Muhimu ni kuepuka kumdanganya. Wakati mwingine mtoto anataka kulinganisha jibu lako na lingine alilopata mahali pengine, ukimdanganya baadaye akijua kwamba ulimdanganya atakosa imani nawe. Vile vile hakuna sababu ya kumfafanulia kwa kirefu. Waweza tu kujibu kwamba wanazaliwa, sio lazima ufafanue wanazaliwaje. Akiuliza wanazaliwaje, mwambie akikua ataelewa. Ila kwa mtoto wa umri kuanzia miaka 8, anajua kila kitu, anafaa kuanza kupata elimu ya uzazi. Utafiti umeonesha hivyo.