- WANAMABADILIKO;
Watanzania wamechoshwa na Rushwa, wanachukia UFISADI, Mzee unamkakati gani dhidiya wala rushwa na mafisadi..?
(Una maanisha mafisadi waliopo saiv serikalini au wapya watakao jitokeza mbeleni?Manake wala rushwa na mafisadi waliopo saivi ni matokeo ya kukosekana kwa uwajibikaji wa watawala jambo ambalo mzee amehaidi uwajibikaji utapewa kipaumbele na hilo linafahamika anaweza hata kabla hajaomba ridhaa ya kuongoza nchi)
- MAMA NTILIE;
Kilio chetu ni juu ya mgambo kutusumbua na mazingira mabovu ya biashara,tukakulalamikia bei kubwa ya vyakula na mazao, jibu letu liko wapi..?au atakuja kutujibu Babu Seya ukishamtoa jela..?
(Kodi za kilimo na mifugo zimefutwa hivyo bei itakusha,kwa kutumia katiba ya wananchi,mgombo hawatakua tena na namna ya kuwasumbua sio ninyi tu,ila kila raia wa nchi hii.Kuhusu mazingira mabovu ya kibiasha,ndiyo maana nilichukua hatua ya kuwatembelea,nimeona nipeni kura nitarudi hapohapo na mkakati kazi wa suala hilo,usinielewe vibaya,babu yesa nimesema kwa wakati muafaka atatolewa kwa kufuata utawala wa sheria)
- MADALADALA;
Mzee tulikubeba kutoka Masaki mpaka Gongo la mboto, njia nzima tukikueleza kero zetu, Hatujakusikia ukisema kitu kuhusu usumbufu wa Traffic na kutunyang'anya leseni zetu..?
(Nilipanda daladala kujionea adha mnayopata,tariffic nimeshawahaidi nyumba bora na maslahi bora,hilo litawafanya wasiwe na njaa ya kuwasumbua tena,)
- WAKAZI WA DAR;
Mzee tumekupa mapokezi ya kufa mtu, lakini unajua kuwa tumeamka saa kumina moja alfajir ili kuwahi mkutano wako wa saa tisa Jangwani, Tatizo la foleni na shida ya Usafiri haujazungumzia kabisa...Mzee umetusahau..?
(Ondoa shaka,mimi mwenyewe nimeishi kwenye hili jiji kwa muda mrefu,japo wakati mwingine mimi hupita kwa vingora,nimeshafanya ziara kwa daladala nimejionea mwneye na nimesema maendeleo yetu sio suala la kisekta,ni la sekta zote ikiwepo ya barabara,jibu sahihi la msongamano wa barabara nipo kwangu,nipe kura yako)
- WANAFUNZI;
Elimu bure kutoka shule ya msingi mpaka chuo kikuu, sawa ila Mzee kwa mapato gani..? Au ndio muendelezo wa maigizo..?
(Kwa kupunguza safari za raisi lukuki nje ya nchi na msafara mkubwa wa watu wasiokuwa na tija,kupunguza manunuzi na matumizi ya mashangingi kwa viongozi wa umma wakati wanaishi masaki ambapo barabara ni nzuri,nitawanunulia toyota vitara,kuthibiti mianya ya rushwa na ukwepeji kodi,sekta ya madini na gesi kutumika kuchangia elimu yenu)
- WACHUMI;
Sarafu yetu imeendelea kushuka kwa kasi ya ajabu, imetoka kuwa hela ya madafu imekuwa hela ya pipi, Mzee na hili nalo umelisahau..?
(Niwape pole watanzania kwa hali hii iliyosababishwa na CCM,shillingi yetu itaimarika kwa kasi sana kama tukiimarisha uchumi wa ndani,kwa kuanza kusafiriza bidhaa vingi zaidi nje na hili litafanykia kupitia viwanda vya usindikaji nilivyowahaidi kuwa nitavianzisha.Tutapunguza uingizaji wa vibadhaa kutoka nje ambavyo vinaweza kutengenezwa hapa nchini hasa za samani,hivyo tutaweza kuimarisha shilingi yetu na uchumi kwa ujumla)
- WANASHERIA:
Nini maana ya utawala wa sheria unaouzungumzia..? ipi haki ya watoto waliolawitiwa kinyume na maumbile na Babu Seya na Wanawe, au Mzee unaujua Ukweli ambao hautaki kutuambia..?
