mankachara
JF-Expert Member
- Sep 27, 2013
- 6,161
- 3,496
Kuna baadhi ya mambo yalinifanya niumize akili enzi za uto to
1- mtu akivaa overall (kanyela mumo) anakunyaje?
2-mama akienda kujifungua, je mototo hupitia wapi kutoka tumboni?
3-baba na mama, walizalia pamoja?
4-mwalimu ndie mtu mwenye akili kuliko watu wote?
5-rais ndie mwenye nchi?
Ongezea maswali yalio kutatiza utoton
na ccm ni nafasi hizo tu eeeh, makamo mwenyekiti bara pwani?, katibu mwenezi bara pwani? kurugenzi nyengine zote ndani ya ccm pwani? jumuiya za chama ya vijana wanawake na watu wazima ? pwani
huachi wewe?
suala la kuzungumzia katiba masuala ya zanzibar na bara vyama vyote viko hivyo kwa sababu hii ni jamhuri ya muungano wa bara na zanzibar, hata cCUF iko hivyo na nnategemea hivyo kote njoo na hoja nyengine
nilipokuwa mdogo nilimwambia mom akaniokotee mdogo wangu baharini akawa ananizungusha tu(mi wa mwisho)
2 mbinguni kupoje je kuna nyumba na watu wanaoishi huko
3 nilimwambia mom kwanini asimbadili kaka angu mmoja kuwa dada nina kaka sita afu sina dada kakaangu nilieombwa abadilishwe kuwa dada alinipigaje tena ndo alikuwa anabalehe kipindi hicho mimi nilikuwa la kwanza lol
Na ikifika usiku unaificha "simu" yako!!!
Mimi sikuwahi kuwa na maswali yasiyo na jibu. Nikijiuliza swali natengeneza na jibu hapo hapo. Nilikuwa najua for sure mimba inapatikana baharini, chini ya mnazi. Mwanamke anasimama anaegemea mnazi, halafu mume anamshika tumbo anamuambia uwe na mimba ya mtoto wa kike. Afu wanarudi nyumbani (sikujua kama kuna kufanya 'matusi')
hilo #2 umeshapata jibu..
hahahaha umeona eeeh hata ukiiba ina alama huchelewi kukamatwa
Ha ha aaaaaa alama tukiita "sain" yaani utoto!!!!
hahahaha umenifanya niwakumbuke rafiki zangu wa utotoni u know
Ndio vizuri umkumbuke mpaka yule aliyekuwaga baba wewe ukiwa mama!!!!!
1.mimi nilijiuliza saana kuhusu kioo,nilidhani ni watu 2 sasa nikigusa upande wa nyuma wa kioo nakuta hewa tu.2. kwa nini baba analala na mama tu3. Mbinguni kuna raha,nilikua najiuliza raha hiyo ni zaidi ya kucheza sundayschool, au kula pilau
Utoto shida et zamani ukiweka sindano au wembe kwenye njia ya treni, tren inaanguka..ila baadaye ikawekewa sumaku ya kuvuta sindano na nyembe!!
Ndani ya redio, nani anakuwemo kutoa sauti?
siku moja nikiwa na mama mahali kwa rafk ake,kukawa na dalili ya mvua,mama akanambia kimbia nyumban mvua inakuja,basi nikaanza kukimbia,sijafika home mvua ikaanza,sasa on way to home kukawa na kidimbwi cha maji barabarani nilipofika pale kuchungulia hv nikaona ina reflect anga,so mi nikajua ni shimo reeeeeeeeeefu saaaana,basi nikawa nalia tu pale nimeshindwa kuvuka,mama kufika nikaona anaingia tu heeeeeeeh nilipigwa butwaa mbona hazami? hadi leo huwa nacheka tu nikikumbuka