Maswali muhimu kuhusu serikali kuhamia Dodoma

Maswali muhimu kuhusu serikali kuhamia Dodoma

structuralist

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,230
Reaction score
909
Wakuu amani ya Muumba iwe juu yenu.

Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na mjadala kuhusu serikali kuhamia dodoma. Binafsi nadhani ni jambo jema haswa ukizingatia kuwa ni swala amablo lilishakuwepo toka kipindi kirefu nyuma.

Hata hivyo kama mtanzania wa kawaida kuna maswali najiuliza na sipati majibu hivyo nimeona nijaribu kuyaleta hapa ili kupata udadavuzi mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali

1: Neno serikali,kwa mujibu wa muktadha huu wa kuhamia dodoma ni kitu gani hasa? Yani ni wizara tu, idara tu, au wanamaanisha nini wanaposema serikali? Ili kueleweka vizuri nitatoa mfano. Wiza ya elimu ikihamia dodoma,taasisi zilizo chini yake kama vile NECTA, NACTE, TCU nk zitahama ama la?

Je, zisipohama hiyo wizara huko dodoma itakuwa inafanyaje kazi ili hali taasisi zake nyingi zitakuwa darisalama? Vivyo kwenye sekta nyingine kama viwanda na biashara -tbs, nk? Hapa naomba ufafanuzi mpana kidogo, ili tujue nai anahama nani hahami.

2: Je, kumetokea nini mpaka kuhama huku kuharakishwe namna hiyo?

3: Je, serikali imetafakari juu ya athari ya zoezi hili kwa ughafla huu? Kuna baadhi ya taasisi za serikali zimepangisha majengo kutoka kwa wadau mablimbali, na kuna mikataba wameingia na wapangishaji hao, Je serikali imliangalia hilo na athari za kuvunja hiyo mikata?

Je, serikali imeangali wazabuni katika tenda mabimbaili inazpata na kuangalia athari ya kuhamia dodoma kwa ishu za zabuni hizo? Je kampuni zenye kutoa huduma za ulinzi na usafi(mfano tu) zitakubali kuendelea kutoa huduma hizo dodoma na kwa makubaliano yapi?

4: Kwakuwa viongozi wakubwa waserikali wana makazi madogo dodoma na kwao haina athari sana kuhama, Je wamehakikisha kuwa wafanyakazi wote watapata makazi dodma maeneo pia mabayo hayataathiri ufanisi wao?

5: Binadamu anaitaji kujiandaa kisaikolojia zaidi kuliko kifedha na muda ni jambo muhimu katika kufanikisha hili, Je serikali imewaanda watumishi wake kisaikolojia juu ya wao kuhamia dodoma? Kwa muda mfupi watakaokuwa nao watuishi, serikali haini kuwa inaweza kunaweza kuwa na mtizamo mbaya wa zoezi hili kwa watumishi wake?

Je, wakihama, kwa muda mfupi huu watawezaje kuacha makazi ya salama? Uimara wa familia je? Hivi serikali haioni kuwa kuna uwezekano wa watumishi kuomba ruksa za mara kwa mara kwenda kuweka mambo ya kifamialia sawa pale ambapo watahama kwa muda mfupi bila ya wao kujiandaa vizuri?

6: Hivi serikali haikuona kuwa kuweka zoezi hili ndani ya muda mfupi kunaweza sababisha gharama za maisha dodoma kuongezeka sana kwakuwa kutakuwa na ongezeko la ghafla la mahitaji bila ya kuwa na ongezeko sawa la usambazaji? Mathalani kodi katika nyumba zitapanda sana,je hilo serikali imeliangaliaje?

7: Majengo yakokuwa yanatumiwa na serikali dar yatatumika kwa utaratibu gani haswa ukizingatia kutakuwa na kuondoka kwa ghafla?

8: Kauli ya mh raisi ilikuwa kuhamia dodoma ndani ya miaka hii minne, Je kama wizara zinahama ndani ya mwezi, kulikuwa na ulazima kweli wa kufanya hivyo?

9: Kwakuwa bajeti ilishapitishwa, ni kutoka fungu gani ambalo serikali italitumia katika kufanikisha zoezi hilo?

10: Kwakuwa serikali inafanya kazi na wadau mablimbali, ni kwanamna gani imejipanga kuhakiksha kuwa kuhama kwake hasa huku kwa muda mfupi hakutaathiri ushirikishwaji wa wadau hao katika nyanja mbalimbali? Kwamfano mabalozi, taasisi na mashirika ya imataifa nk.

