Matajiri tuambieni ukweli, acheni longolongo

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,227
157,419
SAFARI YA KUFIKIA UTAJIRI; Maneno ya kutia moyo huwa yako mengi sana utaambiwa''USIFE MOYO, GANGAMALA,
INUKA USITEGEMEE MTU, FANYA JUHUDI UTAFANIKIWA,MTAJI WA MASIKINI NI NGUVU YAKE MWENYEWE''hayo maneno huwa yanatolewa kutoka kwa watu WALIOFANIKIWA kwenda kwa WASIOFANIKIWA,

Utafikiri kwamba wao walifanikiwa kwa kauli kama hizo!! Matajiri wengi wametajirika kwa KUWEZESHWA,KURITHI,KUKOPA,KUIB
A,KUDHULUMU,KUNYANG'ANYA,KUFISADI na AKIBA ZAO WALIZOJIWEKEA kutokana na vipato vyaoVIKUBWA vyenye ziada,maana huwezi ukaweka akiba kwa mapato madogo upatayo,utakula nini?

Utakosa kutajirika HARAKA kama hulipi kodi kwa biashara zako? Sasa mtu hana chanzo chochote kilichiainishwa hapo juu,atatajirikaje!!??? Atafanikiwaje? Hakuna asemaye ukweli kwa jinsi safari yake ya utajiri ilivyopita.

Sisi tusiokuwa na nyenzo mngetuacha kwanza! Mnatuvuruga! Wengi ujasiliamali wetu unaish kuganga njaa na kulipa madeni.MILUZI MINGI INAMPOTEZA MBWA!
 
Tajiri a nafikiria kuwa tajiri tu. ..masikini ana visingizio chungu nzima. ..utajiri unaanzia ndani yako na unauma kama njaa. .una focus kwenye biashara yako tu. .na unaamini kile unacho kifanya utafanikiwa tu. ..determination. .persistence. ..NA VYOTE HIVI MWANZO WAKE NI NDANI YAKO MWENYEWE. ..waswahili wanasema adui yako mkubwa wa mafanikio yako yuko ndani yako mwenyewe. ..USIOGOPE unaweza. ..
 
Hata ukirithi mamilioni kama huwezi kuyawekeza ukazalisha faida na ukaweka akiba faida yako ili kuongeza uwekezaji kamwe huwezi kutajirika. Wako wengi waliopata pesa nyingi sana kwenye madini lakini wakafilisika. Kwa hiyo akiba na uwekezaji ndio msingi wa kupata utajiri
 
Uko wapi ndugu?
Kuna soda hapa toka kwa mganga maisha mwenzako

Alalaye usimwamshe,ukimwamsha utalala wewe ni kanuni sahihi wanayoifuata.Ukiona umeanza kujihoji hivyo jua akili yako imeanza kufunguka.Ndivyo akili ya Afrika na waafrika inavyopaswa kujihoji.

Ni akili ya kipuuzi tu inayoamini kuwa ikilala itaamshwa na waliomka ili iamke,tunaowapuuza wanapotuamsha wanatupenda.Kwa kuwa tunapenda usingizi tunawachukia.

Wachina wana msemo "rafiki mzuri hukufundisha kuvua hakupi samaki". Wengi wetu tunapenda kupewa samaki hatupendi kufundishwa kuvua.

Hatutaki kufundishwa mbinu za kupata mitaji,tunataka kupewa mitaji.Tukipata mtaji hatutaki kufikiri cha kufanya tunataka tunaodhani wanatupenda sana watufundishe kitu cha kufanya.

Endelea kuumiza akili yako ili itumike vizuri utajua wamepataje utajiri,utachagua njia ya kupita.
 
Kama zisingekuwepo vocha ningekua tajiri mie. Dakika,sms na kubwa lao MB. NDIO adui namba moja, bado kuweka heshima saluni kila wiki kuseti,weaving jipya(laki na kitu),rasta za ukwel. Bado sijajipendekeza kwa mashosti kuwachangia sendoff,kitchen party etc(hata za nisiowajua kisa shosti ndo kaleta kadi) bado vikundi vya akina mama uwiii ntatajirika saa ngap?
 
