Maswali matano muhimu kuhusu Rais Magufuli

Maswali matano muhimu kuhusu Rais Magufuli

Uwezo wake wa kuongoza ndio umefikia hapo. Sasa mnataka afanye Nini zaidi ya hapo ?
 
Naomba nikujibu kwa kifupi sababu hoja zako nyingi zimemlenga mtu binafsi ambaye ni raisi JPM na sio mifumo kama nchi. Najua rais ana mapungufu hasa katika kuteua wateule wake ambao anashirikiana nao kutimiza ilani ya chama chake.

JPM kuteua watu wa ukanda wake sina hakika na hilo sababu nikiangalia kuna
Waziri mkuu(mtwara) ,
Jaji mkuu( muislamu),
Spika wa bunge ( nafikiri anatokea dodoma).
Sasa hapo ndio penye msingi wa nchi.
Mimi simetetei rais JPM bali najaribu kuelezea kile kinachoendelea katika nchi yangu pendwa Tanzania. sababu tukikaa kimya mabepari hayachelewi kuaminisha watu uongo kwa kigezo cha siasa, demokrasia halafu mwisho wa siku watuletee viongozi vibaraka wao warudi kunyonya tena madini yetu. Kuaribu wanyama wetu kwa ujangili, kuharibu vijana wetu kwa madawa ya kulevya n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
mafisadi wanapiga kelele wakati walikuwa wanaelekea kuiharibu nchi na false economy.
 
mitindo huru: Nilifikiri nahojiana na mtu mwenye upeo wa mambo na anayeifahamu TZ, kumbe dhaifu hivyo kiufahamu. Huyo jaji mkuu mwenyewe ni wa kanda yetu ya Ziwa. Au hata hilo hulijui? Kanda yetu ya ziwa ina hawa wafuatao:
1. Jaji mkuu, 2. IGP, 3. Mkuu wa JWTZ, 4. DPP, 5. Mwanasheria mkuu wa serikali, 6. Mlipaji mkuu wa serikali, 7. Mkuu wa nchi, 8. Mawaziri wengi ni wa kanda yetu kuliko kanda zingine. Hata Vice-Chancellor wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, chuo bora Tanzania ni wa kanda yetu.

Tunachotoa maoni ni kwamba si jambo jema kuwa na watu wazito kama hawa toka ukanda mmoja wa nchi. Ni maoni yetu tu ambayo yanaweza kuchukuliwa au kukataliwa.
Usitake niongee unachofikiria wewe, nimekwambia naangalia sana wateule wake wana impact gani katika utendaji wake.
Na pia mimi ninavyojua Rais yeyote duniani atachagua wateule ambao anadhani watakuwa wazalendo kwake.
Mfano Donald Trump wa US kamchagua mkwe kuwa mshauri wake n.k mfatilie Robet Mugabe wa Zimbabwe, Kagame na hata Museven, Zuma n.k wote wamechagua wateule ambao ni wazalendo kwao bila kuangalia ni ndugu yake, dini. Kabila n.k

Hiyo hoja yako ya teuzi za JPM kwamba zina upendeleo hazina mashiko.
 
Nawasalimu wote ,
Naomba niulize maswali kama ifuatavyo.

1. Katika kipindi hiki cha kuelekea miaka miwili ya kuwa madarakani Rais Magufuli. Je, mnaridhishwa na hali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii hapa Tanzania ?

2. Rais Magufuli amekuwa akishutumiwa na upinzani na asasi za kiraia kwa kuminya demokrasia na uhuru wa kujieleza. Je, mnakubaliana na kauli hizi ?

3.Kuna matukio mengi ya uvunjifu wa amani hapa Tanzania, ambapo baadhi ya watu wamepoteza maisha, kuumizwa na kusumbuliwa na kuelekezewa kidole utawala wa JPM. Je, mnadhani ni sahihi kumuhusisha Rais na utawala wake na kile kinachoendelea ?

