samsun
JF-Expert Member
- Feb 9, 2014
- 7,386
- 5,962
Habari zenu wakuu.
DIAMOND au ALIKIBA Unamkubali nani DIAMOND au ALIKIBA Ungependa kufanya kolabo na nani kati ya DIAMOND au ALIKIBA ..........Nyimbo za nani unazisikiliza sana kati ya DIAMOND au ALIKIBA ........... Uimbaji wa nani unaupenda zaidi kati ya DIAMOND na ALIKIBA .............Ungependa uwe na mafanikio kama ya nani kati ya DIAMOND na ALIKIBA.........Wewe unafikiri bifu la DIAMOND na ALIKIBA linawaathiri vipi nyinyi wasanii wadogo .............. Ungependa uwe na menejimenti ya namna gani, kama ya DIAMOND au ALIKIBA ........... Ungewashauri nini kati ya DIAMOND na ALIKIBA ?
Hayo ni mengi kati ya maswali ambayo utegemea kuyasikia msanii yeyote kuulizwa na hawa watangazaji wetu wa dot com. Anakuja/unamuhita msanii studioni muda wote una muuliza kuhusu KIBA na DIAMOND,humuulizi kuhusu muziki wake na kama utamuuliza basi kati ya maswali 20 utakayouliza basi 15 ni kuhusu DIAMOND na ALIKIBA direct or indirect lazima itawahusu hao wawili kwanini jamani?
Pengine maswali sio mabaya, lakini kwanini msanii atakiwe kusema kati ya hao wawili .... kwani TZ wasanii ni wao tu .......... na ukimtaja tofauti na hao wawili (DIAMOND na ALIKIBA) maongezi yanakuwa mafupi na hata shamrashamra ya kukuuliza inawapungua.
Nikisema kati ya watu wanaolitengeneza hili linaloitwa "bifu" ni hawa watangazaji wetu wa 4g lte nitakuwa nakosea?
Na ikitokea ukasema namkubali fulani sikiliza maswali yanayofuata:
Inamaana fulani (DIAMOND/ALIKIBA) hajui kabisa kwa jinsi unavyoona wewe?
Sasa mbona ana tuzo kibao tu,ina maana anatoa rushwa?
Mtu kapewa hadi mkataba na kampuni kubwa kabisa,inamaana wameingia chaka?
Ina maana hata wewe (DIAMOND/ALIKIBA) hakufikii?
Na maswali yatazaliwa zaidi kama unayemfagilia wewe ndio wanaompenda wao na utaulizwa zaidi maswali ya kumchoma yule unayemponda.
Kwa kweli mimi kwa upande wangu huwa wananiboa kwa kweli,na baadhi ya wasanii wasivyojua kujieleza ndio shida kabisa wanavyoulizwa ndivyo wanavyojibu bila ya kujielewa.
Huwa nampenda Vanessa akiulizwa maswali yasiyomuhusu yeye anasema,niulize kuhusu mimi na muziki wangu hayo mambo ya nani zaidi kwangu hayana nafasi.
Na mara nyingine ukimuuliza KIBA na DIAMOND kwako nani zaidi anakwambia zaidi ni mimi.
Sasa nimeona niongelee hili na wenzangu kama mnaweza kuongezea au kupunguza au kurekebisha basi uwanja ni wako.