Maswali yanayonitatanisha..........

Preta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
24,320
Reaction score
18,887
Unakutana na mtu anakuuliza.....hivi bado upo.....?.....swali gani hili.....kama nimekufa si ungesikia.......au labda kazoea kukuona mara nyingi unapokuwa na shughuli zako unapiga misele na gari....siku ya siku akikutana na wewe ukitembea....unasikia....alaaah leo mbona upo kwa miguu....jamani....mtu umezaliwa na gari......?
Au unamuuliza mtu.....kitu kama.....kesho utakwenda....anakujibu....nani mimi....?......aggghh......inachosha sana.....
HEBU ONGEZEA MASWALI YANAYOKUTATANISHA..........
 

hahahaha,,......waswahili wanausemi wao wanasema ubinadam kazi,,....ndo ivyo twatakiwa kuvumiliana mydear,,...!!
 
Hata mimi huwa nakerwa sana na maswali haya!
 
mie nakerwa na umenipendea nini
yaaani au mwingine anakuuliza umempendea nini
 
Unanikuta naangalia muvi, afu unaniuliya tena, He! Unachek muvi!
Unategemea nikujibuje!
 
^^
Mwingine anakurupuka tu,,msalimie wifi angu wakati anajua kabisa uko single.
Aaaa!
^^
 
^^
Mwingine anakurupuka tu,,msalimie wifi angu wakati anajua kabisa uko single.
Aaaa!
^^

yah.....hao ndio wale wanaokuuliza.....shemeji hajambo......na hakufahamu kivile kama una huyo shemeji au lah.........hapo unakuta ndio kwanza umetoka kupigwa kibuti
 
"Hallo, uko wapi?"
Hahaha....hata salamu hakuna waanza na swali upo wapi, kwani wewe ni GPS?
 
"Shemeji hajambo?"...
Hapo umekutana na mbulula asiyekufahamu wala humafahamu...
Na huyo amwitaye shemeji, ni dada yako tumbo moja...kisa tu kawaona mnaongozana pamoja basi kashaashumu ninyi ni wapenzi...
 
Mtu anapiga simu anaanza kuuliza 'unafanya nini' ukimjibu naongea na wewe kupitia simu anachukia... aaah sasa sijui wanataka majibu gani
 
Juzi kati kuna msiba umetokea mdingi mmoja kafariki....
baada ya mazishi binti ake akaiwasha simu ya marehemu mara ikaingia msg
"mzee kuna habari nimezisikia ni kweli'?
tulicheka sana sasa mtu kafariki anatuma msg kuuliza kama ni kweli teh...
kituko kweli!!!!
 
watu hamjawasiliana muda mrefu siku akikupigia anaanza kuuliza mbona kimya? ooh umenichunia?!! wewe mwenywe ulikuwa wapi cku zote hizooo!!!!
 
unakutana na mtu anakuuliza mbona umekondaaa!!!? aaah jamani hamjui watu tunamaintain figure. lol
 
anapiga simu anauliza naongea na nani kwani umempigia nani
 
Mtu anakupigia simu usiku...umelala?
Jibu:hapana nachoma mahindi.

Upo macho?
Jibu:hapana najaribu kufa
 
Hehehehe hii imenivunja mbavu sijui kweli au imetungwa
 
Hivi juzi niko na my wii, akanitambulisha kwa rafiki yake.
My wii: Rafiki huyu wifi yangu, mdogo wake mume wangu.
Rafiki: Hee mbona mumeo mweusi sasa alafu mdogo wake mweupe??!!

Mweeh ilibidi tu mi nicheke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…