Matamko gani ya kisiasa yaliyokuvutia wakati mzee Mustapha Songambele ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,213
4,720
Mkoa wa Dar es salaam umewahi kuhudumiwa na Wakuu mbalimbali wa akiwamo Mheshimiwa Mustapha Songambele

Mzee aliyejaaliwa hekima, busara, weledi, umakini na uadilifu mkubwa

Je ni matamko gani ya kisiasa yaliyokuvutia wakati akihudumu kwa nafasi ya RC wa Dar es salaam

FB_IMG_16282399521157478.jpg
 
Mshana Jr Bujibuji wazee kuna uzi wenu huku wa wahenga
Akizungumza na baadhi ya wafanyakazi katika Idara ya Itikadi na Uenezi, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Songamebele (88), alisema, mwaka 1970, wakati huo akiwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na pia Katibu wa TANU wa mkoa huo, alienda nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chama, Mwalimu Nyerere, kwa ajili ya mazungumzo maalum.
Alisema, wakiwa katika mazungumzo alitamka maneno ambayo yalimfanya Mwalimu Nyerere kucheka hadi kudondoka sakafuni huku akibubujiwa machozi kwa kicheko.
Mzee Songambele alisema, baada ya rais kuondoka kwenda ofisini kwake, maofisa usalama walimsogelea na kumhoji kwa nini umemchekesha rais mpoaka amedondoka chini? Yaani ulitaka Rais afe halafu tupate tatizo la kutoa maelezo kwamba wewe umemchekesha hadi kufa? inabidi tukukamate uwekwe ndani.
Alisema, baada ya Walizni kusema, hayo alilazimika kujitetea akisema "Mimi nilizungumza tu, sikuwa najua kwamba Mwalimu atacheka sana kiasi kile, sasa hili siyo kosa langu naomba mnisamehe".
"Nilipoona wanatafakari kidogo nipanda ngazi hadio ofisini kwa rais, nikamkuta, akasema, 'bwana nimeshacheka sana inatosha basi", nikamwambia Mwalimu mimi sikuja kukuchekesha tena, lakini tazama hawa walinzi wanataka kuniweka ndani kwa sababu wewe umefurahi ukacheka, sasa nimefanya kosa gani?", aliseleza Mzee Songambele.
Alisema, baada ya Mwalimu kusikia malalamiko hayo, aliwaita walinzi na kuwaamuru wamwache huru ndiyo ikawa salama yake, akaondoka.

1628247058589.gif


1628247059015.gif


1628247058805.gif


1628247059238.gif


1628247059451.gif


1628247060093.gif


1628247059659.gif


1628247059877.gif
 
Mkoa wa Dar es salaam umewahi kuhudumiwa na Wakuu mbalimbali wa akiwamo Mheshimiwa Mustapha Songambele

Mzee aliyejaaliwa hekima, busara, weledi, umakini na uadilifu mkubwa

Je ni matamko gani ya kisiasa yaliyokuvutia wakati akihudumu kwa nafasi ya RC wa Dar es salaam

View attachment 1882585
Kwakua huyu mgogo wakongwa unamfahamu ungetupia moja unayoifahamu ili mengine yafata ,hata wewe hujui
 
Back
Top Bottom