Maswali ya kujiuliza juu ya Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station

Teyari tuna gesi ya Songosongo na Mnazi bay ambayo ndiyo tunaitumia Kinyerezi 1,2 3 na pia Ubungo 1,2.

Gesi yenye walakini ni hiyo Kikwete aliyoipigia debe 2010 ambayo bado haijaanza kuchimbwa huko mtwara. Hiyo ni gesi nyingi sana na visima vipo ila wanaomilki ni makampuni ya kigeni pamoja na viongozi wa awamu ya nne. Walichokipanga ni kutulazimisha kutumia umeme wa gesi hiyo kwa bei kubwa ili wao wanufaike.

Uchimbaji wa gesi/mafuta ni ghali sana hasa kama visima viko majini (rejea , watanzania mnaweza kuwekeza kwenye jwisi tuu). Makampuni hayo makubwa ya uchimbaji yakipewa (nunua) leseni hutumia gharama zao kuyapata (hua wanaongeza gharama makusudi). Sasa sijui kiundani mikataba hiyo serikali ya Kikwete ilifanya nini ila kuna ufisadi wa hali ya juu ambao ingewagharimu wananchi kwa kutumia gesi hiyo.

vipi akija kiongozi mwingine baada ya mda akaamua ku-focus kwenye gesi? Maana naamini kwa dhati kabisa SG haiwezi kuisha kipindi cha JPM! Huu ni mradi mkubwa sana.
Umeongelea jambo ambalo hata mimi na wasi wasi nalo, akija Rais mwenye mahusiano na waliosaini mikataba ya gesi itakuwaje? Hili nadhani ni jambo ambalo wahusika wanaliangali kwa makini. Watu wengi hawakupenda maamuzi ya Magu ya kujenga SG, ndiyo maana kelele ziko duniani kote na watu hawa wana nguvu na pesa nyingi ndiyo maaana ulinzi wa Rais Magufuli si wa kawaida.

Kuhusu kumalizika kwa mradi hilo usiwe na shaka, miradi mingi husuasua kwa kukosa fedha ila Magufuli ameamua kuhakikisha pesa inapatikana, tuombe uhai tuu tuone itakuwaje muhula wake ukiisha.
Yote kwa yote, mimi namsifu JPM kwa hili. Lakini wasiwasi wangu ni kwamba kama taifa tunashindwa kuwa na vipaumbele ambavyo kila chama/utawala utaviheshimu! N mwisho wa siku itatugharimu sisi walipa kodi.
Tatizo siyo vipaumbele bali ni sabotage, mataifa makubwa hayapendi kuona mataifa kama yetu yakiendelea hivyo wanafanya kila njia kuzuia maendeleo. Na moja ya njia wanazotumia ni kuwaweka au kuwashawishi viongozi wetu ili wafanye kazi kwa niaba yao. Hawa jamaa huangalia udhaifu wa viongozi wetu (kama kutajirika haraka au kuishi kifahari). Na wakishampata mtu wao huanza kuiendesha nchi kiholela ili kuwe na utamaduni wa rushwa, wizi wizi, ukwepaji kodi na kutokuwa na uwajibikaji. Ni rahisi sana kuitawala nchi kwa "remote" kama kuna chaos (Libya, Congo,S. Sudan n.k) .
 
Asante sana kiongozi. Sijawahi kuwa na shaka na patriotism ya JPM. Wasiwasi ni kuhusu institutions zetu. Ingawa anachokifanya ni kwa manufaa ya taifa, hakika watakaofuata sijui kama watakuwa na uzalendo kama yeye. Hii miradi miwili ya SG na Train kama ikifanikiwa, inaweza kusaidia maendeleo ya taifa letu. Again, hakuna asiye na kasoro, lakini, bado naamini na mapungufu ya huyu bwana, he is trying to have bigger vision for the country. Unfortunately wachache watamuelewa especially kipindi hiki ambacho njaa imetamalaki
 

Hapa sijakuelewa kidogo,kwamba gesi haitumiki au haitumiki ipasavyo au hujui kama gesi inatumila ?
 
Kua na ustaarabu, umejibiwa vizuri wewe unaingiza propaganda zako na vimisimamo vya kidem.
 
Umeniwahi nilikua nataka kumjibu kama wewe nakupa heko!
 
