Matangazo ya Channel Ten hewani

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,799
30,724
Kampuni ya Africa Media Group (Ltd) inayomiliki Kituo cha Televisheni cha Channel Ten na Radio Magic FM, imetangaza kuwa kuanzia sasa matangazo yake yataanza kupatikana kwa njia ya satelaiti ya INTELASAT na masafa ya 3905.63 MHZ.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi Channel Ten/ Radio Magic FM, Augustino Mganga, alisema wameanza kuyapata matangazo ya Radio Magic FM na televisheni kupitia Satelaiti ya INTELSAT 906 64E, masafa ya 3905.63 MHZ, Symbol Rate 2.8435 Msp na FEC 2/3 LHLCP.

Alisema matangazo hayo yanatumika kwa wale wanaotumia Satelaiti Dish kupata matangazo ya Channel Ten na redio hiyo. Alisema hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwa wananchi wanaotumia antena za kawaida kwa televisheni na wasikilizaji wa redio.
Source:Habari leo
 
Well wanasema sababu ni nini walikuwa hawapatikani? Kwa nini hawakutupa taarifa za kutokurusha matangazo yao?
 
Hello Channel Ten,
Holla, we welcome you back on air. Stesheni yenu ni bomba na tuliimisi sana kwa taarifa za habari za mapema kuliko vituo vingine.
Big up!!
 
"Well wanasema sababu ni nini walikuwa hawapatikani? Kwa nini hawakutupa taarifa za kutokurusha matangazo yao?"

***************************
Eeka Mangi:
Inasemekana walikuwa wanatumia freequency za ITV -- na Mengi akawakatia ghafla kwa sababu aliona Channel Ten imeingiliwa na mafisadi -- RA na yule Tanil Somiya wa kashfa ya radar.
 
Waache usanii! Mpaka leo hawajarudi hewani. Hizo details zilizotolewa wala hazijawa updated kwenye website ya lyngsat mpaka leo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom