• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Maswali yanayokutatiza - 2

salimkabora

salimkabora

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2012
Messages
2,445
Points
1,225
salimkabora

salimkabora

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2012
2,445 1,225
TUKIO: Samaranta binti mzuri aliondoka chuoni kwake jioni moja kwa kusudi la kwenda kumfurahisha mzee mmoja jirani yao, ambaye amekuwa akimtaka kimapenzi kwa ahadi ya zawadi kemkem. Haikumchukua muda kufika kwenye hoteli waliyokubaliana na kumkuta mzee kajaa tele chumbani na baadhi ya vivazi keshaanza kuvipunguza. Samaranta hakutaraji kama mzee atakuwa moto kiasi hicho kwani alitaka wapoteze kwanza muda, saa ya kuondoka ikikaribia ndio amuonjeshe kiduchu. Kimsingi alikuwa na mahitaji mengi ya pesa lakini hakuwa tayari kumfanya mzee afaidi sana kwani wala hakumpenda. Binti akazugazuga na orodha zake za mahitaji kwanzaaa na alipohakikishiwa kupata vyote ndipo alianza kuvua nguo kivivuvivu.

UCHAMBUZI: Hakuna kufanikiwa katika maisha bila kutoa. Huwezi kuvuna bila kuiachia mbegu ardhini. Lazima upande wazo kisha uvute taswira ili kuvuna uhalisia. Ukilenga kupata kabla ya kupanda chochote au kuvuna kwa wingi mahali ulipopanda kidogo utakuwa unajiongopea, maana yake mambo yatakuendea kinyume kabisa na unavyotarajia.
Kutoa sio lazima iwe pesa au vitu vya thamani. Kumfanya mtu atabasamu kwa jambo au neon zuri ni kutoa na kufanya hivyo unaitia nguvu sumaku yako au unaimarisha lokali yako. Sasa ulaghai anaoufanya binti hautamzalia mazuri. Anaweza akapewa hizo pesa zikaenda kumuua mbele. Anaweza kuchukua mchumba wa mtu na kwenda kumstarehesha na huko akachomwa kisu. Anaweza kununua gari halafu akapata nayo ajali akawa kilema.Yeye anataka kumpa mzee kidogo lakini yeye avune mengi. Huo ni ubongo mchafu na roho ya mashetani inayomwangamiza mhusika.
Si kama nahalalisha hayo ya zinaa wanayofanya, ila nalizungumzia jambo lenyewe kama lilivyo na mikingano yake. Mkataba ni mkataba tu hata kama ni wa kidhalimu, lazima uutendee haki kwa maana ni kifungo chako mwenyewe. Tayari umeshapata malipo ya uovu wako kuiendea zinaa, lakini bado inakubidi utekeleze misingi yake kwa haki. Huwezi kusema kwa kuwa ni zinaa basi hata kinyume na maumbile ni sawa. Sheria na taratibu ziko palepale ukizidisha inakula kwako na ukipunguza unaiendea toba na inakuwa nafuu kwako.
Riziki ya mwanamke ipo mikononi mwa mwanaume na jinsi ya kuipata imeainishwa katika sheria ya Mungu ya mahusiano. Inampasa mwanamke kuiachilia sumaku itakayovuta riziki zake toka mikononi kwa mwanaume na si vinginevo. Nguvu ya sumaku husika ndio itakayoswichi riziki za mwanamke toka kwa mwanaume pasipo hata kutoa kwanza mlolongo wa maelezo.
Pale kwenye bustani ya Eden Mungu alimuweka Hawa mbele ya Adam ambaye aliweka vipimo vyake ili kujua stahili zake. Baada ya kuridhika na alichokiona ndipo akayathibitisha majukumu yake mbele za Hawa. Hivyohivyo haimsaidii mwanamke yeyote kujipigia mahesabu yake mwenyewe kwa binafsi yake akachune vipi wanaume. Mchuno wakweli na hakika ni ule ambao mwanaume ataridhika nao mwenyewe katika nafsi yake kuuachilia kulingana na sumaku ya mwanamke inayomfikia.
Hakuna utapeli wala ujanja ujanja katika hili. Kununuliwa gari, halafu uwape wamaume wengine waendeshe au kufanya nao mapenzi humohumo ni ujanjaujanja unaoangamiza tu. Kumlaghai mwanaume akujengee nyumba halafu unaingiza wanaume wengine kustarehe nao humo ni ujanjaujanja wa kiwendawazimu tu. Bwana huyohuyo unayemuona mali atabadili nyaraka zako za umiliki wa nyumba halafu atakupeleka bafuni akukabe ufe. Ndugu wakiibuka wakisema nyumbani ni ya ndugu yetu, anawaonesha nyaraka nyumba alijenga yeye.
Unapoishi ubaya na udhalimu hiyo ndiyo inakuwa taswira moyoni mwako na yule mkuu wa uzalishaji katika kiwanda chako anachukulia ya kwamba hiyo ni oda inayohitaji kutengenezwa na kukabidhiwa katika uhalisia wa maisha yako. Ufahamu wako wa ndani hauulizi maswali wala kubishana na wewe.- Imetolewa ktk gazeti la Imani Weekly @ www.quasserer.com - Email: quasserer4me@yahoo.com
 

Forum statistics

Threads 1,405,649
Members 532,072
Posts 34,491,930
Top