Matajiri wausiwa kudai nchi bora kutokana na ajali ya Anthony Joshua

Matajiri wausiwa kudai nchi bora kutokana na ajali ya Anthony Joshua

Ili tujikwamue kutoka kwenye umasikini huu lazima tukubali na kukiri kuwa SISI NI MASIKINI,ukishajua na kukiri hivyo lazima pia tukae chini tujiulize UMASIKINI WETU UNATOKANA NA NINI? baada ya hapo tujiulize JE NI NJIA GANI TUZITUMIE KUONDOKANA NA UMASKINI HUU? baada ya hatua moja baada ya nyingine tunapambana na umaskini huo. Lakini kwa hapa Afrika umasikini hauwezi kutoka kamwe ikiwa tu nchi za bara ulaya,amerika asia na kwingineko bado zitakuwa zinategemea raw materials kutoka kwetu. lazma tujue umasikini wetu unatokana na ukoloni mambo leo na ukitaka kupambana na ukoloni wa aina hii basi wewe utakuwa umeweka rehani maisha yako. so,afrika yatupasa tuukubali ukweli na tuishi nao, afrika ikiungana,kuwa kitu kimoja,sauti moja tutaushinda umasikini,lakini kwa kila nchi kupambana kivyake itachukua miaka 500 kuuondoa umaskini huu. cc HAYA LAND HOV
Nchi za bara Ulaya zinategemea malighafi kutoka KOTE duniani, sio Africa tu.
 
Ali Mufuruki aliwahi kusema katika moja ya talks zake hapa bongo hata ukiwa tajiri uko na milioni 100 cash kwenye gari ukipata ajali mkoa wa pwani tu nje kidogo tu ya mji ambako hata sio mbali na jiji la Dar es Salaam sio ajabu kufa kwa kukosa huduma ya ambulance helicopter tu kwa wakati ikuwahishe hospital.
Wakati tuko wadogo,kuna jirani alikuwa na pesa sana. Nasikia alikuwa ananunua mazao kama tumbaku na pareto ana export. Alipata ajali akiwa na BMW yake huko Makambako. Alikufa akiwa na hela za kununua mazao kwenye booty ya gari.
 
Ndugu yangu 😃
Siye waafrika ni kama tumeumbiwa maisha ya purukushani flani hivi. Nchi za wenzetu huduma za kijamii ni jambo nyeti saaana.

Ngoja nikupe mfano: Miaka ya nyuma, niliwai kuishi Japan. Siku moja nimeamka kichwa kinauma sana. Nikaenda pharmacy nikanunua dawa (Japan masuala ya dawa za hospital yana uthibiti mkubwa, Kwahiyo ukienda kununua hata panadol watachukua taarifa zako n.k)

Kesho yake, watu wa pale pharmacy walinipigia simu kujua naendeleaje na kama nahitaji msaada wowote zaidi. Kisheria wanatakiwa kufanya follow up kunijulia hali. Ilinishangaza maana mimi niliitikia kimoyomoyo “ah wazee, kichwa tu mnakaba hivi?”

Kama mdau wa sekta ya afya natambua ni kiasi gani wagonjwa wengi wa saratani wanakufa kwa kukosa uduma za kutambua ugonjwa mapema, mbadala wa tiba kama chemotherapy/radiotherapy na patient care iliyo bora. Kwa wenzetu huku hata wagonjwa wa saratani wanayo matumaini kwa sababu ya huduma bora. Anyway, tumuombe Mungu 🙏😃
Acha kulinganisha Marekani na Takataka za Africa

Black Americans are about 13% of the US population, but ~37% of the homeless population.

Huoni kama ni uvivu wao... Umewahi kukutana Wahindi au wachina homeless US ? Wapo ila in few number.

All in all Ukiwa na Hela na umezungukwa na masikini wewe ni masikini mwenye Hela tu.

Mfano mzuri ni hiyo ajali ya Anthony Joshua.

Mtu kapata ajali ila anabebwa kama Yuko mapori ya Morogoro au Katavi miaka ya 1970.

Alier
Bodaboda umezitaja. Zinaua sana watu hizi.

Sasa huku kuzifanya usafiri wa kulipia ndiyo kabisaa.

