Maswali magumu: Viko wapi visu vya Mahita?

Maswali magumu: Viko wapi visu vya Mahita?

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
KWANINI serikali inahangaika kupandikiza hisia za udini na ugaidi katika siasa? Mwaka 2005 ilikitangaza Chama cha Wananchi (CUF) kuwa cha kidini na kigaidi. Sasa hivi inasema vitu viwili.

Kwanza, inasema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kidini, kikabila na kigaidi. Pili, inawatumia makada wake kutamka kwamba chama hicho kitakufa.

Tunajua kuwa inafanya hivyo kunusuru Chama Cha Mapinduzi (CCM). Lakini kwa tabia hii, tutaiita serikali au genge la wapika propaganda za kigaidi?

Hebu tuulizane. Watawala wanaotumia na kupandikiza hisia za udini na ukabila kama mbinu ya kuwashinda wapinzani wao wanastahili kuaminiwa tena? Wanaweza kuzungumzia amani na utulivu?

Watawala wanaoingiza Jeshi la Polisi katika misukosuko ya kiitikadi, wanadhani wanapanda mbegu ya amani na ustahamilivu? Chama cha siasa kinachotegemea nguvu za dola kama njia ya kupata ushindi kina haki ya kuendelea kuaminiwa?

Tukumbushane. Mwaka 2005, katikati ya joto kali la Uchaguzi Mkuu, baada ya kubanwa na CUF, serikali ilimtumia Mkuu wa Jeshi la Polisi wa wakati ule, Inspekta Jenerali Omar Mahita, kutisha wapiga kura.

Mahita akajidhalilisha, akaibukia kwenye TV akiwa na visu vilivyopakwa rangi za bendera ya CUF, akisema jeshi lake limekamata kontena la visu ambavyo chama hicho kilikuwa kinakusudia kufanyia ugaidi.

Hadi leo hawajatueleza visu hivyo vilipelekwa wapi. Hatujaambiwa kontena hilo liliishia wapi. Hatujasikia mtu yeyote au kiongozi wa CUF amekamatwa kwa ugaidi. Wala hakuna kesi yoyote mahakamani dhidi ya viongozi au wanachama wa CUF kutokana na tukio hilo.

Ni dhahiri lilikuwa tukio la kupika na kuidhalilisha CUF mbele ya umma. Ilikuwa mbinu ya ushindi mchafu. Na kwa kuwa iliwasaidia kuipiku CUF na kuidhoofisha, sasa wamedhani mbinu ile ile itakuwa msaada kwao kuimaliza CHADEMA.

Ndiyo maana na tambo zao eti CHADEMA kitakufa kabla ya 2015. Ndiyo sababu ya kauli za kidini, kikabila ka kigaidi dhidi ya CHADEMA. Wanapanda mbegu chafu katika siasa za Tanzania, kwa hofu tu ya kuondoka madarakani!

Halafu wanathubutu kusimama majukwaani kutamka kwamba wapinzani wana uchu wa madaraka. Yapi? Nani anang’ang’ania madaraka kati ya wale waliokaa madarakani kwa miaka 50 na wale wanaotaka kuingia madarakani kwa mara ya kwanza?

Mbinu chafu za kutumia vyombo vya dola, udini, ukabila na ugaidi hazioneshi uzoefu, weledi, wala umakini katika kutawala. Kwa maana nyingine, tunaweza kusema miaka 50 ya kukaa madarakani haijawasaidia watawala wetu. Bado wanabahatisha!

Zaidi ya hayo, wanatujengea Jeshi la Polisi lisilo adilifu, lililo tayari kuingizwa kwenye michezo michafu ya kihuni na kihalifu kwa ajili ya kutukuza watawala.

Kama leo tungeulizana, upo wapi uadilifu wa Mahita? Tunakuwa na uhakika gani na uadilifu wa viongozi wa Jeshi la Polisi baada ya Mahita?

Kwanini serikali inataka kulifikisha Jeshi la Polisi mahali ambapo halitaheshimika wala kuaminika? Kwanini inatumia vyombo vya dola kukandamiza haki na kulinda uovu?

Na baada ya yote yaliyotokea katika nchi za wenzetu – Syria, Tunisia, Misri, Libya, Kenya, Zimbabwe na kwingineko, kwanini watawala hawajifunzi kwamba matumizi ya Jeshi la Polisi hayawezi kuzuia wimbi la mabadiliko?

Jambo moja ambalo watawala hawajaelewa ni kwamba walifanikiwa kuidhoofisha CUF kwa sababu kilishitukizwa. CHADEMA kimeandaliwa, na kimejiandaa kisaikolojia na kimkakati kushinda propaganda hizi.

