Kashfa ya Ufisadi wa Escrow ni doa kubwa sana kwa Kiongozi na mtumishi wa Umma yeyote. Ubabe na visasi ni sehemu ya tabia ya Maswi achilia mbali kashfa ya Escrow.
Inakuwaje mtuhumiwa huyu na mbabe huyu anakabidhiwa idara muhimu ya kukusanya Fedha za Umma? Anapata wapi moral justice ya kusimamia uadilifu? Atamwambia nn mtumishi aliye chini yake juu ya rushwa na Ufisadi?
Hivi hakuna kabisa wataalamu wengine katika nchi hii?
Tusitarajie jipya kutoka kwa mtu huyu, zaidi ya kashfa, ubabe na visasi.
MH. RAIS MAGUFULI KAMA KWELI UNATAKA UFANISI KATIKA SERIKALI YAKO ZINGATIA HILI.
UKWELI HUU UTAKUMBUKWA.
Huyu ndugu si mtuhumiwa tena, uchunguzi ulishafianyika na kama inavyotakiwa watuhumiwa aidha husafishwa au kupatikana na hatia, huyu pamoja na Muhongo hawakupatikana na hatia, hii ni rekodi iliyopo bungeni, (ansadi). Sasa uondoe (withdraw) hiyo kauli ili mambo yawe sawa bila kuwa emotional.
Tena, huyu ndubu ni kaimu naibu kamishna, yaani, kwanza yupo kwenye majaribio, hajahakikishwa (confirmed) katika hiyo nafasi, lakini, ni naibu kamishna mkuu, kamishana mkuu yupo! sasa ataiharibu vipi kwa nafasi ya number 2?
Kuhusu ubabe, yaweza kuwa ni hisia au mazingira yaliyopelekea wewe kuhitimisha hayo, kumbuka kwamba hawa wenye nafasi kubwa wanapewa malengo mahsusi ambayo wanatakiwa kuyatekeleza bila mikwamo, sasa kama alikuwa anasukumwa kufanya jambo na bosi wake usitegemee atakuwa compromizing.
Watu wengine wa kufanya hayo majukumu wapo lakini huyu ameonekana ana special features ambazo mheshimiwa rais anazitaka, na alifanya kazi nzuri sana TAMISEMI na Nishati na madini, achana na maamuzi ya siasa mbaya zilizo muwajibisha, kiutendaji, not many can match his performance.