Matangazo ya bahati nasibu yamezidi sasa

Matangazo ya bahati nasibu yamezidi sasa

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,557
Matangazo Yamezidi si kwenye TV si kwenye simu zetu
Sasa hivi imefikia washindi wanaonyeshwa katika Matangazo ya biashara Kutwa
Tunashuhudia mmoja wa washindi akizungushwa mitaani akiwa juu ya Hammer, yote hii ni nini?
Nadhani imefikia wakati tujiridhishe wote na namna mshindi anavyopatikanaanavyopatikana,
Hoja nyingine ni kuwa michezo hii hata kama umeshinda lakini umezima simu au upo busy na kazi ukipigiwa usipokee simu kwa wakati eti unakua umepishana na pesa kwa maana anatafutwa mwingine japokua namba yako ndio imeshinda mwanzo, hii imekaaje?
Nimitegemea sana takukuru watoe ushirikiano mkubwa kipindi hiki.
 
Siku hizi hata vipindi vya redio vimeharibiwa na hawa wa kamali.Yaani tangazo linapigwa alafu wanakuja tena watangazaji nao wanalizungumzia weeee yaani imekuwa too much.
TCRA mko wapi sijui
 
Mitandao ya simu imekuwa ni chaka la majambazi maana unashinda wewe million 50 anapewa mtu mwengine, kama si ujambazi ni nini?
 
Member mliochangia mko sahihi
Hata mimi nakerwa na haya matangazo ndio maana muda mwingi siangalii channel za bongo
 
Matangazo Yamezidi si kwenye TV si kwenye simu zetu
Sasa hivi imefikia washindi wanaonyeshwa katika Matangazo ya biashara Kutwa
Tunashuhudia mmoja wa washindi akizungushwa mitaani akiwa juu ya Hammer, yote hii ni nini?
Nadhani imefikia wakati tujiridhishe wote na namna mshindi anavyopatikanaanavyopatikana,
Hoja nyingine ni kuwa michezo hii hata kama umeshinda lakini umezima simu au upo busy na kazi ukipigiwa usipokee simu kwa wakati eti unakua umepishana na pesa kwa maana anatafutwa mwingine japokua namba yako ndio imeshinda mwanzo, hii imekaaje?
Nimitegemea sana takukuru watoe ushirikiano mkubwa kipindi hiki.
Itv aanaonyesha kwenye habari za michezo
 
kuna siku hii michezo itapigwa marufuku kama ilivyopigwa marufu nchi za mbali ambao waliathirirka zaidi...ni jambo la kusubiri muda tu.
ukweli ulio dhahiri ni kwamba serikali yetu kuna taasisi haipo hai, haifanyi kazi wala haina uelewa juu ya madhara ya hii kitu.... na adhari yake kwa uchumi wa viwanda...
 
Hali ngumu sana ndio maana wengi wanaamua kucheza hiyo michezo na wenye michezo hiyo wanapata pesa nyingi ili kuvutia watu wanalipia matangazo mengi sana.
 
Back
Top Bottom