Ni uelewa tu, tume ya maadili ilifanya uchunguzi wa kina na kugundua kwamba Maswi hakuhusika na kashfa ya escrow. na hata katika list ya watu waliopata mgao yeye hakuwemo, kwa nini apate adhabu. Haiwezekani mtu awe mhalifu kwa tuhuma, na kama ikibainika hakuhusika ni kwa nini aadhibiwe. Chuku binafsi tuzisipe nafasi kwa manufaa ya nchi yetu.
Wait a minute! Tume ya maadili ipi? Tume hiyo unauoiita ya maadili ni clap na sehemu ya matumizi mabaya ya fedha za umma. Hata chenge mzee wa visenti aliwaambia walipomuita kumhoji kuwa ninyi ni cha mtoto hamna uwezo huo, uchafu ni uchafu hata kama umetiliwa mashaka tu hufai kuendelea ku-serve in public office
Mimi binafsi sikubaliani na magufuli juu ya uteuzi wa huyo mtu na wengine kama prof muhongo na wenzake majina mnawajua ambao tulisha wajadili kwenye thread nyingi tu humu JF. Nyie mnaoshabikia humu eti jembe nina wasiwasi na viwango vyenu vya elimu na uelewa wa maadili ya uongozi.
Katika nchi inayofuata sheria na miiko ya utumishi wa umma haiwezekeni na wala haingii akili ni kwa Mtu au watu waliothibitishwa na vyombo kama;Bunge,Takukuru na CAG
Kuwa wamehusika na ubadhirifu, rushwa na matumizi mabaya ya ofisi na kuthibitishwa beyond no doubt na baadhi yao wakalazimika kuachia nyadhifa zao kwa tuhuma hizo leo hii tunawateua kushika nyadhifa aidha hizo hizo au nyingine kubwa sehemu nyingine! This is unspeakable.
Halafu mnadiriki kusema eti ni JEMBE! REAL! IS THIS SOME KIND OF A JOKE! hivi kweli magufuli au serikali inapeleka picha gani kwa wananchi! au ile kamati ya bunge (off course bunge lenyewe) kama mhimili wa serikali, CAG na Takukuru! .
Kama rais anaamini kuwa wote acha huyo wa kodi hawakua na hatia hiyo guts ya kuwafanya wasafi na kuwa appoint imethibitishwa wapi na chombo cha kisheria na umma (general public ) ikaambiwa kuwa hawa hawana hatia na baadala yake wenye hatia ni so and so na halafu sheria ikachukua mkondo wake! WHERE AND WHEN? CAN SOMEBODY EXPLAIN! . Ni tume juu ya tume, kamati juu ya kamati, uchunguzi juu ya uchunguzi then inaishia hewani, na ku register scandal baada ya scandal lakini hakuna matokeo chanya yoyote. Watawala wanaendelea kuneemeka watawaliwa wanaishia kulalama life goes on.
Mwl nyerere katika one of his hotuba alitoa mfano wa waziri mmoja huko uingereza kama si kosei alishutumiwa kutembea na changu doa na baada ya kuandikwa sana akajiuzuru na kumuandikia waziri mkuu barua na according to mwl nyerere yule waziri mkuu hata hakumjibu yeye aliteua tu waziri mwingine. MORAL OF THE LESSON ni kwamba unapokua mtumishi wa umma haswa nafasi kuu zenye kuamua mustakabali wa nchi kuna miiko ambayo ukiiivunja inakuondolea sifa ya kuwa kiongozi. HUFAI
Nawasilisha nitarudi tena.