NB: Tafadhali tuache ushabiki na tujikite kwenye hoja. Ingependeza kama ungejibu baadhi ya hoja(kama una majibu) ama ukaongeza maswali(kama unayo pia) ili mwisho wa siku tupate uelewa mpana wa hii dhana ya serikali kuhamia dodoma. Nawasilisha
 
Maswali yote majibu yake yatatolewa serikali ikishahamia Dodoma.Sasa hivi watu wanafungasha mizigo kupakia kwenye malori kwenda Dodoma.Kipindi cha maswali na majibu kisubirie dodoma tangulia na wewe na maswali yako tukukute kule Dodoma.Serikali inaposema watu wahamie Dodoma ni pamoja na wenye maswali yao waende na maswali yao Dodoma.
 
HILI NALIUNGANISHA NA KAULI YA MH. SUGU "SERIKALI INAENDESHWA KWA MZUKA".....HAIWEZEKANI RAISI ASEME NDANI YA MIAKA MI4 NA MIEZI MI4 ATAKUWA KAHAMIA DODOMA...MARA UNAWASIKIA WASAIDIZI WAKE WOTE WANAHAMIA DODOMA NDANI YA MWEZI MMOJA.

"MZUKA AT WORKS......"
 
USILETE MAJIBU MEPESI KWA MASWALI MAZITO YA MTOA HOJA.....WANAPAKIA MIZIGO KWA BAJETI NA FUNGU LIPI LILILOPITISHWA "KUHAMIA DODOMA" ?....

MKULU ALIKUWA SAHIHI ILA HAWA NDIO WAMEKURUPUKA... MIAKA MI4 NA MIEZI MI4 INATOSHA KUHAMIA DODOMA IWAPO BAJETI INGEWEKWA KUANZIA MWAKA UJAO WA KILA WIZARA 8 KWA MWAKA KUHAMIA DODOMA..... ILA HII MIZUKA NAONA HATA WEWE UNAITUMIA KUJIBU.
 
Fanya mchakato wa wapi utafikia,unayaachaje mazingira yako ya Dar na familia yako unaondoka nayo vipi au unaiachaje. Maana hayo maswali tumeyauliza sana ktk wiki hii kuna threads visizopungua 20 zinahusu jambo hilo na ukizitafuta utakuta wadau walichokihoji na hatukupata majibu na Govt inaendelea na kusudio lake.
 
USILETE MAJIBU MEPESI KWA MASWALI MAZITO YA MTOA HOJA.....WANAPAKIA MIZIGO KWA BAJETI NA FUNGU LIPI LILILOPITISHWA "KUHAMIA DODOMA" ?....
.

Kaa hivyo hivyo aliposema elimu bure inaanza mkasema kwenye bajeti haikuwepo haiwezekani na ikawezekana! Aliposema anataka kila shule lazima iwe na madawati ya kutosha hataki kuona mtoto anayekaa chini mkabeza mkasema hilo haliwezekani haliko kwenye bajeti likawezekana!!

Wewe endelea kuimba bajeti,bajeti watu saa hizi wengine wanakaribia kufika DODOMA na mizigo yao
 
Hayo maswali majawabu yake nitakupa tukiwa Dodoma...twendeni Dodoma kwanza...acheni upoyoyo...
 
Binafsi mpaka sasa bado natafakali kwanini waziri mkuu wakati wa bunge la budget hakutoa taarifa ya yeye kuhamia Dodoma mapema Kama alivyosema!!!! Tafakari yangu ni kuhusu pesa za watumishi wa ofisi za waziri mkuu kuhamia huko wiki ijayo na wengine wengi watafuta, wataishi kwa pesa ipi? Imepitishwa na bunge lipi? Navyojua kuna mkusanya pesa na kuna mpanga matumizi ya hizo pesa then kuna mpitisha matumizi ya pesa zote yaani bunge.
 
Maswali yote majibu yake yatatolewa serikali ikishahamia Dodoma.Sasa hivi watu wanafungasha mizigo kupakia kwenye malori kwenda Dodoma.Kipindi cha maswali na majibu kisubirie dodoma tangulia na wewe na maswali yako tukukute kule Dodoma.Serikali inaposema watu wahamie Dodoma ni pamoja na wenye maswali yao waende na maswali yao Dodoma.
kumekucha
 
HILI NALIUNGANISHA NA KAULI YA MH. SUGU "SERIKALI INAENDESHWA KWA MZUKA".....HAIWEZEKANI RAISI ASEME NDANI YA MIAKA MI4 NA MIEZI MI4 ATAKUWA KAHAMIA DODOMA...MARA UNAWASIKIA WASAIDIZI WAKE WOTE WANAHAMIA DODOMA NDANI YA MWEZI MMOJA.

