VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Mniwie radhi kwa kuuliza. Nauliza kwa mara ya mwisho. Sitauliza tena. Nitabaki kimya hata kisemwe au kifanywe niní. Sitauliza tena juu ya Escrow. Nitasubiria tu kashfa za bomba la gesi na sukari. Basi.
Kwakuwa tumeambiwa na Rais kuwa mabilioni yaliyokuwemo Escrow yote yalikuwa ya IPTL. Na kwakuwa tumeambiwa na kuaminishwa na Rais kuwa mabilioni ya Escrow yalilipwa au kupewa mwenyewe ambaye ni IPTL.
Na kwakuwa mwenye mabilioni,IPTL,amechukua chake kiutaratibu na Serikali ilijua. Je,uchunguzi na hatua zinazoendelea kuchukuliwa hivi sasa zinalenga niní? Wanaochunguzwa wanachunguzwa kwa makosa yapi hasa?
Hata nisipojibiwa,nitaridhika kama mwafrika!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam