matajiri wa kiarabu wabandikiana kesi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

matajiri wa kiarabu wabandikiana kesi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by rajabu hosea, Apr 6, 2012.

 1. r

  rajabu hosea New Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania, ukitaka kujua rushwa imekithiri kupita kiasi ni kuhusu kesi inayoendelea hivi sasa katika mahakama zetu.
  Kesi hiyo ina husu mfanya biashara ya ngozi za ng'ombe wa anaitwa Salum Ally ambaye anatuhumiwa kwa kufanya biashara ya kuuza binaadamu kwa kuwapeleka katika nchi ya yemen.
  Kesi hii ni ya kutunga ambayo mfanya biashara wa D'salaam anayejulikana kwa jina la mahonda ambaye pia ni mwarabu amenunua vyombo vya sheria serikalini kumkomesha mfanyabiashara mwenzie,walioshindwa kuelewena katika biashara zao.
  ningeomba vyombo vya habari vifanye utafiti kuhusu kesi hii isiyokuwa na hata chembe ya ukweli. kama kuhusu watanzania kwenda kufanya kazi nje ya nchi kwa kutumwa na raia wanaoishi hapa tanzania,wapo wengi sana hivi sasa nchi za nje.
  katika karne hii utawezaje kumchukua binaadamu kichwa kichwa kumpeleka kufanya kazi za kitumwa ,huyo atakuwa mwendawazimu. Naomba serikali ichunguze kesi ambayo inatia aibu kwa watanzania wa sasa kama tunaweza kusafirishwa bila kujua nini tunaenda kufanya nchi za nje.
  ndugu mahonda ubaya unaomfanyia mwenzio ipo siku siri zako zitaanikwa kwa biashara unazofanya hapa Tanzania na matajiri wa nchi za kiarabu ambao wanahusishwa na mitandao ya kigaidi.
   
 2. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Eh makubwa haya!
   
 3. m

  mdoe mchaina Senior Member

  #3
  Apr 9, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu hii kesi ina mkono wa fisadi mfanya biashara maarufu ambaye wapambe wake wana kesi na salimu aliyy aliwakamata na makontena yake ya ngozi amefungulia kesi anawadai fidia sasa wameamua kumtisha kwa kumbambikia kesi na yeye na wamempa shart akitaka kesi yake iiishe afute yao nae kagoma amesema atafia jela akitetea haki yake .
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Uweli ni kwamba hii biashara ya utumwa mambo leo ya kuwachukua vijana [ hasa wasichana] na kuwapeleka nchi za kiarabu wanakowafanyisha kazi za ndani na pia ukahaba ipo, na facilitators wakubwa wa biashara hii ni idara ya uhamiaji ambako pasi za kusafiria zinatolewa. Mimi mwenyewe nimeshuhudia kijana wakike kigori asiyejua kusoma wala kuandika akiomba pasi ya kwenda uarabuni kufanya kazi za ndani, wakati akiomba pasi hiyo alikuwa ameongozana na mwanaume mwenye asili ya kiarabu ambae ndio aliyekuwa anasimamia mipango ya kupata pasi ya kusafiria.. Nikajiuliza kama huyu binti hajui kusoma wala kuandika huko anakokwenda atasalimika kweli? Hata kama hawa wafanyabiashara wana ugonvi wao lakini hii biashara ipo na serikali kwa kisingizio cha vijana kukosa ajira hailivalii njuga tatizo hili la utumwa mambo leo; ni aibu kubwa kwa Taifa tajiri kama Tanganyika!
   
Loading...