Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,932
- 31,178
Kampuni ya Africa Media Group (Ltd) inayomiliki Kituo cha Televisheni cha Channel Ten na Radio Magic FM, imetangaza kuwa kuanzia sasa matangazo yake yataanza kupatikana kwa njia ya satelaiti ya INTELASAT na masafa ya 3905.63 MHZ.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi Channel Ten/ Radio Magic FM, Augustino Mganga, alisema wameanza kuyapata matangazo ya Radio Magic FM na televisheni kupitia Satelaiti ya INTELSAT 906 64E, masafa ya 3905.63 MHZ, Symbol Rate 2.8435 Msp na FEC 2/3 LHLCP.
Alisema matangazo hayo yanatumika kwa wale wanaotumia Satelaiti Dish kupata matangazo ya Channel Ten na redio hiyo. Alisema hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwa wananchi wanaotumia antena za kawaida kwa televisheni na wasikilizaji wa redio.
Source:Habari leo