Tatizo si CHADEMA. Hoja si CHADEMA. Hoja ni mabadiliko. Yatakuja tu. Kama si kwa kupitia mlangoni, yatapitia dirishani. Nguvu ya mabadiliko ni baraka. Hata ukifunga milango, itapenya!

Bahati mbaya, watawala hawajasoma alama za nyakati. Wananchi wa sasa wameshaelewa mbinu zao. Maoni ya kizazi cha leo cha Watanzania ni kuondoa mfumo wa utawala uliodumu kwa miaka 50.

Elimu ya uraia iliyotolewa kwa wananchi wa sasa – ikichangiwa na harakati za vyama vya siasa, asasi za kiraia na udhaifu wa serikali yenyewe katika kuhudumia wananchi – imesaidia kuamsha wananchi kuamka. Wanajua haki zao, na wapo tayari kupambana na dhalimu yeyote.

Kwa muda sasa, kutokana na mwenendo wa serikali, wananchi wamejenga hasira dhidi ya watawala, kiasi kwamba anapopatikana hata mtu mmoja wa kupambana na watawala hao anaonekana shujaa mbele ya umma.

Na jitihada zozote za watawala kumdhulumu mtu yeyote anayekosoa au kusumbua watawala huzaa chuki kutoka kwa umma.

Ndiyo maana wananchi wanaelewa fika kwamba ugaidi wa CHADEMA unaozungumzwa sasa ni siasa za mchoko wa CCM na serikali yake. Ni propaganda na hujuma zile zile walizofanyiwa CUF miaka ile.

Ni hatua za mwisho za kutapatapa kwao baada ya kushindwa siasa za hoja majukwaani na katika nyanja nyingine rasmi. Ni teke zito la ngamia anayekata roho!

Kizazi cha leo kinachotafuta ukombozi wa pili wa Tanzania hakiwezi kuogopa kuitwa magaidi. Kinajua kuwa hata ikibidi, CUF na CHADEMA si wa kwanza kuitwa hivyo.

Mifano ni mingi, lakini nitatoa michache kukazia hoja hii. Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, aliitwa gaidi baada ya kutishia masilahi ya watawala.

Alitafutwa kunyongwa. Alihukumiwa kifungo cha maisha jela. Kumbukumbu zinaonesha yeye mwenyewe aliwahi kukiri makosa yapatayo 156 ya kigaidi dhidi ya serikali ya Kaburu!

Mara kadhaa, utawala wa kikaburu, chini ya Rais P. W. Botha uliwahi kumtaka Mandela akanushe kuhusika na ugaidi ili rais amsamehe, amwondolee kifungo.

Mandela alikataa! Aliona ni bora aendelee kuitwa gaidi iwapo ugaidi huo ni harakati za kuwakomboa wananchi wa Afrika Kusini.

Lakini watawala wa Afrika Kusini, hawakuanza na Mandela. Walianza na Chama chake, African National Congress (ANC), kilichoasisiwa mwaka 1912. Kati ya 1961 na 1990, watawala na maswahiba wao wa ndani na nje walitangaza na kutuhumu ANC kuwa ni chama cha kigaidi.

Historia imekitetea. Mwaka 1994 gaidi akawa rais; na chama cha kigaidi kikawa chama tawala!

Hoja yangu hapa ni kwamba Serikali ya Tanzania inajua kuwa CHADEMA si chama cha kigaidi. Inajua ni chama cha siasa kinachowapa watawala wakati mgumu sasa. Inaona kinaungwa mkono na wananchi wengi, hasa vijana.

Inaona kimebeba dhima ya mabadiliko. Inajaribu kujenga mazingira ya kutengeneza hofu miongoni mwa Watanzania. Inadhani kwamba itakapotangaza CHADEMA kuwa chama cha kigaidi kitakosa mashabiki, kitapwaya na kitakufa!

Bahati mbaya, serikali haijasoma hata saikolojia ya umma inaoulazimisha ukubali suala hili. Hadi sasa viongozi wa serikali na CCM hawajajua kwamba wanafanya kazi nzuri ya kisiasa kwa manufaa ya CHADEMA.

Hawajajua kwamba kwa kelele hizi wanakipigia debe. Hawajajua kwamba kwa tuhuma hizi wanakifanyia kampeni. Hawajajua kwamba kwa kukisingizia ugaidi wanakifanya kionewe huruma hata na wale waliokuwa hawajakiunga mkono. Hawajajua kwamba kwa kukisakama namna hii wanaonesha kwamba wanakiogopa.

