Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

The iron batterfly

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
1,952
Reaction score
2,527
Habari za mida wana jf

Kipindi nakuwa moshi town pale wenyewe wanapaita mji wa wagumu, kulikuwa na matajiri wanajulikana na kusifika sana.
Walikuwa maarufu sana hadi makanisani.Ukienda kanisani ukimwona hata mke wake unabaki waooo
Walikuwa hadi na siti zao kristu mfalme pale.waliishi uzungun,wengine njia ya old moshi.

Kuna siku tumeenda nyumbani kwa rafiki yetu mmoja tulikuwa tunasomanaye mafundisho kanisan maeneo ya uzunguni kule,huo mjumba looh tulibak mdomo wazi.Na ilikuwa first time naona swimming pool nyumban.

Anyway zama zimepita, wengi wameaga dunia,wengine wapo ila umaarufu sio kama zamani.Nilikuwa natoka familia ya kikapuku kabisa so nilitaman siku moja at least na sisi family yetu iweze kuwa na jina kama family zile ama hata visenti tu.

Kuna mzee mmoja alikuwa maarufu sana hapo moshi town,alikuwa na maduka,garages,mabar,mabasi na biashara kibao.Alikuwa anaheshimika kama mfanyabiashara mkubwa moshi.Na wengi tuliamini hivyo.Bwana weeh siku moja katika harakati zake,akapatwa na majanga kwenye mbuga za Kenya, akapigwa risasi akafa,wenzie walifanikiwa kukimbia.Ikaja fahamika mzee alikuwa mwindaji haramu kwenye mbuga ya tsavo,alikuwa anawinda tembo na kuuza pembe na ndio ulikuwa siri ya utajiri wake.

Alirudishwa moshi akaenda zikwa kwao migombani ,after wards Mali zile zikayeyuka kama barafu. Since then nikajifunza kutokutamani cha mtu kwani hujui kakipataje. Utajiri una siri kubwa so vijana wenzangu tufanye kazi.Usiamini story za nilianza na kushona viatu stend,huwa hawasemi ukweli.
 
Kuna wafanyabiashara wengi tu wametajirika kupitia njia haramu wengi tu nawafahamu wameuawa kwa kupiga risasi wakienda kufanya matukio ya ujambazi...
Wengine walikuwa wezi wa magari wakamalizwa
Halafu si wajua wenzetu wakenya walivyokatil walikuwa wakiwakamata hakuna msalie mtume ni risasi tu
 
Kuna mmoja alipata ajali mbaya njia ya moshi-arusha akafa papo hapo. Kilichofuta mali zake zilipukutika kama majani makavu kwa sababu familia yake including mke wake hakuwa anazifahamu mali nyingi za mumewe.
Hahah namkumbuka huyo
Mwengine alikuwa mwizi wa magari Kenya afu anakuja yauza bongo,alikuwa na zinga la mjengo pale town,basi wakatofautiana na mkewe ,akaenda mripot police akakamatwa na kula mvua za kutosha,mwanamke akaolewa na mwanaume mwingine huko Arusha
Nilirudi mwaka juzi mo town nikakuta nyumba imegeuzwa hostel,wanae sasa wameharibika kwan shule waliacha,wanapiga vijiti tu
 
Inasikitisha…

Watoto ndio hupata shida sana kwani wengi wao unakuta walilelewa kama mayai kipindi mamboa kiwa swafi.
Sasa hali inapobadilika ghalfla, wengi wao huishia kukata tamaa ya maisha ikiwa na kukacha masomo yao na mwisho wa siku kuja kuwa watu huni mitaani (umalaya,walevi, ganja,nk).
 
Ndio inasikitisha sana
Vijana wameharibika wale
Dada yao kaishia kuzalishwa na muuza vijit yani tabu tupu
Wakati walikuwa na option ya kusoma shule bora na kutusua
 
Back
Top Bottom