 jioni akiwa na BANK SLIP na Gari aina ya FUSO ili kubeba BIA zake, mteja alionekana mwenye haraka sana. Wenye DEPOT wakapiga simu Benki na kugundua kuwa hakuna pesa zilizowekwa, wakati wanagundua hivyo ndipo wanajua kuwa mteja "ameshasepa akimuacha mwenye Fuso anashangaa". Mwenye Fuso amehojiwa na kudai kuwa yeye amekodiwa tu. (Risiti hii hapa chini inasemekana ndiyo iliyokabidhiwa kwenye DEPOT na mteja, na inatajwa kuwa feki).
FB_IMG_1485531327099.jpg

Chanzo Mimi mwenyewe nipo DEPOT
 
Mbona huelweki kama unaoga njee
Yaani ni kwamba mteja kaja na pay slip lakini hiyo pay slip ni feki, inaonesha imelipiwa benki na mhuri upo ila benki wanasema hakuna pesa iliyowekwa na jamaa kashaondoka na mzigo.
Mwenye fuso anasema amekodiwa hajuani na aliyekuja kuchukua bia.
 
Wahusika wa hiyo depot siyo waangalifu au hawajui pay slip inatakiwa iweje au wamekula deal na huyo jamaa.

Mbona pay slip inaonekana kabisa haipo sawa na watu wakaikubali.
 
Hakuna mwizi anayekuja kukuibia bila kutumia akili duh hali mbaya mnatakiwa kuwa makini sana .
 
MATAPELI WANA AKILI SANA...
Huko Mwanza, mteja amekwenda DEPOT ya bia na kuweka ODA, akapewa akaunti namba ili akalipie fedha benki, karejea saa 11.30 jioni akiwa na BANK SLIP na Gari aina ya FUSO ili kubeba BIA zake, mteja alionekana mwenye haraka sana. Wenye DEPOT wakapiga simu Benki na kugundua kuwa hakuna pesa zilizowekwa, wakati wanagundua hivyo ndipo wanajua kuwa mteja "ameshasepa akimuacha mwenye Fuso anashangaa". Mwenye Fuso amehojiwa na kudai kuwa yeye amekodiwa tu. (Risiti hii hapa chini inasemekana ndiyo iliyokabidhiwa kwenye DEPOT na mteja, na inatajwa kuwa feki).
View attachment 464356
Chanzo Mimi mwenyewe nipo DEPOT
Yaani hueleweki...sasa huyo tapeli alisepa na bia kwa kutumia usafili upi,?....wakati huo huo akimuacha mwenye fusso..kwenye depot..??
 
Yaani hueleweki...sasa huyo tapeli alisepa na bia kwa kutumia usafili upi,?....wakati huo huo akimuacha mwenye fusso..kwenye depot..??
Zamani sisi tukisoma Kiswahili kulikuwa na "topic" ya "Utungaji"
Katika maada hiyo tulifundishwa jinsi ya kusoma habari na kuifupisha,jinsi ya kusoma habari na kuipa kichwa cha habari na pia jinsi ya kutunga habari kwa kutumia visa vya kweli na vya kutunga.

Mtoa maada ni kama hivi vitu,hasa jinsi ya kuweka kichwa cha habari hakuvipata vizuri wakati wake
 
Wahusika wa hiyo depot siyo waangalifu au hawajui pay slip inatakiwa iweje au wamekula deal na huyo jamaa.

Mbona pay slip inaonekana kabisa haipo sawa na watu wakaikubali.
Si ndo maana wakapiga simu benki.kuhakikisha jamaa akasepa.
 
Back
Top Bottom