Kuna vijana wengi sana wanamalizika. Hii keo nineoeea taarifa kuna mwana wa miaka kibao Upanga amefariki kwa ajali ya Bodaboda. Miezi kadhaa nyuma mwaka huu kuna cousin alifafiki kwa ajali ya Bodaboda.
Alierasimisha boda ziwe usafiri wa umma alitukosea sana!

Boda imeua watu wengi sana
 
Umasikini hauwezi kuisha Afrika kwa sababu Waafrika wameukubali umasikini.

Hawafanyi jitihada za kitosha kuukataa umasikini.

Kuanzia viongozi mpaka wananchi wa kawaida.

Viongozi wana lawama kubwa, wana wajibu mkubwa, wanafungwa na kanuni ya "noblesse oblige" kwa sababu wao ndio wana wajibu wa kuongoza, na najua mara nyingine kuwasema wananchi inakuwa kama "blaming the victim" lakini hili ni tatizo la jamii nzima na hata hao viongozi ni zao la hii jamii.

Jamii ingejitambua na kusimamia kuupiga vita umasikini hata hao viongozi wabovu wasingeweza kuwapo.

Ndiyo maana kwenye tamaduni nyingine kiongozi akikumbwa na kashfa anaanza kujiondoa mwenyewe katika uongozi.
umoja wa afrika ukiimarishwa ukawa na nguvu na sauti moja basi umaskini utahamia amerika,ulaya na huko asia, lakini kama afrika ikiendelea kuwa disoganized kama ilivyo sasa basi itaendelea kuwa maskini forever. Inatakiwa tuwapate viongozi makini kama MAGUFULI,GADAFI,TRAORE,LUMUMBA,
 
Waache kutoana makafara, ajali itokee wafe watu wawili alaf watatu hata michubuko hakuna ?? hakuna ambulance ingesaidia hapo , although ni kweli Africa huduma ni mbovu zinazingua
 
Ndugu yangu 😃
Siye waafrika ni kama tumeumbiwa maisha ya purukushani flani hivi. Nchi za wenzetu huduma za kijamii ni jambo nyeti saaana.

Ngoja nikupe mfano: Miaka ya nyuma, niliwai kuishi Japan. Siku moja nimeamka kichwa kinauma sana. Nikaenda pharmacy nikanunua dawa (Japan masuala ya dawa za hospital yana uthibiti mkubwa, Kwahiyo ukienda kununua hata panadol watachukua taarifa zako n.k)

Kesho yake, watu wa pale pharmacy walinipigia simu kujua naendeleaje na kama nahitaji msaada wowote zaidi. Kisheria wanatakiwa kufanya follow up kunijulia hali. Ilinishangaza maana mimi niliitikia kimoyomoyo “ah wazee, kichwa tu mnakaba hivi?”

Kama mdau wa sekta ya afya natambua ni kiasi gani wagonjwa wengi wa saratani wanakufa kwa kukosa uduma za kutambua ugonjwa mapema, mbadala wa tiba kama chemotherapy/radiotherapy na patient care iliyo bora. Kwa wenzetu huku hata wagonjwa wa saratani wanayo matumaini kwa sababu ya huduma bora. Anyway, tumuombe Mungu 🙏😃
Nilipoona hii story ya treni moja ya Japan kutofungwa kwa miaka kwa ajili ya binti mmoja tu mwanafunzi ndio nilijua wenzetu kweli huko wanaishi, sisi hapa tupo tuna exist tu kama viumbe hai wengine wowote😁, bado tuna safari ndefu sana
20251230_090435.jpg
 
View attachment 3522577

Huko wenzetu hata kulipa kodi ni jambo la kujisikia raha sana. Anajua pesa yake inarudi kwake kwa njia ya huduma safi za kijamii.
 
umoja wa afrika ukiimarishwa ukawa na nguvu na sauti moja basi umaskini utahamia amerika,ulaya na huko asia, lakini kama afrika ikiendelea kuwa disoganized kama ilivyo sasa basi itaendelea kuwa maskini forever. Inatakiwa tuwapate viongozi makini kama MAGUFULI,GADAFI,TRAORE,LUMUMBA,
Hili wazo la kutaka viongozi makini waje watumalizie matatizo yetu ndio tatizo la Afrika.

Yani hapo wewe ushamtegea kazi ya umakini kiongozi.

Umejitoa katika kazi ya umakini. Unaendeleza fantasy kwamba Gaddafi alikuwa kiongozi mzuri.