"MZUKA AT WORKS......"
sugu
 
Kaa hivyo hivyo aliposema elimu bure inaanza mkasema kwenye bajeti haikuwepo haiwezekani na ikawezekana! Aliposema anataka kila shule lazima iwe na madawati ya kutosha hataki kuona mtoto anayekaa chini mkabeza mkasema hilo haliwezekani haliko kwenye bajeti likawezekana!!

Wewe endelea kuimba bajeti,bajeti watu saa hizi wengine wanakaribia kufika DODOMA na mizigo yao

KARIBU KWETU NZUGUNI....VYUMBA VYA KUPANGA VIPO NA BEI TUMEPANDISHA ILA HATUPOKEI KODI CHINI YA MWAKA MMOJA....NA MARUFUKU WANAUME ZAIDI YA MMOJA KULALA AU KUSHEA CHUMBA MUSIJE KUWAAMBUKIZA WATU WA DODOMA USHOGA WA DAR.
 
Kwa Maoni yangu Sio lazima serikali yote ihamie dodoma namaanisha wizara...hakuna haja ya wizara inayohusika na viwanda kwenda domu wakati viwanda ving vipo dar,wizara ya madini&nishati hii ingeenda hata Mwanza ule ndo ukanda wenye madini,Wizara ya kilimo peleka hata mbeya kusini wanalima sana,Dodoma pale zingekaa wizara chache kama tamisemi/ajira na utumishi kwan ni katikati nani rahisi kufikika,Je izo nyumba za wafanyakazi zipo au ndo kwenda kukaa guest nakuingizia nchi gharama ambazo hazina msingi...
 
Maswali yote majibu yake yatatolewa serikali ikishahamia Dodoma.Sasa hivi watu wanafungasha mizigo kupakia kwenye malori kwenda Dodoma.Kipindi cha maswali na majibu kisubirie dodoma tangulia na wewe na maswali yako tukukute kule Dodoma.Serikali inaposema watu wahamie Dodoma ni pamoja na wenye maswali yao waende na maswali yao Dodoma.

Mungu alipokupa kichwa ni kwa ajili ya kufikiri na kuchanganua mambo kwa upana wake. sasa kwa mtu kama wewe sijui kazi ya kichwa chako nini. eti tu kwa vile tu mizuka na wewe umezuka. kwa kweli miaka hii mitano tutaona mengi.
 
Maswali yote majibu yake yatatolewa serikali ikishahamia Dodoma.Sasa hivi watu wanafungasha mizigo kupakia kwenye malori kwenda Dodoma.Kipindi cha maswali na majibu kisubirie dodoma tangulia na wewe na maswali yako tukukute kule Dodoma.Serikali inaposema watu wahamie Dodoma ni pamoja na wenye maswali yao waende na maswali yao Dodoma.
Mbavu zangu jamani
 
Wakuu amani ya Muumba iwe juu yenu.
Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na mjadala kuhusu serikali kuhamia dodoma. Binafsi nadhani ni jambo jema haswa ukizingatia kuwa ni swala amablo lilishakuwepo toka kipindi kirefu nyuma. Hata hivyo kama mtanzania wa kawaida kuna maswali najiuliza na sipati majibu hivyo nimeona nijaribu kuyaleta hapa ili kupata udadavuzi mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali
1: Neno serikali,kwa mujibu wa muktadha huu wa kuhamia dodoma ni kitu gani hasa? Yani ni wizara tu, idara tu, au wanamaanisha nini wanaposema serikali? Ili kueleweka vizuri nitatoa mfano. Wiza ya elimu ikihamia dodoma,taasisi zilizo chini yake kama vile NECTA, NACTE, TCU nk zitahama ama la? Je zisipohama hiyo wizara huko dodoma itakuwa inafanyaje kazi ili hali taasisi zake nyingi zitakuwa darisalama? Vivyo kwenye sekta nyingine kama viwanda na biashara -tbs, nk? Hapa naomba ufafanuzi mpana kidogo, ili tujue nai anahama nani hahami.

2: Je kumetokea nini mpaka kuhama huku kuharakishwe namna hiyo?

3: Je serikali imetafakari juu ya athari ya zoezi hili kwa ughafla huu? Kuna baadhi ya taasisi za serikali zimepangisha majengo kutoka kwa wadau mablimbali, na kuna mikataba wameingia na wapangishaji hao, Je serikali imliangalia hilo na athari za kuvunja hiyo mikata? Je serikali imeangali wazabuni katika tenda mabimbaili inazpata na kuangalia athari ya kuhamia dodoma kwa ishu za zabuni hizo? Je kampuni zenye kutoa huduma za ulinzi na usafi(mfano tu) zitakubali kuendelea kutoa huduma hizo dodoma na kwa makubaliano yapi?