(Utawala wa sheria ni utawala unaofanya mambo yake kwa kufuata katiba ya wananchi,sheria na taratibu za nchi,kwa maelezo zaidi rejea somo la uraia darasa la nne,kuhusu babu seya,kuna mengi yanasemwa lakini utawala wangu hauna lengo la kuingilia muhimili wa mahakama ndo maana nimesema kwa kufuata utawala wa sheria na kwa wakati muafaka hilo litafanyika)
- WAZANZIBARI;
Ni upi msimamo wako na maoni yako juu ya Katiba inayopendekezwa..kuwa Muwazi..?
MZEE hauoni tofauti ya maisha ya Wazanzibari kabla na baada ya kufungwa kwa Farid na Kundi lake..? Mzee amani imerudi Zanzibar au tuambie mahusiano yako na UAMSHO..?
(Msimamo wangu ni kama nilivyosema,nchi hii inahtaji katiba ya wananchi,sio katiba ya watawala,kuhusu kundi la uhamsho,uhusiano wangu na wao upo kwenye misingi ya haki na utawala bora,kwa mantiki hiyo hili kundi lina haki ya kupata haki kwa msingi uleule wa utawala wa sheria)
- WAGONJWA;
MZEE watanzania wenzako tunaumwa Mzee..,Nini Hatma ya Afya za Watanzaniaau WEWE mwenzetu sio mgonjwa..?
(Hujaeleweka,ni watanzania wote ndo wanaumwa au?hatma ya afya za watanzania zipo mikononi mwao,kwenye kadi zao za kupigia kura,tuiondoe CCM madarakani na kama ilivyohaidi kwenye ilani,wananchi mtapata bima ya afya nafuu,tutajenga hospitali za kisasa kuepuka watu kwenda nje kutibiwa na kama alivyosema mgombea mwenzangu duni,tutaimarisha afya ya mama na mtoto na kutoa lishe bora)
- WANAMABADILIKO;
MZEE tuliahidiwa SLAA atahudhuria jangwani na kuipa nguvu mpya kasi ya mabadiliko, Mzee mlimsahau au ilikuwa ni Changa la macho..?
(hiyo siyo ssehemu ya ilani ya chama changu na sio hitaji la watanzania kwa sasa,pamoja na hilo mimi sio msemaji wa mambo ya ndani ya chama changu)
- VIJANA;
MZEE ulisema tatizo la ajira ni bomu, ila hatujakuelewa, ina maana umetuacha tulipuke au mkakati wetu uko kwa Balal..?
(nimeshaeleza tena kwa kirefu sana,mikakati ya kuongeza kasi ya upatikanaji wa ajira kwa vijana ikiwepo kuanzisha viwanda kupatua kilimo na ufugaji,kupunguza kodi kwenye sekta zinazoongeza ajira ili kuchochea ukuaji na kupitia uanzishaji wa vyuo vya ufundi fursa za kujiajiri zitaongezeka zikichakizwa na utoaji wa mikopo ya riba nafuu kwa vijana)
- WANAKIJIJI;
MZEE umetukomoa au umefanya kwa bahati mbaya kutuwekea hotuba yako kwenye Intaneti, haujui zaidi ya watanzania asilimi 80 hawajui kitu kinaitwa Intaneti..?
(Ninyi huko kijiji ondoeni shaka,ndo nimezindua tu leo kampeni nitakuja huko nitaongea na ninyi na mtayapata yote yaliopo kwenye ilani yangu live)
- WATUMISHI;
MZEE, mishahara yetu haikidhi mahitaji, gharama za maisha ni ghali mno..mbona hatujakusikia ukitutaja, au sisi ni mpango wa kando..?
(Ilivyo hata ukipandisha mishahara mara kumi,kama uchumi wa nchi umedorora bado mshahara huo hautawatosha,laikin tukiimarisha uchumi kwa kuanzisha viwanda,kupanua kilimo na ufugaji,afya,maji na elimu hata mshahara unaopata utakuwa na uwezo wa kuwasaidia,sina nia kuwa sitawaboreshea maslahi,hapana ndo maana nimewataja walimu na wafanyakazi ya sekta ya afya,hapo ni pa kuanzia tu,)
- WACHUMI;
MZEE, nini hatma ya mchumi mwenzetu Prof Lipumba katika genge la wanamabadiliko, au umemchukua TAMBWE Hizza Mhitimu wa darasa la saba kuwa mbadala..?
(sio sehemu ya ilani wala halina maslahi kwa watanzania)