Umesoma "Gaddafi's Harem: The Story of a Young Woman and the Abuses of Power in Libya" by Annick Cojean?

Umesoma "The Return: Fathers, Sons and the Land in Between" by Hisham Matar?

Unam romanticize Lumumba?

Umesoma "The Lumumba Plot: The Secret History of the CIA and a Cold War Assassination" by Stuart A. Reid ?

Hao viongozi wote uliowataja wana mapungufu makubwa sana.

Magufuli, Gaddafi, Traore na Lumumba, wote ni populists wenye matatizo mengi sana.

Na bila ya kuwa na wananchi makini wa kuwasimamia hao viongozi, hata viongozi makini wa kweli watachoka na kuishia kuharibu tu.

Moja ya matatizo makubwa ya Afrika ni hii habari ya kutegeana umakini.

Wananchi wanawategea viongozi, viongozi wanawategea wananchi.

Wakubwa wanawategea "Gen-Z", "Gen-Z" wanawategea wanajeshi, wanajeshi wanawategea raia.

Mwishowe watu wanashangaa kwa nini bara lenye rasilimali nyingi bado linagubikwa na umasikini, maradhi na vita?
 
Hauelewi shida inayojadiliwa hapa. Au umejiamulia kutokumuelewa ndugu Kiranga

Antony Joshua ni Millionaire, tena millionaire wa Pounds siyo madafu. Wiki 2 zilizopita kwenye pambano lake inadaiwa alilipwa kama $90M hivi. Leo kakalishwa kwenye ndinga ya polisi akiwa na maumivu makali bila huduma ya mtu wa msaada wa kwanza wala ambulance. Maskini wa marekani, anayebeba maboksi anapata huduma safi sana kuzidi huduma aliyopata millionaire Antony Joshua leo. Hata hao unaowataja ya kuwa wanatembea na escort, gia yao ya kwanza ikitokea emergency ni kukimbilia kwa akina Kiranga walipo . Sasa wewe tulia tu hapo Mwananyamala ambapo kila kipimo cha damu ukienda huwa ni una UTI au malaria 😆😆
😃😃
 
Waache kutoana makafara, ajali itokee wafe watu wawili alaf watatu hata michubuko hakuna ?? hakuna ambulance ingesaidia hapo , although ni kweli Africa huduma ni mbovu zinazingua
Ila Waafrika hata sehemu ikitokea "ajali" ya kweli kwa sababu ya ujinga mnakimbilia habari za uchawi.

Sasa hapo unahakikishaje ni makafara na si kitu kingine?

Huyo Joshua kapona kwa sababu kakaa nyuma, wengine wamepatwa na impact kubwa kwa sababu walikuwa mbele, isn't that a logical explanation? Unaona haitoshi mpaka ulete habari ya makafara?
 
Mimi uzuri wangu nilivyoondoka Tanzania nilijua naondoka kimoja, sikusema naondoka halafu nirudi.

Kurudi labda kuwe na msiba wa karibu sana nimelazimika, au jambo ka dharula kubwa kama hivyo.

Najua nikirudi nitaanza kugombana na watu tangu ubalozini hukuhuku kabla sijagusa Bongo.

Nikifika hapo huo ukiritimba wa airport tu najua nitagombana na watu.

Sasa kuondoa huo ugomvi ndiyo naona bora likizo niende Turks and Caicos tu 😂😂😂
Mkuu fast paced life ya majuu haikufanyi ku miss life letu la kibongo la maisha ya taratibu, mwendo mdogomdogo, ku chill out muda mwingi, hakuna haraka? Nyakati nyingi tu mtu unaamka hujui hata siku, wiki au mwezi utaishije, hakuna mipango yoyote ya maana ila maisha yanaenda tu kama gari kwenye mteremko😁
 
Hili wazo la kutaka viongozi makuni aaje watumalizie matatizo yetu ndio tatizo la Afrika.

Yani hapo wewe ushamtegea kazi ya umakini kiongozi.

Umejitoa katika kazi ya umakini. Unaendeleza fantasy kwamba Gaddafi alikuwa kiongozi mzuri.

Umesoma "Gaddafi's Harem: The Story of a Young Woman and the Abuses of Power in Libya" by Annick Cojean?

Umesoma "The Return: Fathers, Sons and the Land in Between" by Hisham Matar?

Unam romanticize Lumumba?

