Maswali matano muhimu kuhusu Rais Magufuli

Maswali matano muhimu kuhusu Rais Magufuli

Hizo kelele ni za waujumu uchumi na mafisadi

Hii kali.

In maana kila anayedadisi na kupiga kelele ni fisadi ? Kwa tafsiri hio Watanzania wengi wanadadisi hali kwa hivyo itakuwa mafiasadi ni wengi kuliko wasafi na hio = na Tanzania kuwa nchi ya mafisadi kweli ?
 
1. Hali ya kiuchumi na kijamii inaridhisha, kuhusu hali ya siasa watanzania hawaitaji siasa bali maendeleo

2. Wapinzani kila siku ni watu wa kushutumu mana hata kikwete walisema ni dhaifu na walisema wanaitaji mtu mwenye maamuzi magumu, kuhusu demokrasia na uhuru wa kujieleza bila maendeleo havina maana

3. Uvunjivu wa amani haujaanza leo, unakumbuka sumu walizopewa Mwandosya na Mwakyembe je ni Magufuli aliwapa? Kung'olewa kucha na meno kwa Ulimboka je ni Magufuli alifanya?

4. Hakuna watanzania waliogawanyika kisiasa, bungeni au wafanyabiashara sababu serikali ya Magufuli inawahudumia wananchi wote sawa bila kuangalia vyama, biashara au uwakilishi bungeni

5. Rais Magufuli ni mkweli na ni jasiri hivyo anaongea maneno yale hadharani ili wabadhirifu wa mali waelewe na waache ujinga.
Na ndio maana akasema KAZI TU.

Hivyo nakushauri acha propaganda na mawazo yako mgando.
Watanzania ni watu wavivu sana wakipewa kiongozi mzembe hii inchi yote itakuja gawanywa vipande na mabepari nacsababu Rais Magufuli anapigania nchi yake watanzania tunatakiwa kumuunga mkono kwa moyo mmoja kwa manufaa yataifa.

Hii demokrasia tunayoililia ndio waliyoitaka Libya n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Ww kijana mi mwaka wa pili nimemaliza elimu ya juu nipo nasota chunga ulimi wako, sio hivyo 2 tuna nyumba yetu imevunjwa nililelewa humo humi toka nazaliwa eti kwa utawala wa bwana wako ndio imekuwa tumevamia , kanyie kwenye matawi ya mabunju wenzio cio humu unakera kijanaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha magumu ekesha unaambiwa ufidadi sijuw,mafisad si mafsiem wnyewe iyo pesa iachiwe mabos wapate, na ss walala tupate tutumwe lkn unaambiwa pesa serikalini inakusanywa matirilion,misaada wanapewa matirilion ,pesa zilizookolewa kwa walaji matirilion baadae ajira hamna ,pesa imewekwa ktk hazina mitaani haipo,mara wapiga debe hawatakiwi,mara nyumba zivunjwe watu walale nje, ahadi za viwanda mwaka wa pili hata mradi wa mabanda ya kuku hamna ,kuongea sana kwa ukali na kamata kamata vitendo 0 ,ahadi zisotimizwa, upuuzi 2 la mana la kufaidika kwetu ss wananchi halionekani, CCHAFYAA!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawaomba tujielekeze kwenye masuali na ufafanuzi uelekee kwa undani kuhusu masuali yetu kwa faida ya wana JF wote.
 
