Matajiri tuambieni ukweli, acheni longolongo

Matajiri tuambieni ukweli, acheni longolongo

SAFARI YA KUFIKIA UTAJIRI; Maneno ya kutia moyo huwa yako mengi sana utaambiwa''USIFE MOYO,GANGAMALA,
INUKA USITEGEMEE MTU, FANYA JUHUDI UTAFANIKIWA,MTAJI WA MASIKINI NI NGUVU YAKE MWENYEWE''hayo maneno huwa yanatolewa kutoka kwa watu WALIOFANIKIWA kwenda kwa WASIOFANIKIWA,utafikiri kwamba wao walifanikiwa kwa kauli kama hizo!! Matajiri wengi wametajirika kwa KUWEZESHWA,KURITHI,KUKOPA,KUIB
A,KUDHULUMU,KUNYANG'ANYA,KUFIS
ADI na AKIBA ZAO WALIZOJIWEKEA kutokana na vipato vyaoVIKUBWA vyenye ziada,maana huwezi ukaweka akiba kwa mapato madogo upatayo,utakula nini? Utakosa kutajirika HARAKA kama hulipi kodi kwa biashara zako? Sasa mtu hana chanzo chochote kilichiainishwa hapo juu,atatajirikaje!!??? Atafanikiwaje? Hakuna asemaye ukweli kwa jinsi safari yake ya utajiri ilivyopita. Sisi tusiokuwa na nyenzo mngetuacha kwanza! Mnatuvuruga! Wengi ujasiliamali wetu unaish kuganga njaa na kulipa madeni.MILUZI MINGI INAMPOTEZA MBWA!
Kautajiri ni kamchezo na hakahitaji hasira uki punic tu unaishia kutapatapa,kama kuogelea vile
 
Hii mm naipinga.

Mkuu;
Unachokataa hapa ni nini?? Kwamba kwako umasikini ni baraka sio?? Nitakuambia kwa herufi kubwa, UMASIKINI NI LAANA. Hujaona watu wanaliwa na funza wakiwa hai?? Mpaka unashindwa kumtambua kama ana akili au kichaa?? Hiyo kwako ni baraka?? Hujasikia watu wakisema ati kwetu mazao haya hayalimwi?? Hiyo ni nini?
 
Kweli mkuu..ni wanafki mno kwa maneno yao laini...huwa nachekaga mno naposikilizaga story za mjasiriamali Shigongo....uongo mtupuuu!!njoo nyuma ya pazia sasa..
Namkubali sana jamaa,so huwa anadanganya mkuu?unafahamu nini kuhusu yeye?tafadhali nifahamishe
 
Tajiri a nafikiria kuwa tajiri tu. ..masikini ana visingizio chungu nzima. ..utajiri unaanzia ndani yako na unauma kama njaa. .una focus kwenye biashara yako tu. .na unaamini kile unacho kifanya utafanikiwa tu. ..determination. .persistence. ..NA VYOTE HIVI MWANZO WAKE NI NDANI YAKO MWENYEWE. ..waswahili wanasema adui yako mkubwa wa mafanikio yako yuko ndani yako mwenyewe. ..USIOGOPE unaweza. ..
hicho ndo mtoa mada hakipendi afu na wewe umerudia duuuh.
 
Kua tajiri au masikini ni uamuzi wako tu,nitawapa njia 9 za kuyafikia mafanikio ila ni kwa ufupi tu;
  1. Work hard on urself
  2. Leadership
  3. Motivation
  4. Value based decision making
  5. Problem solving
  6. Negotiation skills
  7. Be innovative
  8. Learn idea creation
  9. Creativity skills.
 
For every fortune there is a crime story

Natokea kilimahewa lugha siijui
 
Tajiri a nafikiria kuwa tajiri tu. ..masikini ana visingizio chungu nzima. ..utajiri unaanzia ndani yako na unauma kama njaa. .una focus kwenye biashara yako tu. .na unaamini kile unacho kifanya utafanikiwa tu. ..determination. .persistence. ..NA VYOTE HIVI MWANZO WAKE NI NDANI YAKO MWENYEWE. ..waswahili wanasema adui yako mkubwa wa mafanikio yako yuko ndani yako mwenyewe. ..USIOGOPE unaweza. ..
Wewe ni tajiri?
 
utajiri una mbinu nyingi sana ......unatakiwa ujue mbinu yako ukijua zote utachanganyikiwa
 
Huwezi kuwa tajiri kama huna kifua cha kutunza siri... ya mungu mengi ila ya binadamu ndo zaidi
Kuwa tajiri kunahitaji; uwe na ulinzi wa fedha zako (kiimani zaidi) bila hivyo utaishia na hela za kula na kufanikiwa kujenga vibanda vyako basi hili wengi huwa hawalizingatii kabisa...kuna watu asubuhi hadi jioni ni binadamu wa kawaida usiku ni panya wa kuiba pesa za watu kila duka( reference:Kariakoo na maeneo mengine ya kazi)
 
Back
Top Bottom