4: Kwakuwa viongozi wakubwa waserikali wana makazi madogo dodoma na kwao haina athari sana kuhama, Je wamehakikisha kuwa wafanyakazi wote watapata makazi dodma maeneo pia mabayo hayataathiri ufanisi wao?

5: Binadamu anaitaji kujiandaa kisaikolojia zaidi kuliko kifedha na muda ni jambo muhimu katika kufanikisha hili, Je serikali imewaanda watumishi wake kisaikolojia juu ya wao kuhamia dodoma? Kwa muda mfupi watakaokuwa nao watuishi, serikali haini kuwa inaweza kunaweza kuwa na mtizamo mbaya wa zoezi hili kwa watumishi wake? Je wakihama, kwa muda mfupi huu watawezaje kuacha makazi ya salama? Uimara wa familia je? Hivi serikali haioni kuwa kuna uwezekano wa watumishi kuomba ruksa za mara kwa mara kwenda kuweka mambo ya kifamialia sawa pale ambapo watahama kwa muda mfupi bila ya wao kujiandaa vizuri?

6: Hivi serikali haikuona kuwa kuweka zoezi hili ndani ya muda mfupi kunaweza sababisha gharama za maisha dodoma kuongezeka sana kwakuwa kutakuwa na ongezeko la ghafla la mahitaji bila ya kuwa na ongezeko sawa la usambazaji? Mathalani kodi katika nyumba zitapanda sana,je hilo serikali imeliangaliaje?

7: Majengo yakokuwa yanatumiwa na serikali dar yatatumika kwa utaratibu gani haswa ukizingatia kutakuwa na kuondoka kwa ghafla?

8: Kauli ya mh raisi ilikuwa kuhamia dodoma ndani ya miaka hii minne, Je kama wizara zinahama ndani ya mwezi, kulikuwa na ulazima kweli wa kufanya hivyo?

9: Kwakuwa bajeti ilishapitishwa, ni kutoka fungu gani ambalo serikali italitumia katika kufanikisha zoezi hilo?

10: Kwakuwa serikali inafanya kazi na wadau mablimbali, ni kwanamna gani imejipanga kuhakiksha kuwa kuhama kwake hasa huku kwa muda mfupi hakutaathiri ushirikishwaji wa wadau hao katika nyanja mbalimbali? Kwamfano mabalozi, taasisi na mashirika ya imataifa nk.

NB: Tafadhali tuache ushabiki na tujikite kwenye hoja. Ingependeza kama ungejibu baadhi ya hoja(kama una majibu) ama ukaongeza maswali(kama unayo pia) ili mwisho wa siku tupate uelewa mpana wa hii dhana ya serikali kuhamia dodoma. Nawasilisha
Kwanza niseme siyo ghafla kama wengi wanavyo sema. mpango wa kuhamia Dodoma ulikuwa ni wa serikali, na ulitangazwa mwaka 1975.Kimsingi ni mpango mzuri kwani Dodoma ni katikati ya Nchi, kwahiyo mikoa mingi itapata huduma kwa urahisi.

Kuhusu nani anatakiwa kuhamia Dodoma ikiwa serikali inahamia huko, ni kwamba, Kwanza Rais lazima ahamie. maana yake ni kwamba ikulu itahamia Dodoma.Kama hivyo ndivyo, maana yake nyingine ni kwamba kikiosi cha ulinzi wa Rais kinahama.Wengine ambao lazima wahamie Dodoma kwa maana hiyo ni Usalama wa Taifa, polisi, Makao makuu ya JWTZ, na Wizara zote.

Wizara zina idara lazima zihame.ila vitengo kama ulivyo sema NECTA,NACTE,HESLEB nk siyo lazima sana wahame sasa.Ila ili kuwarahisishia watu kupata huduma muhimu sehemu moja, huko mbeleni hata vitengo hivyo vitahamia Dodoma! Ama kuhusu mikataba mbalimbali hiyo haina maana sana kwasababu ni vitu vinavyo zungumzika.Kifupi ni kwamba hakuna jambo lisilo na Changamoto zake! mwanzo mgumu lakini huko mbeleni kuna faida nyingi makao makuu ya serikali kuwa Dodoma kuliko Dar es salaam.
 
Magufuli yupo serious sana na ahadi zake waliombeza haiwezekani kuamia Dodoma ndio hao hao wanapoona inawezekana wanalia lia machozi.
 
We kama huna kiwanja Dodoma kaa kimya, acha serikali ihamie.
 
Madawati imenunua serikali? au watu wamechangia? Na kula na kulala mtaomba mchangiwe? Elimu bure unajua kila mwezi ina gharimu sh ngapi? au hujui upo upo tu
 
Back
Top Bottom