Mataifa makubwa duniani yanajiandaa na vita na migogoro ya mwezini

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Katika maisha ya baadae vita zote za duniani kwa mataifa makubwa zitaamia mwezini ambapo ndipo eneo linalokimbiliwa na mataifa makubwa yote .

Unadhani kwanini mataifa mengi yameanza harakati za mwezini tena katika nyakati za sasa ndio zimezidi kwa kasi kubwa sana haswa.

Iko hivi mwezi wetu una hazina kubwa ya mali ghafi zenye madini muhimu na yanayohitajika haswa na wanadamu ili kuendesha viwanda na mitambo yao mbalimbali huku duniani

Mwezi umejawa na madini mengi mbalimbali na yenye thamani kubwa bila kusahau aina za gesi kama vile Helium na hydrogen ambayo inatokana na hazina kubwa ya maji yaliyoganda ambapo kama yakichakatwa basi tunaweza kupata hazina kubwa ya gesi ya hydrogen ambayo hutumika katika vyombo vingi vya anga za mbali kama nishati ya kuendeshea vyombo hivyo .

Kwa uwepo wa oxygen mwezini mataifa kibao yamelenga kufanya mwezi kuwa eneo moja wapo la kimkakati katika suala zima la maendeleo ya viwanda vyao , kwa sasa mbio zao zote ni kwa kila mmoja kutaka kupata uhakika wa eneo kama tu muda utafika kwa wanadamu kuweza kufika na kuanzisha maisha huko .

Mataifa makubwa yatakumbana na Migogoro ya Uchimbaji na uvunaji malighafi hizo katika masiku ya baadae.

Nadhani kama hakutakuwa na mikataba au sheria kadhaa juu ya malighafi za mwezini basi tutashuhudia mapigano makali sana kama tunavyofahamu mara ya mwisho mwezi uliwekwa kama eneo ambalo ni wazi kwa Nchi au taifa lolote kwenda na kufanya chochote ambacho hakitaweza kuhatarisha mustakabali wa maisha ya duniani kwetu tu .

Kama unavyofahamu vita nyingi duniani hapa zilitokana na upatikanaji wa malighafi tu hakuna chengine

Unadhani dunia yetu na mataifa haya makubwa yataepukana na vita kuhusu malighafi za mwezini kwetu .

Kumbuka mwezi wetu unahazina kubwa ya oxygen kuliko inayopatikana hapa duniani kwetu .

Pichani ni Neil Amstrong akiwa amesimama karibu na bendera ya Marekani baada ya kuchomeka bendera hiyo na Mwanaanga mwenzake Buzz Aldrin .

AstronomyKiswahili.

FB_IMG_1695063830941.jpg
 
Write your reply...KUNA OKSEJENI YA KUTOSHA?vp kuhusu maji na hali ya udongo unafaa kwa kilimo?
 
Back
Top Bottom