Maswali matano muhimu kuhusu Rais Magufuli

Maswali matano muhimu kuhusu Rais Magufuli

Tuombe Mungu muda wake uishe haraka tuchague mtu sahihi.

Swali tu,
Hivi kiukweli watanzania wamewahi kuchagua rais wamtakaye? Kwanza nina wasiwasi kama kiujumla waliwahi kuwa na hilo chaguo sembuse kuchagua, mtanisamehe, mawazo yangu lakini
 
mitindo huru: Kwani kwa uelewa wako maendeleo ni nini? Tujuavyo wengine maendeleo katika nchi ni hatua ya kusonga mbele kwa mafanikio Kisiasa, kiuchumi, na kijamii.
Kwa uelewa wangu maendeleo ya nchi ni jambo la kutoka katika hali duni kwenda hali nzuri kiuchumi, kiteknolojia, kijamii, kiuongozi n.k ila siasa ni ya mwisho.
Lakini siasa kwangu sio maendeleo sababu kuna nchi zimeendelea bila kuwa na siasa bali ni mifumo waliyoiweka kama nchi na nchi zao zina maendeleo kuliko sisi waafrika walala hoi tunaokesha kuwaza siasa badala ya maendeleo.

Je unajua rais wa uchina anachaguliwa na watu nane tu?

Je unajua siasa za marekani ni kiini macho tu, bali wanamuweka rais wao watu wachache kulingana na wakati ulivyo?

Je unajua kwanini US alimuua Gadafi ambaye wengi mliaminishwa ni gaidi?

Kwanini hadi leo Hitler anapendwa ujerumani ingawa alikuwa Dictator?

Naomba majibu ya hayo maswali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivyo nakushauri acha propaganda na mawazo yako mgando.
Watanzania ni watu wavivu sana wakipewa kiongozi mzembe hii inchi yote itakuja gawanywa vipande na mabepari nacsababu Rais Magufuli anapigania nchi yake watanzania tunatakiwa kumuunga mkono kwa moyo mmoja kwa manufaa yataifa.

Hii demokrasia tunayoililia ndio waliyoitaka Libya n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
umejibu vizuri ila umevurunda hapo kwenye blue. sasa wewe unajibu hoja za mawazo mgando. Na majibu yako basi nikiyaita mgando nimekosea!
 
Kwa uelewa wangu maendeleo ya nchi ni jambo la kutoka katika hali duni kwenda hali nzuri kiuchumi, kiteknolojia, kijamii, kiuongozi n.k ila siasa ni ya mwisho.
Lakini siasa kwangu sio maendeleo sababu kuna nchi zimeendelea bila kuwa na siasa bali ni mifumo waliyoiweka kama nchi na nchi zao zina maendeleo kuliko sisi waafrika walala hoi tunaokesha kuwaza siasa badala ya maendeleo.

Je unajua rais wa uchina anachaguliwa na watu nane tu?

Je unajua siasa za marekani ni kiini macho tu, bali wanamuweka rais wao watu wachache kulingana na wakati ulivyo?

Je unajua kwanini US alimuua Gadafi ambaye wengi mliaminishwa ni gaidi?

Kwanini hadi leo Hitler anapendwa ujerumani ingawa alikuwa Dictator?

Naomba majibu ya hayo maswali

Sent using Jamii Forums mobile app
Yote hiyo ni siasa ya namna yake. Siasa huitoi kwenye maisha ya watu na jamii nzima endapo kuna kiongozi wa kuongoza hiyo jamii
 
Ww kijana mi mwaka wa pili nimemaliza elimu ya juu nipo nasota chunga ulimi wako, sio hivyo 2 tuna nyumba yetu imevunjwa nililelewa humo humi toka nazaliwa eti kwa utawala wa bwana wako ndio imekuwa tumevamia , kanyie kwenye matawi ya mabunju wenzio cio humu unakera kijanaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza nitake radhi sababu mimi sio kijana,

cha pili ni kwamba mimi sina bwana.

Cha tatu unatakiwa ujue kwamba tatizo la ajira ni la dunia nzima sababu ya maendeleo ya teknolojia, kwa hiyo tumia akili yako vizuri na elimu uliyopata chuo kuweza kujiajiri na nakuhakikishia tanzania bado ni virgin country yenye fulsa za kila aina, sio unang'ang'ania Dsm halafu una lalamika, kuna mikoa huko utajiri uko njenje ukiitaji msaada wa hilo nijulishe.

Cha nne ni kwamba kama umebomolewa nyumba yako kisheria tafuta wakili au muone mbunge wenu mliomchagua muungane na wenzako mliobomolewa pamoja mkadai fidia kisheria.