SAFARI YA KUFIKIA UTAJIRI; Maneno ya kutia moyo huwa yako mengi sana utaambiwa''USIFE MOYO,GANGAMALA,
INUKA USITEGEMEE MTU, FANYA JUHUDI UTAFANIKIWA,MTAJI WA MASIKINI NI NGUVU YAKE MWENYEWE''hayo maneno huwa yanatolewa kutoka kwa watu WALIOFANIKIWA kwenda kwa WASIOFANIKIWA,utafikiri kwamba wao walifanikiwa kwa kauli kama hizo!! Matajiri wengi wametajirika kwa KUWEZESHWA,KURITHI,KUKOPA,KUIB
A,KUDHULUMU,KUNYANG'ANYA,KUFIS
ADI na AKIBA ZAO WALIZOJIWEKEA kutokana na vipato vyaoVIKUBWA vyenye ziada,maana huwezi ukaweka akiba kwa mapato madogo upatayo,utakula nini? Utakosa kutajirika HARAKA kama hulipi kodi kwa biashara zako? Sasa mtu hana chanzo chochote kilichiainishwa hapo juu,atatajirikaje!!??? Atafanikiwaje? Hakuna asemaye ukweli kwa jinsi safari yake ya utajiri ilivyopita. Sisi tusiokuwa na nyenzo mngetuacha kwanza! Mnatuvuruga! Wengi ujasiliamali wetu unaish kuganga njaa na kulipa madeni.MILUZI MINGI INAMPOTEZA MBWA!
Maneno Yao ni mazuri, if unafanya biashara seriously kabisa Ukizingatia unafika mbali. MI nilikuwa kama wewe in past year sikuona umuhimu wa misemo but since last year nilivoanza soma books za mafanikio nakagundua misemo mingi explanation zake ziko vitabuni kama sio msomi wa vitabu huwezi elewa Nini namaanisha. Oneday nilisoma kitabu kimoja kilinifungua Sana sales ya kufanya ya kupata wiki nzima nikaanza kupata kwa siku moja. So, naitrust Sana misemo Yao naamini ndio maisha walioyopitia. Issue ni kujituma fanya kazi kwa bidii zingatia misemo Yao utafika mbali. Biashara ni challenge sio lelemama ndio maana wengi wanashindwa na kukata Tamaa wanaona misemo hiyo ni upuuzi
 
Maneno Yao ni mazuri, if unafanya biashara seriously kabisa Ukizingatia unafika mbali. MI nilikuwa kama wewe in past year sikuona umuhimu wa misemo but since last year nilivoanza soma books za mafanikio nakagundua misemo mingi explanation zake ziko vitabuni kama sio msomi wa vitabu huwezi elewa Nini namaanisha. Oneday nilisoma kitabu kimoja kilinifungua Sana sales ya kufanya ya kupata wiki nzima nikaanza kupata kwa siku moja. So, naitrust Sana misemo Yao naamini ndio maisha walioyopitia. Issue ni kujituma fanya kazi kwa bidii zingatia misemo Yao utafika mbali. Biashara ni challenge sio lelemama ndio maana wengi wanashindwa na kukata Tamaa wanaona misemo hiyo ni upuuzi
Kitabu gani hicho? naomba unisaidie na mimi
 
tajiri akienda kanisani anaomba mungu ailinde familia yake na kiipa afya tele. masikini kaz yake ni kulaumu tu. oooh mungu mbona unioni mm kwanini yule tu. mara nimekukosea nini mimi! F.A kasema kuna vingi vya kumuomba mungu kabla ujamuomba utajiri...............
 
Komaa mkuu ukiwasikiliza hao utaingia chaka kila mmoja ananjia zake za kupita kuelekea kwenye utajiri ila usiende tu kwa kalumanzila
 
Ukweli ni kwamba hakuna aliyetajirika kwa njia halali asilimia 100, hawa wakina Bakhresa tunaambiwa sijui walianza kuuza maandazi ndio wakawa matajiri. Hizi ni danganya ulimwengu tu.

Hakuna anayeweza akakwambia jinsi alivyopata utajiri hasa sisi waafrica.
 
Back
Top Bottom