mitindo huru: Kwa hayo uliyosema naomba ujibu maswali yafuatayo kwa hoja zako tano ulizotoa kwa mfuatano:
1. Umesema watanzania hawahitaji siasa bali maendeleo. Kwa uelewa wako maendeleo ni nini? Sisi wengine tunajua maendeleo ya nchi huonekana katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hata huyu unayemtetea amepata hicho cheo kupitia siasa. Pia
Nyerere alitufundisha kuwa ili nchi iendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Kwa hiyo nyanja ya siasa ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa. Kumbuka wabunge, mawaziri, Rais, Waziri mkuu na makamu wa Rais wote ni wanasiasa. Unasemaje kwamba hatuhitaji siasa wakati hata unaowatetea ni wanasiasa? Pia huyo unayemtetea bado anafanya siasa hata kwenye ziara zake tunaona anawapokea wanachama wanaojiunga na chama chake na pia yeye mwenyewe ni mwenyekiti wa chama cha siasa.
2. Umesema demokrasia na uhuru wa kutoa maoni na kujieleza havina maana, eti kinachotakiwa ni maendeleo tu. Je, kwa uelewa wako demokrasia na uhuru wa kutoa maoni/kujieleza ni vikwazo vya maendeleo? Mbona hata wewe umejieleza na kutoa maoni yako tunayoyajadili hapa JF? Je, kwa kufanya hivyo umekwamisha maendeleo?
3. Hoja yako ya tatu inaonyesha kwamba wewe mwenyewe unakiri wazi kwamba uvunjifu wa amani upo na ulikuwepo hata kabla ya mzee wako kuingia madaraka. Kwa hiyo unakiri wazi kwamba mzee wako ameshindwa kukomesha tatizo hili kama walivyoshindwa wengine? Kwa nini sasa unasema hakuna tatizo?
4. Umesema huyu jamaa habagui watu kivyama na kwa namna yoyote ile. Mbona viongozi wote wakubwa aliowateua wanatoka kanda ya ziwa tu? Mfano, IGP, DPP, Mkuu wa JWTZ, Mlipaji mkuu wa serikali, na mwanasheria wa serikali. pia mawaziri wengi ni wa kanda hiyohiyo. Mbona pia akienda kwenye majimbo ya wapinzani anawadhalilisha na kuwaambia wananchi kwamba walikosea kuchagua mtu wa upinzani na ndio maana hawana huduma fulani mfano maji?
5. Umesema hana maneno ya kuudhi bali anawapasha watu ukweli ili waache ujinga. Kumbuka alitamka hadharani kwamba mawaziri wake wengi ni wapumbavu. Kisha akasema wastaafu wengi wanawashwawashwa na ndio maana wanaongeaongea maneno. Je, mbona watu wakitumia maneno hayohayo kwake wanakamatwa na vyombo vya dola kwamba wamemkashfu?
 
1. Hali ya kiuchumi na kijamii inaridhisha, kuhusu hali ya siasa watanzania hawaitaji siasa bali maendeleo

2. Wapinzani kila siku ni watu wa kushutumu mana hata kikwete walisema ni dhaifu na walisema wanaitaji mtu mwenye maamuzi magumu, kuhusu demokrasia na uhuru wa kujieleza bila maendeleo havina maana

3. Uvunjivu wa amani haujaanza leo, unakumbuka sumu walizopewa Mwandosya na Mwakyembe je ni Magufuli aliwapa? Kung'olewa kucha na meno kwa Ulimboka je ni Magufuli alifanya?

4. Hakuna watanzania waliogawanyika kisiasa, bungeni au wafanyabiashara sababu serikali ya Magufuli inawahudumia wananchi wote sawa bila kuangalia vyama, biashara au uwakilishi bungeni

5. Rais Magufuli ni mkweli na ni jasiri hivyo anaongea maneno yale hadharani ili wabadhirifu wa mali waelewe na waache ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
baba wa taifa mwl nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, mojawapo ni uongozi bora na siasa safi. r ejea wino mwekundu, maendeleo bila demokrasia haiwezekani, madikteta wote waliotangulia ( iddi amini, mobutu seseseko kuku wa zobanga, bokasa, adolf hitler nk) waliziachia nchi zao majanga badala ya maendeleo, leo duniani nchi zenye demokrasia na utawala bora ndizo nchi zenye uchumi mkubwa USA vs. Russia, Japan vs. North Korea, Western Europe vs. Eastern Europe.
Unajua kila mwananchi ni mdahu wa maendeleo wa nchi yake, sasa mtu mmoja peke yake hawezi kujipachika jukumu hilo na wananchi wenzake wabakie watazamaji tu, mimi nafikiri mjinga ni yule ambaye anadhani yuko peke yake kwenye maendeleo ya nchi
 
Kwa hiyo kwa majibu yako , Siasa hii iliyopo ndio inapaswa kuwepo sio ? kwa sababu watanzania hawahitaji siasa lakini vyama vipo kikatiba hapa inakuwaje.

Kwa ufupi unaridhishwa.
Maendeleo kwanza siasa baadae. Hivi umeshafatilia siasa za nchi kubwa kiuchumi kama Uingereza, urusi, china, india na hata US yenyewe.
Pale kinachofanyika ni kiini macho cha siasa ila sio siasa.

Jiulize kwanini Putin wa Urusi alimaliza mda wake wa uongozi ila badae akarudi kwenye urais kwa mlango wa nyuma?
Je umewahi fatilia siasa za nchi ya china?

Hata marekani wenyewe wana malengo yao kama nchi.
US mtu atapiga kelele kwenye kampeni za uchaguzi ila mwisho wa siku ataenda kutimiza manifesto ya US ya miaka hamsini iliyopita.
Kwa kifupi siasa kwa hizi nchi zetu hazina tija sana zaidi ya kutuletea vibaraka katika nchi, ufisadi, mivurugano katika kuendesha nchi n.k sababu kila upande unahisi una haki na nchi hata kama ni mamluki kwa kigezo cha demokrasia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom