Napata wasiwasi na upatikanaji wa kazi zinazotangazwa hapa nchini,kinachonishangaza ni kwamba kila kukicha matangazo ya kazi mpya ni mengi sana cha ajabu matangazo ya kuitwa interview hayapatikani,hawa wanao post kazi humu anzisheni pia utaratibu wa kufuatilia uhakika wa kazi hizo pamoja na feedback kuhusu usaili,pia napendekeza hawa wanaopost kazi mpya hapa wajaribu pia kuwa wanaweka na matangazo ya interview,vinginevyo nimeanza kuamini kuwa kazi za tanzania ni kujuana,wanaoleta matangazo ni kweli kwamba wanakuwa tayari wana watu wao,wanatangaza kama ushahidi tuu...kungekuwa na uwazi, kasi ya matangazo ya ajira mpya ingekuwa sawasawa na kasi ya matangazo ya usaili...nawasilisha