Umesoma "The Lumumba Plot: The Secret History of the CIA and a Cold War Assassination" by Stuart A. Reid ?

Hao viongozi wote uliowataja wana mapungufu makubwa sana.

Magufuli, Gaddafi, Traore na Lumumba, wote ni populists wenye matatizo mengi sana.

Na bila ya kuwa na wananchi makini wa kuwasimamia hao viongozi, hata viongozi makini wa kweli watachoka na kuishia kuharibu tu.

Moja ya matatizo makubwa ya Afrika ni hii habari ya kutegeana umakini.

Wananchi wanawategea viongozi, viongozi wanawategea wananchi.

Wakubwa wanawategea "Gen-Z", "Gen-Z" wanawategea wanajeshi, wanajeshi wanawategea raia.

Mwishowe watu wanashangaa kwa nini bara lenye rasilimali nuingi bado linagubikwa na umasikini, maradhi na vita?
You nailed

Hat off
 
Mkuu fast paced life ya majuu haikufanyi ku miss life letu la kibongo la maisha ya taratibu, mwendo mdogomdogo, ku chill out muda mwingi, hakuna haraka? Nyakati nyingi tu mtu unaamka hujui hata siku, wiki au mwezi utaishije, hakuna mipango yoyote ya maana ila maisha yanaenda tu kama gari kwenye mteremko😁
Nikikutana na watu wanaoishi hiyo slow paced life nitagombana nao, moja ya sababu inayonifanya nione poa tu kutorudi.

Kuna siku nilikuwa Zanzibar likizo, wakaniletea hizo hizo za nyoronyoro mambo hayaendi sawa, standards mbovu, usalama hauzingatiwi, maisha ya watu yanachukuliwa poa tu.

Niligomba, niligomba, niligomba, mpaka baadaye nikajistukia hapa watu speed yao ya maisha na standards zao si sawa na za New York City huko ninavyo assume mimi.

Inabidi mimi ndiye nifanye adjustment, nimaona naweza kugomba nikaonekana mimi ndiye mkorofi.

Sasa ku avoid yote hayo ndo nina mute huku tu.

I guess ukikaa muda kidogo unazoea ile hali ila I don't miss that.
 
Sijui kwa nini unakuwa kilaza hivi!
Wanaoongoza kunyonya malighafi za Africa kwa sasa ni Wachina ndugu zenu wa damu.
wewe utakuwa unajibu kwa hisia pasipo kufanya utafti hata kwa kutumia google search! Tuanze na Hapa tanzania wawekezaji wengi ni makampuni ya wachina ama wamerekani na bara asia, nenda congo na nchi za franco phone uniambie ni nchi gani zimewekeza huko? Fanya utafti kwanza kabla hujamuita mtu kilaza.
 
Afrika tumelaaniwa yaani wote tupo hivyo hivyo ,familia ya kizigha na samuya wakikusanya magari yao ya bei mbaya unaweza kujenga barabara (za kuunganisha mitaa/rings roads) nchi nzima na pia kuweka emergency road za Ambulance kama ilivyo kwa mwendo kasi.
Mkuu kuna kipindi uwa unaisifia Kenya huwa nashangaa sana. Africa almost yote inafanana if you are not exposed utafikiri kuna wenzio ni bora kuliko kwako.
 
Nikikutana na watu wanaoishi hiyo slow paced life nitagombana nao, moja ya sababu inayonifanya nione poa tu kutorudi.

Kuna siku nilikuwa Zanzibar likizo, wakaniletea hizo hizo za nyoronyoro mambo hayaendi sawa, standards mbovu, usalama hauzingatiwi, maisha ya watu yanachukuliwa poa tu.

Niligomba, niligomba, niligomba, mpaka baadaye nikajistukia hapa watu speed yao ya maisha na standards zao si sawa na za New York City huko ninavyo assume mimi.

Inabidi mimi ndiye nifanye adjustment, nimaona naweza kugomba nikaonekana mimi ndiye mkorofi.

Sasa ku avoid yote hayo ndo nina mute huku tu.

I guess ukikaa muda kidogo unazoea ile hali ila I don't miss that.
watu kama nyie ndio tunawahtaji sana katika bara hili. Lakini nyie ndo kwanza hamjali,mmekimbia na kuendelea kulidharau bara hili. Rudini tuanze ukombozi sasa.
 
Back
Top Bottom