Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 752
- 1,810
Wakati jeshi la polisi mkoani Arusha, likitazamiwa kutangaza hadharani majina ya wauza unga, wabwia unga na wasambazaji, baadhi ya matajiri wameanza kuhaha wakitaka kujua orodha ya majina yaliopo kwenye orodha ya polisi.
Hata hivyo taarifa zilizotufikia hivi punde kamanda wa polisi Charles Mkumbo aliyekuwa atangaze orodha hiyo leo, ameingia mitini na waandishi wa habari kujikuta wamebaki wenyewe ofisini kwake ,taarifa kutoka kwa msaidizi wake, zilidai kuwa kamanda huyo amepata udhuru wa ghafla hivyo zoezi la kutangaza litafanyika kesho saa 5 asubuhi.