Maswali yalioninyima usingizi nilipokua mtoto

Baba alinunuaga viatu flani kama vya Kungfu nikaviiba kupeleka kwa fundi avipunguze nivivae mimi fundi akasema haiwezekani.

Niliwahi kuchukua saa ya baba nikaivaa mguuni kwa sababu mkononi ilikuwa haitoshi (inapwaya).

Niliwahi kuweka maji kwenye kibatari nikidhani itakuwa kama mafuta ya taa.
 

Hahaahaaa.....
Mama alitembea juu ya maji kama yesu
 

Viatu viliitwa kunfu shoes
 

nimecheka mpaka mbavu sina.utoto raha sana pia kharaha
 
Niliamini kuwa kitu kikipotea unatema mate kwenye kiganja cha kushoto unayachapa na vidole viwili vya kulia yatakakoelekea ndiko hicho kitu kilopo.2 Mdudu akiingia machoni unatema mate juu mara tatu au nne na mdudu anatoka,kweli utoto raha.
 
Niliamini mtu akijikwaa alafu kesho yake akirudi maeneo alipo jikwaa lazima ataokota hela
 
Mi nlikua najiuliza watu wanoonekana kwenye tv wanapitia wapi? Mana tv ndogo lkn watu teleee

Siku moja nlimuuliza mama mtoto anazaliwa vp akanambia anatolewa mdomoni.

Hahahaha yani kama mimi enzi hizo..watu kwenye tv walikuwa wananipa mawazo sana jinsi ya kuwatoa ndani ya tv waje tule.
Mimi nilimuuliza mama yangu mtoto anatoka wapi akaniambia wanauzwa.nikawa sitaki midoli nataka na mimi nipelekwe sokoni kununua na mimi mtoto wangu maana mama alikuwa ananizuia nisimbebe mdogo wangu
alikuwa bado mchanga.
 
Mimi
  1. Nilikuwa nakataa na staki kuamini kama nilizaliwa, nilikuwa nadhani nilikuwa tu hivyo hivyo
  2. Nlikuwa najiuliza kwa nini wavulana walikuwa wanafanyiwa circumcision na wanafanyiwaje na ili iweje?
  3. Nlikuwa najiuliza kwa nini nikiwa kwenye gari miti nyumba na vitu vingine vinatembea kurudi nyuma?
 
nilikuwa nikiona magari madogo naamini sikumoja nayo yatakuwa makubwa
 
Mimi kuna vitu vingi. 1. nilikua nikijiuliza hivi nitapataje uhakika kuwa mtu au watu flani wanaendelea kuwepo vile vile kama walivyo wakati siwaangalii. Nilihisi nikiona mtu halafu nigeuke anaweza akawa kabadilika na hayuko vile tena, sasa nitaprove vipi kuwa mama ana baki kuwa mama hata mda ambao simwoni!

Nilikua sipendi kula na nikawa nalazimishwa sana, nikatengeneza idea kua hawa watu labda wanataka ninenenpe ili wanile, maana sikuona faida kwao ni nini ya hadi kunichpa nile eti!
 
Nilikuwa nikimwambia mama naumwa tumbo ananiambia ka.nye, sikujua kama kuna dawa ya tumbo. Kuna siku nilimsikia untie yangu anaulizwa ujauzito huo ulionao umeupata wapi akajibu NILITEMBEA na Fulani, ilinisumbua mno sikujua walitembea aje hadi apate mimba.
 
Nina ndugu yangu alikua akivua nguo kujiandaa wa kuoga anajificha balaa chumbani halaf akishavua anapita uchi vizuri tu mbele ya watu.
Alikua anafikiri swala ni kujificha kwenye uvuaji na sio utupu wake.
 
Nilishawahi kupata kwenzi hilo sitasahau kutoka kwa mjomba kisa nilikua naimba "embe dodo embe dodo limelala mchangani.." aisee hehehe sikuelewa mpaka kesho kwanini.
 
nilikua najiuliza, inakuaje unakula chakula vizuri lakn knatoka tofauti (kinyesi), nikaambiwa knameng'enywa, saasa knaswagwa vipi, nikawa nabonyeza tumbo nione labda kuna kijimashine Ndan ya tumbo, km zle za kukobolea mahindi.

Matangazo ya Always (pad), nilikua siyaelewi kabisaaa, siku nipo kwa uncle, saa 2 wote sebuleni tunaangalia Itv, nikauliza "eti mjomba zile ni nini", dah nkafukuzwa "mtoto mdogo una maswali kama polisi". Nikajiuliza kwan kuna shida gan si wangenijibu tu, nilikua nahisi ni chakula, ila mbona hawazili sasa.
 
1. Nilikuwa nikisimama kwenye stuli nilingane na baba naona kizungu zungu, basi nikawa naona urefu sio dili maana unakuwa unaona kizungu zungu
 
me nilimuuliza bibi kuzini ndo nini? akaniambia we mtoto funga mdomo wako!

Hivi umasikini huu wa Tanzania mpaka lini?
Shule za tech zinapokuwa za mwisho, hivi kuna mpango wa kuwekeza kwenye sayansi nchi hii?
 
nilikua naamini ukishan'goa jino lazima utupe juu ya bati ili kunguru alile then ndo liote tena
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…