Nawasalimu wote ,
Naomba niulize maswali kama ifuatavyo.
1. Katika kipindi hiki cha kuelekea miaka miwili ya kuwa madarakani Rais Magufuli. Je, mnaridhishwa na hali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii hapa Tanzania ?
2. Rais Magufuli amekuwa akishutumiwa na upinzani na asasi za kiraia kwa kuminya demokrasia na uhuru wa kujieleza. Je, mnakubaliana na kauli hizi ?
3.Kuna matukio mengi ya uvunjifu wa amani hapa Tanzania, ambapo baadhi ya watu wamepoteza maisha, kuumizwa na kusumbuliwa na kuelekezewa kidole utawala wa JPM. Je, mnadhani ni sahihi kumuhusisha Rais na utawala wake na kile kinachoendelea ?
4. Kuna viashiria vya kugawanyika kwa watanzania kutokana na mwenendo wa mambo yalivyo hapa Tanzania kuanzia kwa wanasiasa, bungeni na hata wafanyabiashara. Je, wakati haujafika kwa rais JPM kuleta suluhu ya Kitaifa ?
5. Rais JPM analaumiwa kwa kutoa hadharani maneno ya kuudhi na kushindwa kuchagua maneno kutokana na uhalisia wa mambo ambapo anatuhumiwa kulipasua Taifa na kuleta msuguano usio na umuhimu. Je, mnadhani shutuma hizi ni sahihi ?
Naomba mjibu maswali hayo kwa kadri mnavyoweza ili Watanzania waweze kupima maoni yenu.
Kishada.