Kwani Tz ni nchi ya kufugia wanyama tu? Wewe umepewa ruzuku na mabeberu ili utafsiri makala zao kiswahili kuwatisha watu. Acha tujiamulie kutumia ardhi yetu
apo umesema kwel wazung hifadhi za wanyama zilisha isha kitambo nw wanyama unawakuta zoo 2 af cc 2endelee kua zizi kwakua hatuna matumiz mengne na ardhi ye2
 
Je maji ni chanzo ya uhakika?tusije haribu mazingira ukaja ukame ikaja stori ya mtera ya kununua mvua
 
Ingekuwa Viongozi wa CCM Wajibu hoja hivi, si bungeni tu popote pale hoja zingekuwa zinajibuwa kwa hoja na sio matusi, kejeli, propaganda au kuteka. Hili taifa lingekuwa mbali sana. Mkuu umenipa darasa la kutosha Mungu akubariki.
 
Je maji ni chanzo ya uhakika?tusije haribu mazingira ukaja ukame ikaja stori ya mtera ya kununua mvua
kama unaijua jiografia ya Tanzania vizuri utaelewa kuwa vyanzo vya mto rufiji vinatoka nyanda za juu kusini ambako muinuko wake kutoka usawa wa bahari ni kwenye wastani wa mita 1,700 (5500ft). Kukupa picha ya muinuko huo ni sawa na kupanda theluthi moja ya mlima kilimanjaro. Vyanzo hivi ni vingi vikiendelea mpaka Iringa kwenye muinuko wa mita 1,500 (5,090 ft) kutoka juu ya usawa wa bahari.

Kama umewahi kufika nyanda za juu kusini utaona kiasi cha uoto wa asili kilichopo kule, si mchezo. Kuwa na uoto wa asili ni kiashiria chanya na cha uhakika wa maji na katika vitu ambavyo huwezi kudanganya kwa muda mrefu dunia hii ni asili. Angalia Dubai wanavyohangaika kutumia mabilioni ya dola kupendezesha jangwa lakini wapi, bado kukavu.

Kiasi cha uoto wa asili uliopo kule na jinsi kusini ilivyoinuka "inakuwa rahisi na karibu kuivuta mvua huko mbinguni , (not really but you get the point).

kiasi hicho kikubwa cha uoto kinatengeneza mvuke mwingi unaotengeneza mvua nyingi ambayo inaotesha mimea mingi, inayokuja kutoa mvuke mwingi unaokuja kuleta mvua nyingine nyingi (alichonacho ataongezewa). Mvua hizo zote ndiyo zinatengeneza vyanzo vya mto rufiji huko chini kwenye bwawa.

Kwahiyo usikonde sana, bwawa haliwezi kukakuka, leo wala kesho.
 
hivi hiyo miti yote(2.6mil) ikikatwa hayo maji yatakuwa yanatokea wapi?
 
Kwenye hii makala nimependa picha tu. Hayo mambo mengine tuwaachie wao.Inaweza ikawa motive ya kuanzisha huu mradi ni teni pasenti , kwa kuwa mradi wa ges watu walishapiga chao, yaweza ikawa ni nia nzuri ya kutafuta urahisi wa bei ya umeme ,wenye ukweli ni wenye mradi. Sisi wengine ni hisia tu
 
Mkuu umevuta bhange. Unajua ufisadi uliofanyika kwenye gesi au unalopoka tu. Hamjui kuwa mlishasainishwa mikataba ya Mangungo kwenye gesi na yote iko kwa mabeberu na mafisadi wakiisubiri serikali na tanesco waingie kichwakichwa wapigwe
Mnawalaani MABEBERU wakati waliwasomesha mababu zenu hadi ninyi wenyewe ili wawakamue vizuri?

Hata huyo unayemtetea ni walewale,wala hana tofauti na watangulizi wake.

Unaweza ukajifanya hujui,lkn niambie ...wenzake waliuza gesi kwa MABEBERU,alichukua hatua gani?

Lodilofa kauza migodi yote ya dhahabu kwa mkataba wa ki mangungo...kachukuliwa hatua gani?

Ruksa ....kuna mkataba wa TEGETA APTL nambie..mzee meko kachukua hatua gani?

Hivi...hizi ndege zetu zimenunuliwa kwa shs ngapi? Ww unajua?

Kule chato kuna uwanja wa ndege wa kimataifa..jiwe hapigi hela?

Tuko chini ya mkoloni mweusi ccm,tujitambue.

Kazi iliyopo ni utekaji,ni mauaji,kupoteza watu.sheria nyingi zisizo kichwa wala miguu..etc

Mkoloni tuliye naye ni janga la taifa...tujitambue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…