Maswali ya mwisho juu ya Escrow

mkuu tupatupa uliadi utakuja na majibu ya wale wazee wa dar mbona kimya au uliwapa majibu wazee sisi hatutakiwi kujua?
 

Hilo swali tumeshalijibu humu, unaonesha ni mvivu wa kutembea-tembae JF kwenye mada zinazohusu hii kadhia, si kitu, hili hapa jibu la aliyeuliza kama wewe, nawe litakufaa:

 

Kwahiyo kesi ilimalizika vizuri ndiyo mahakama ikakubali IPTL walipwe fedha zao ?
 
Kweli wewe ndiyo hujitambui , kama hizo fedha siyo za umma.....
Unachunguza kama rushwa imetendeka, Kwanini rushwa itendeke?
Kwanini Maswi achunguzwe kama anahusika? Anahusika na nini sasa?
Kwanini muhongo anachunguzwa kama anahusika , anahusika kwa nini sasa kama mambo yote yalifuata utaratibu na fedha si za umma?
Stanbic inasafisha pesa chafu au la , km pesa siyo za umma hao stanbic wanachunguzwa ya nini na kulikuwa na haja gani ya wao kusafisha hela ya malipo halali kutoka BOT?
Na huyo CAG kasema lini hizo hela siyo za umma?

Kuficha wizi ni kazi sana.
Taratibu mtaendelea kuumbuka, just wait.
 

Yaani wewe ndiyo hovyo kabisa , kwa post hii unaonekana hamna kitu unajua kichwani kwako kuhusu escrow.
Shame on you.
 
Anayebisha kuwa pesa siyo za IPTL natilia shaka sana akili zake huenda zinashida mahala fulani.

Uchunguzi aliodai rais ni wa nini? Kwa nini Anna Tibaijuka amewajibisha kwa kupokea fedha halali?? Mtajichanganya sana zile ni pesa zetu. Rejea mahojiano ya Utoh na mwandishi kwenye gazeti la Raia mwema wiki hii.
 
Mkuu umenichanganya kabisa.kwenye katiba inayopendekezwa chama chetu kimeruhusu viongozi wa umma wawe na account nje ya nchi.Je hizo account ni kwa ajiri ya kupokelea mshahara tu?
 
Kwa hili sakata la ESCROW Rais ametoa funzo kubwa sana kwa waliomtangulia na watakaokuja:

-Kwanza ni somo la utawala bora unaofuata misingi ya sheria, kanuni tulizojiwekea kwenye utumishi na mamlaka mbalimbali;
-Pili ni mgawanyo wa madaraka kikatiba na kisheria juu ya mihimili yetu mitatu ambayo ni Dola, Mahakama na Bunge;
-Tatu ni juu ya dhana nzima ya uwajibikaji pale inapolazimu kufanya hivo na
-Nne ni ITIFAKI na nidhamu.


Kwa kweli ambao hamtaki kumwelewa Rais wetu ni kwa kuwa tu mliamua kwa pupa, kwa jazba, kwa visasi na mihemuko ya kisiasa. Kwa mfano, ilikuwaje Bunge zima likashindwa kuelewa taratibu za kuwawajibisha Majaji? Ilikuwaje Bunge zima likashindwa kuelewa kuwa Katibu Mkuu ni Mtumishi wa UMMA na ziko taratibu za kufuatwa ili kumwondoa madarakani?
 
Hilo swali tumeshalijibu humu, unaonesha ni mvivu wa kutembea-tembae JF kwenye mada zinazohusu hii kadhia, si kitu, hili hapa jibu la aliyeuliza kama wewe, nawe litakufaa:
Shangazi FaizaFoxy nami nimekuwa mvivu naomba kufahamu AG amaendika barua ya kujiuzulu akidai ushauri wake haukueleweka na kupelekea kuchafua hali ya hewa, kwa nini asifafanue tena huo ushauri wake ili aeleweke na kwanini bosi wake ambaye ni JK aridhie kujiuzulu kwake?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hapa serikali iliingiaje?au nayo ina hisa IPTL
 

Naona unachanganya mambo.

Kuna mambo manne makuu tofauti katika suala la escrow, Jee, unayajuwa au unakurupuka tu?

Hilo la kuchunguza ni azimio la Bunge, sasa waulize wabunge wako kwanini walitaka ufanyike uchunguzi? au ulitaka uchunguzi usifanyike kama azimio la bunge lilivyoazimia? Na Kikwete kalielezea hilo wazi wazi na hatua zilizochukuliwa, hili hapa:


Azimio la Tatu: Linasomeka; "Bunge linaazimia kwamba TAKUKURU, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama vichukue hatua stahili kwa mujibu wa sheria za nchi yetu dhidi ya watu waliotajwa kwenye taarifa maalum ya Kamati husika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya ESCROW, na watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea kuhusu kuhusika kwao katika vitendo hivyo vya jinai"

Vyombo husika vimekwishaagizwa kufanya hivyo na kazi imeanza na inaendelea. Ikiwa wapo watu wenye makosa hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.
 
Anayebisha kuwa pesa siyo za IPTL natilia shaka sana akili zake huenda zinashida mahala fulani.
Mmoja wao ni Prof.Mwandosya,Wassira na Mwigulu mawaziri katika Serikali ya ccm
 
Huyu Singa aliiangusha KANU kwa deal zake na mtoto wa Moi sasa anaiangusha CCM kwa deal zake na familia ya Rais
 
Maazimio haya yalifikiwa na Bunge(Wananchi) kwa kuamini/kujua kuwa pesa zile zilikuwa ni za Umma.Kwa Kuwa mkuu wa nchi amethibitisha kuwa pesa zile hazikuwa za umma,Mapendekezo yale yalitakiwa yawe yamejifuta yenyewe.Kuendelea kuchunguza tuhuma hewa ni ufisadi mwingine
 
Wewe ndiyo unakurupuka na kujaribu kupotosha.
Kama huyo Kikwete ameona hakuna lolote na fedha si za umma kulikuwa na umuhimu gani wa kuendesha uchunguzi kama Azimio la bunge lilivyotaka.
 
Mkuu hapa serikali iliingiaje?au nayo ina hisa IPTL
Escrow is money or property which is given to someone, but which is kept by another person until the first person has done a particular thing or met a particular requirements( mainly LEGAL).
Rais wetu alikuwa sahihi kwa tafsiri hiyo. Tuendelee tu na porojo za akina Kafulila.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…