4. Kuna viashiria vya kugawanyika kwa watanzania kutokana na mwenendo wa mambo yalivyo hapa Tanzania kuanzia kwa wanasiasa, bungeni na hata wafanyabiashara. Je, wakati haujafika kwa rais JPM kuleta suluhu ya Kitaifa ?

5. Rais JPM analaumiwa kwa kutoa hadharani maneno ya kuudhi na kushindwa kuchagua maneno kutokana na uhalisia wa mambo ambapo anatuhumiwa kulipasua Taifa na kuleta msuguano usio na umuhimu. Je, mnadhani shutuma hizi ni sahihi ?


Naomba mjibu maswali hayo kwa kadri mnavyoweza ili Watanzania waweze kupima maoni yenu.


Kishada.
Mkuu yakubidi uangalie mambo kwa mapana na si ya mtaa mmoja au wilaya mmoja tu mmarufu bali nchi nzima kwa ujumla.
Issue kuu ya Magufuri hataki watu kuiba au kufanya ufisadi wa mali ya umma .
Magufuri hataki watu au taasisi au kampuni isiolipa kodi za serikali hata Yesu alilipa kodi ya Kaisari
Magufuri hataki wazembe,kama una hormone za kizembe umekwenda na maji.
Magufuri hataki watu wanaoishi kihasara hasara akina mission town karudi kwenu ukalime.
Magufuri anapunguza urasimu na umangimeza na ndio hapo anatonesha kidonda,kufanya kazi kwa mazoea hakuna nafasi.
Pammoja na hayo nae Magufuri anayo mapungufu yake kama binadamu yeyote na ni ukweli uraisi hausomewi ,uraisi unaugobea,na unapigiwa kura na wananchi, zinahesabiwa kura,unashinda,unaapishwa ndio unakuwa raisi.Uraisi ni safari ndefu dont waste your ample energy discussing Magufuri give him time will judge him,its a new era,a new beginning,a new approach,A NEW KID ON THE BLOCK.
 
1. Hali ya kiuchumi na kijamii inaridhisha, kuhusu hali ya siasa watanzania hawaitaji siasa bali maendeleo

2. Wapinzani kila siku ni watu wa kushutumu mana hata kikwete walisema ni dhaifu na walisema wanaitaji mtu mwenye maamuzi magumu, kuhusu demokrasia na uhuru wa kujieleza bila maendeleo havina maana

3. Uvunjivu wa amani haujaanza leo, unakumbuka sumu walizopewa Mwandosya na Mwakyembe je ni Magufuli aliwapa? Kung'olewa kucha na meno kwa Ulimboka je ni Magufuli alifanya?

4. Hakuna watanzania waliogawanyika kisiasa, bungeni au wafanyabiashara sababu serikali ya Magufuli inawahudumia wananchi wote sawa bila kuangalia vyama, biashara au uwakilishi bungeni

5. Rais Magufuli ni mkweli na ni jasiri hivyo anaongea maneno yale hadharani ili wabadhirifu wa mali waelewe na waache ujinga.
Na ndio maana akasema KAZI TU.

Hivyo nakushauri acha propaganda na mawazo yako mgando.
Watanzania ni watu wavivu sana wakipewa kiongozi mzembe hii inchi yote itakuja gawanywa vipande na mabepari nacsababu Rais Magufuli anapigania nchi yake watanzania tunatakiwa kumuunga mkono kwa moyo mmoja kwa manufaa yataifa.

Hii demokrasia tunayoililia ndio waliyoitaka Libya n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Asee kunywa soda afu unambie ulipo nitalipia Mimi umetoa majibu stahiki kwa maswali stahiki
 
Asee kunywa soda afu unambie ulipo nitalipia Mimi umetoa majibu stahiki kwa maswali stahiki
Unajua watanzania inabidi wajifunze kujivunia vya kwao hata kama ni vidogo.
Sasa kila siku ni shutuma tu na maneno ya kipuuzi wanasema kwa Rais hadi inatukera wengine
 
Uongozi wowote unataka hekima kama ya Sulemani je anayo?
 
Kwani ww unaonaje au unaishi wapi ? Maana majibu unayo hapo.....!
 
Back
Top Bottom