Matapeli bwana, nimetumiwa hii SMS

Matapeli bwana, nimetumiwa hii SMS

Sirdirashy

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
3,252
Reaction score
3,074
Habari, naitwa Mr. Raymond from EUROCARTA LTD Dar, tupo kikaoni tunapitia CV tuchague candidates wa kuinterview for FINANCE OFFICER POST, salary ni 1,200,000/=. CV yako ni nzuri nataka kukusaidia upate hii kazi, kwa terms zifuatazo, ukishaanza kazi utanipa laki 3, na kabla ya saa 9 mchana uwe umetuma sh. elfu 40 by tigopesa to 0713-765442 ili nimpe mtu wa interview amesema anataka hiyo hela leoleo ili atoe maswal ntakutumia kwenye e-mail for now siwezi ongea mpaka badae nikitoka kikaoni na ndio muda huo utapigiwa simu lini uje for interview, jitahidi utume mapema.
 
Ujadadavua
kuwa wewe ulishatuma cv kwenye hiyo kampuni husika?
na ye wewe umesomea hiyo field?
maana kuanzia hapo ndio tutajua kuwa kuna kutapeliana hapo
 
kwani interview ya kazi ni kama mtihani wa shule kwamba ukitumiwa maswali ndio unaweza kufaulu? Maswali common ya interview mbona yanajulikana na bado watu wanachemka. Utapeli huo umeshaanza ku expire waje na single nyingine.
 
Mara ya mwisho kutapeliwa ilikuwa mwaka 2000 tena nilitapeliwa 500 kanyaboya baada ya hapo kila mtu namuona mwizi.
 
hawa matapeli naona wameishiwa mbinu huwezi kumpata mtu kwa style hii.
na kama atapatikana basi atakua hajielewi.
 
Halafu sijui ni nani huyu mtu anapenda kutuma message hiyo mie mwenyewe alinitumia wakati nimeishia form two si ndo hapo nilishangaa
 
Mara ya mwisho kutapeliwa ilikuwa mwaka 2000 tena nilitapeliwa 500 kanyaboya baada ya hapo kila mtu namuona mwizi.

You are right!
Hata mm nikienda maeneo ya town yeyote atakayeniita naona mwizi vivyo hivyo ktk simu,akitanguliza nimtumie kitu kinachoitwa ''Pesa" naona mwizi.
 
mbona huu utapeli wa sms unafanana sana? inaonekana kuna watu wanaingia mkenge. wanajamii mliopo dar kwanini msiwakamate hawa watu? ni rahisi sana kuwaingiza mtegoni
 
Hizi meseji nimezizoea mwenzenu ila ushauri wangu ni kwamba USITUME PESA hata siku moja kwa style hii hata kama huna kazi ndugu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom