FaizaFoxy sijapiga porojo bali nimeuliza maswali yanayonisumbua mimi mwenye ubongo mdogo usioweza kufikiri kwa kina. Nakuamini sana kuwa wewe ni genious utaweza kutupatia majibu sisi wenye akili ndogo.
Kwa hiyo huoni kuwa akaunti ya ESCROW imefunguliwa baada ya anayoihita ICSID - 1 kuamua na kwa jinsi hiyo haina mahusiano na maamuzi hayo kama ulivyojaribu kupotosha huko juu na wala haihusiani na mgogoro wanahisa!Usipotoshe, jisomee halafu tuonesha hayo usemayo yako wapi?, hotuba mbona ipo karibu:
Ndugu Wananchi;
Mwaka 1998 TANESCO walifikisha kwenye Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji, London, malalamiko kwamba gharama za uwekezaji za IPTL ni kubwa mno kuliko kiasi halisi walichowekeza. Mwaka 2001 Kituo cha Usuluhisi kilifanya uamuzi wa shauri hilo. Madai ya TANESCO yalikubaliwa kuwa uwekezaji halisi uliofanyika ni Dola za Marekani 127 na siyo Dola milioni 163.17 walizodai IPTL. Kutokana na kupungua huko kwa gharama za uwekezaji, tozo ya uwekezaji (capacity charges) nayo ilipunguzwa kutoka Dola za Marekani milioni 3.6 kwa mwezi mpaka Dola za Marekani milioni 2.6 kwa mwezi. Kituo pia, kilitoa mwongozo kuhusu ukokotoaji wa tozo hiyo.
Ndugu Wananchi;
Miaka minne baadaye TANESCO ilianza vuguvugu la kutaka kupata nafuu zaidi. Waliamua kugomea kulipa tozo ya uwekezaji kwa mkokotoo wa mwaka 2001. Nimeambiwa kuwa wanasheria wa TANESCO walishauri Shirika hilo lidai ukokotoaji kiwango cha tozo ya uwekezaji wa IPTL ufanyike kwa kuzingatia thamani ya hisa walizolipia wawekezaji ambayo ni shilingi 50,000 badala ya kutumia msingi wa mtaji uliotokana na mkopo wa Dola za Marekani milioni 38.16 wa wanahisa uliotumiwa na usuluhisho wa kwanza ICSID-1.
Wakati wakisubiri mchakato wa usuluhishi wa mzozo huu mpya kuanza, pande zote mbili zilikubaliana kuanzisha Akaunti ya Escrow ya Tegeta. Tarehe 5 Julai, 2006, akaunti hiyo ikaanzishwa kwa mkataba uliyotiwa sahihi na IPTL upande mmoja na Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya TANESCO upande mwingine. Aidha, Benki Kuu iliteuliwa kuwa wakala wa kutunza akaunti hiyo nayo ilitia sahihi.
Ndugu Wananchi;
Kwa mujibu wa mkataba huo, Kampuni ya IPTL iliendelea kupeleka madai ya tozo ya uwekezaji kwa TANESCO ambayo nayo iliwajibika kulipa madai hayo. Malipo hayo yalitakiwa kupelekwa kwenye Akaunti ya Escrow ya Tegeta tofauti na ilivyokuwa kabla ambapo yalipelekwa IPTL moja kwa moja. Utaratibu huu mpya ulikubaliwa kutumika hadi pande mbili zitakapofikia mwafaka kuhusu kiwango cha ukokotoaji. Kwa upande wa malipo ya gharama ya umeme (energy charges) TANESCO imeendelea kulipa moja kwa moja kwa IPTL bila kupitia Akaunti ya Tegeta ESCROW maana hizo hazikuwa na mgogoro.
Ndugu Wananchi;
Kwa miaka saba tangu tarehe 5 Julai, 2006, akaunti hiyo ilipoanzishwa mpaka tarehe 5 Septemba, 2013, wakati Mahakama Kuu ilipokabidhi shughuli zote za IPTL kwa PAP, hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa tozo ya uwekezaji baina ya ITPL na TANESCO. Pande mbili husika hazikuwahi kukaa kuzungumza na wala hakuna shauri lililofikishwa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Mogogoro ya Uwekezaji kama ilivyofanyika mwaka 1998.
Wakati wote huo, TANESCO iliendelea kulipa madai ya tozo ya uwekezaji ya IPTL na kupeleka malipo hayo kwenye Akaunti ya Escrow. Ulipaji ulisimama katika kipindi kifupi wakati kampuni ya IPTL ilipowekwa kwenye ufilisi. Kwa mujibu wa taarifa ya CAG, wakati akaunti hiyo inafungwa tarehe 20 Novemba, 2013, kulikuwa na fedha taslimu shilingi 8,020,522,330.37; Hatifungani zenye thamani ya shilingi 159,231,370,000 na Dola za Marekani 22,198,544. Fedha zote hizo ni sawa na shilingi bilioni 202.9.
Ndugu Wananchi;
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kama TANESCO ingelipa tozo ya uwekezaji ipasavyo, wakati huo Akaunti hii ingekuwa na shilingi bilioni 306.7. Kwa sababu ya kutolipa fedha zote ipasavyo, wakati Akaunti inafungwa TANESCO walikuwa wanadaiwa na IPTL shilingi bilioni 103.8. Kwa mujibu wa Mkataba wa Mauzo ya Umeme (PPA) malipo yaliyocheleweshwa, yanatozwa riba ya asilimia mbili ya fedha zote ambazo hazikulipwa kwa wakati. Hivyo basi, riba iliyotokana na TANESCO kuchelewesha malipo ilikuwa Dola za Marekani milioni 33.6.
Ni matumaini yangu kuwa ufafanuzi uliotolewa katika Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali unasaidia kuweka kumbukumbu sawa na sahihi kuhusu kiasi gani kilichokuwepo kwenye Akaunti ya ESCROW siku uamuzi wa Mahakama ulipofanya akaunti hiyo ifungwe. Kwa kifupi Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaeleza kuwa Akaunti hiyo ilikuwa na shilingi bilioni 202.9 na siyo shilingi bilioni 306.7 kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Kwa hiyo huoni kuwa akaunti ya ESCROW imefunguliwa baada ya anayoihita ICSID - 1 kuamua na kwa jinsi hiyo haina mahusiano na maamuzi hayo kama ulivyojaribu kupotosha huko juu na wala haihusiani na mgogoro wanahisa!
natilia Shaka akili yako nakushauli uende ukapime milemba ili wakuambie matatizo yako
Bado kuna maswali mengi.... Je miamala iliyofanyika Mkombozi na Stanbic bank ilikuwa halali kwa sheria za kibank hapa tanzania? Walonufaika ni watumishi wa umma je ilikuwa ni per Diem au mishahara wanalipwa.? Fedha ni za IPTL kwanini zipo ktk vitabu vya Tanesco? Je kuna hati halali ya mahakama iliyoandikwa kwenda BoT na Tanesco kuonesha mgogoro umeisha. Je TRA wamekwisha omba radhi kuwa walikosea kudai kodi kwa fedha ambazo hazistahili kulipiwa kodi? Rugemalira amesharudishiwa kodi yake maana pesa hiyo haistahili kulipiwa kodi? Kodi ya ongezeko la mtaji , Mabadiliko ya wanahisa na dokyument halali zilishakabidhiwa kwa Brella, fedha zote ni za IPTL SAWA je hivi ndivyo madeni yote na kesi zinazofanana ni hizi hushughulikiwa na Bank Kuu. Au ndiyo mambo ya mkuu wa nchi kuuita sarafu yake madafu.
Walonufaika ni watumishi wa umma je ilikuwa ni per Diem au mishahara wanalipwa.?
Hilo limeng'ang'aniwa na akina Kafulila ili Singasinga aonekane sio mmiliki halali wa IPTL! Sikumsikia Rais wetu akiliongelea hilo. Halituhusu sana zaidi ya uwepo wa mitambo ile ndani ya nchi yetu, inazalisha umeme tunaununua, tunautumia.
Anayebisha kuwa pesa siyo za IPTL natilia shaka sana akili zake huenda zinashida mahala fulani.
Hawezi kuzungumzia iptl kwa sababu ndio msingi wa tatizo.
Kama ni pesa zao za nini zikae BOT. Na kwani ni Zikaguliwe.
Umenifanya nitilie shaka utashi wako. Yaani bila wasiwasi unasema pesa yote ni ya IPTL!? Ulikuwepo wakati wanakokotoa hizo hesabu za 'capacity charges' na wakakubaliana pesa zote ni za IPTL? Uhalisia ni kwamba bila ukokotoaji wa hesabu za capacity charges kwa pande zote mbili pesa haziwezi kujulikana zipi ni za IPTL na zipi ni za TANESCO.
Hapa kinachoendelea ni 'betting' au 'utabiri tu'. Zile pesa hazikupaswa kutolewa mpaka hizo hesabu zitakapofanywa maana ndio msingi wa mgogoro.
walikokotoa ndo wakalipa,we unadhani walitakiwa kupita nyumba kwa nyumba wakitangaza kuwa wanakwenda kukokotoa?
Kama ni pesa zao za nini zikae BOT. Na kwani ni Zikaguliwe.
BOT alikua agent tu,kukaguliwa hakuzifanyi za umma
Kwa porojo tu haujambo, lakini ukweli NIL.
Hilo ndiyo tatizo lenu kubwa bavichaa.
Mimi sio Bavicha. Nina umri sawa na Rahisi wako. You can fool some people sometimes, but you cant fool all the people all the times.
Utakuwa mjomba wao.
Faiza foxy sikujuwa kuwa upeo wako wa kufikiri no mdogo kiasi hicho.
Faiza foxy sikujuwa kuwa upeo wako wa kufikiri no mdogo kiasi hicho.
Nashukuru unakubaliana na wengi kuwa Escrow si zao la maamuzi ya kwanza ya ICSID na wala si mgogoro wa wana hisa. Huu ndiyo uongo ulioenezwa awali. Ni kwa nini Tanesco ambao ndiyo waliolalamikia tozo lililokuwa si la haki hawakuchukua hatua ni vyema serikali pia ikatoa maelezo ya hili na wala si kuwasukumia Tanesco pekee. Hii ni kwa sababu ilifikia huko nyuma maamuzi mengi yalitoka serikalini (kumbuka hata huu ushauri wa malalamiko yaliridhiwa na serikali ikiwa mpaka ufunguaji wa hii akaunti). Ikiwa tatizo halijatatuliwa lililopelekea akaunti hii kufunguliwa ilikuwaje ifungwe na pesa zichukuliwe na upande mmoja au ni kwa 'shinikizo'?Hivi ni nini hapo hujakielewa, unanshangaza sana, ICSID ilishatowa maamuzi 2001. Akaunti ya escrow imeanzishwa 2006 imesitishwa kwa amri ya mahakama 2013, rudia:
Kwa miaka saba tangu tarehe 5 Julai, 2006, akaunti hiyo ilipoanzishwa mpaka tarehe 5 Septemba, 2013, wakati Mahakama Kuu ilipokabidhi shughuli zote za IPTL kwa PAP, hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa tozo ya uwekezaji baina ya ITPL7 na TANESCO. Pande mbili husika hazikuwahi kukaa kuzungumza na wala hakuna shauri lililofikishwa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Mogogoro ya Uwekezaji kama ilivyofanyika mwaka 1998.
Wakati wote huo, TANESCO iliendelea kulipa madai ya tozo ya uwekezaji ya IPTL na kupeleka malipo hayo kwenye Akaunti ya Escrow. Ulipaji ulisimama katika kipindi kifupi wakati kampuni ya IPTL ilipowekwa kwenye ufilisi. Kwa mujibu wa 8taarifa ya CAG, wakati akaunti hiyo inafungwa tarehe 20 Novemba, 2013, kulikuwa na fedha taslimu shilingi 8,020,522,330.37; Hatifungani zenye thamani ya shilingi 159,231,370,000 na Dola za Marekani 22,198,544. Fedha zote hizo ni sawa na shilingi bilioni 202.9.
Hili shauri ulilosema halijatatuliwa ni lipi?
Huwa nauliza hivi, hizi shule huwa mnaenda kusomea ujinga?