In Our Time Let Us Do Good


Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. HAPANA

2. NDIYO

3. NDIYO

4. SIJUI

5. NDIYO

Acha nikusanye paper langu. 100% sikosi hapo. Nikianguka sana basi 80% kwa maana ya kwamba kila swali ni 20% marks
 
mitindo huru: Kwa hayo uliyosema naomba ujibu maswali yafuatayo kwa hoja zako tano ulizotoa kwa mfuatano:
1. Umesema watanzania hawahitaji siasa bali maendeleo. Kwa uelewa wako maendeleo ni nini? Sisi wengine tunajua maendeleo ya nchi huonekana katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hata huyu unayemtetea amepata hicho cheo kupitia siasa. Pia
Nyerere alitufundisha kuwa ili nchi iendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Kwa hiyo nyanja ya siasa ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa. Kumbuka wabunge, mawaziri, Rais, Waziri mkuu na makamu wa Rais wote ni wanasiasa. Unasemaje kwamba hatuhitaji siasa wakati hata unaowatetea ni wanasiasa? Pia huyo unayemtetea bado anafanya siasa hata kwenye ziara zake tunaona anawapokea wanachama wanaojiunga na chama chake na pia yeye mwenyewe ni mwenyekiti wa chama cha siasa.
2. Umesema demokrasia na uhuru wa kutoa maoni na kujieleza havina maana, eti kinachotakiwa ni maendeleo tu. Je, kwa uelewa wako demokrasia na uhuru wa kutoa maoni/kujieleza ni vikwazo vya maendeleo? Mbona hata wewe umejieleza na kutoa maoni yako tunayoyajadili hapa JF? Je, kwa kufanya hivyo umekwamisha maendeleo?
3. Hoja yako ya tatu inaonyesha kwamba wewe mwenyewe unakiri wazi kwamba uvunjifu wa amani upo na ulikuwepo hata kabla ya mzee wako kuingia madaraka. Kwa hiyo unakiri wazi kwamba mzee wako ameshindwa kukomesha tatizo hili kama walivyoshindwa wengine? Kwa nini sasa unasema hakuna tatizo?
4. Umesema huyu jamaa habagui watu kivyama na kwa namna yoyote ile. Mbona viongozi wote wakubwa aliowateua wanatoka kanda ya ziwa tu? Mfano, IGP, DPP, Mkuu wa JWTZ, Mlipaji mkuu wa serikali, na mwanasheria wa serikali. pia mawaziri wengi ni wa kanda hiyohiyo. Mbona pia akienda kwenye majimbo ya wapinzani anawadhalilisha na kuwaambia wananchi kwamba walikosea kuchagua mtu wa upinzani na ndio maana hawana huduma fulani mfano maji?
5. Umesema hana maneno ya kuudhi bali anawapasha watu ukweli ili waache ujinga. Kumbuka alitamka hadharani kwamba mawaziri wake wengi ni wapumbavu. Kisha akasema wastaafu wengi wanawashwawashwa na ndio maana wanaongeaongea maneno. Je, mbona watu wakitumia maneno hayohayo kwake wanakamatwa na vyombo vya dola kwamba wamemkashfu?
Naomba nikujibu kwa kifupi sababu hoja zako nyingi zimemlenga mtu binafsi ambaye ni raisi JPM na sio mifumo kama nchi. Najua rais ana mapungufu hasa katika kuteua wateule wake ambao anashirikiana nao kutimiza ilani ya chama chake.

JPM kuteua watu wa ukanda wake sina hakika na hilo sababu nikiangalia kuna
Waziri mkuu(mtwara) ,
Jaji mkuu( muislamu),
Spika wa bunge ( nafikiri anatokea dodoma).
Sasa hapo ndio penye msingi wa nchi.
Mimi simetetei rais JPM bali najaribu kuelezea kile kinachoendelea katika nchi yangu pendwa Tanzania. sababu tukikaa kimya mabepari hayachelewi kuaminisha watu uongo kwa kigezo cha siasa, demokrasia halafu mwisho wa siku watuletee viongozi vibaraka wao warudi kunyonya tena madini yetu. Kuaribu wanyama wetu kwa ujangili, kuharibu vijana wetu kwa madawa ya kulevya n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. HAPANA

2. NDIYO

3. NDIYO

4. SIJUI

5. NDIYO

Acha nikusanye paper langu. 100% sikosi hapo. Nikianguka sana basi 80% kwa maana ya kwamba kila swali ni 20% marks

Ufafanuzi na mifano ndio hutowa marks nyingi.

Vigezo na masharti kuzingatiwa
 
mitindo huru: Nilifikiri nahojiana na mtu mwenye upeo wa mambo na anayeifahamu TZ, kumbe dhaifu hivyo kiufahamu. Huyo jaji mkuu mwenyewe ni wa kanda yetu ya Ziwa. Au hata hilo hulijui? Kanda yetu ya ziwa ina hawa wafuatao:
1. Jaji mkuu, 2. IGP, 3. Mkuu wa JWTZ, 4. DPP, 5. Mwanasheria mkuu wa serikali, 6. Mlipaji mkuu wa serikali, 7. Mkuu wa nchi, 8. Mawaziri wengi ni wa kanda yetu kuliko kanda zingine. Hata Vice-Chancellor wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, chuo bora Tanzania ni wa kanda yetu.

Tunachotoa maoni ni kwamba si jambo jema kuwa na watu wazito kama hawa toka ukanda mmoja wa nchi. Ni maoni yetu tu ambayo yanaweza kuchukuliwa au kukataliwa.
 
Ufafanuzi na mifano ndio hutowa marks nyingi.

Vigezo na masharti kuzingatiwa

Failure to follow instructions.......
Mtunzi wa mtihani amesema "Naomba mjibu maswali hayo kwa kadri mnavyoweza ili Watanzania waweze kupima maoni yenu."
Kwa nionayo mimi, maswali yake haupaswi kushuka essay. Unatizamia mkuu.
 
Back
Top Bottom