Kimsingi, wanataka kuilazimisha CHADEMA ifanye ugaidi kama wa kina Mandela. Inavyoonekana, wameshindwa kujifunza kutokana na historia.

Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga, hakufika hapo kirahisi. Miongoni mwa misukosuko ya kisiasa iliyompata ni pamoja na kuitwa gaidi, mhaini na kufungwa zaidi ya mara tisa. Haikuzuia harakati za kuleta mabadiliko Kenya. Leo wana katiba mpya, sisi bado tunang’ang’ania mambo yale yale!

Mwaka 1995 viongozi wa CCM walitumia mikanda ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda kutisha wananchi, eti wakichagua upinzani wataleta vita kama ya Rwanda. Mbinu na hofu hiyo haviwezi kufanya kazi leo.

Watawala wetu wa sasa wasipopata mwanga mpya, iwapo wataendelea kupanda mbegu ya udini, ukabila na ugaidi wa kisiasa, wananchi wapenda mabadiliko watatumia udini, ukabila na ugaidi huo huo kuwaondoa madarakani. Lakini nchi itakuwa imegawanyika, na imechafuka. Badala ya kuwa tishio, ugaidi unaweza kugeuka silaha ya mabadiliko.

Watawala wasipotaka kutumia hoja kukabiliana na nguvu ya kisiasa ya CHADEMA, wakawekeza kwenye hila na dhana ya ugaidi; kama watafunga milango ya hoja na kutumia mabavu ya vyombo vya dola, wasidhani hawatavuna zao la mbegu wanayopanda.

CHADEMA wako katika kipindi kigumu. Lakini ni kipindi kizuri, chenye rutuba kisiasa, kwa sababu ‘wanasaidiwa’ na CCM na serikali. Ni kipindi pekee katika historia ya mageuzi nchini ambapo chama tawala kinafanya siasa za kujiua na kukuza wapinzani. Tulalamike? Tushangilie?

Imeandikwa na Ansebert Ngurumo.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mwandishi wa hii makala atakuwa ni mchumia tumbo.

Anauliza swali halafu anajijibu yeye mwenyewe.
 
Mwandishi awe anachumia tumbo au vinginevyo mimi nimefurahishwa na huu umaliziaji wake, "CHADEMA wako katika kipindi kigumu. Lakini ni kipindi kizuri, chenye rutuba kisiasa, kwa sababu
‘wanasaidiwa’ na CCM na serikali. Ni kipindi pekee katika historia ya mageuzi nchini ambapo chama tawala kinafanya siasa za kujiua na kukuza wapinzani".

Chezea propaganda za ccm kila cha Watanzania ni cha ccm! Na ccm ndiyo yenye hati miliki ya kutawala Tanzania. Wanajiona watatawala milele.
 
Mwandishi wa hii makala atakuwa ni mchumia tumbo.

Anauliza swali halafu anajijibu yeye mwenyewe.

Hivi kati ya wewe Sumu na muandishi wa makala mchumia tumbo ni nani?! Kama kuandika ukweli ni uchumia tumbo basi wewe unaye andika uwongo ni mchumia dhambi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
hakuna anayejua nyumbani kwa mahita?tanzania kuna vituko sana,yani lile jambawazi nalo lilikuwa IGP!
 
Mwandishi wa hii makala atakuwa ni mchumia tumbo.

Anauliza swali halafu anajijibu yeye mwenyewe.

Saumu Mohamed,wewe si ulishafukuzwa kazi ya usekretari kitengo cha upigaji chapa- chadema,naona Marando kaunasa mpango wako wewe na magamba wenzako.,
 
Mwandishi wa hii makala atakuwa ni mchumia tumbo.

Anauliza swali halafu anajijibu yeye mwenyewe.

Mwenyewe unajiona ni bonge la spin doctor! Ishukuru sana JF imekupa ajira Lumumba...Back kwenye mada; Mleta uzi umeuliza swali la msingi sana:- Yale Majambia ya Mahita mliyoyatangaza na kuwaaminisha watanzania kuwa CUF ni chama cha Kidini kigaidi yako wapi? Lini mtawaomba msamaha CUF na Watanzania?
 
Mwandishi wa hii makala atakuwa ni mchumia tumbo.

Anauliza swali halafu anajijibu yeye mwenyewe.

yaani we jamaa comments zako ka za mama mwenye mimba changa!
unawashwa?
 
Wapinzani waungane...kwneye chaguzi za ubunge na urais hapo ndipo patakuwa nafuu yao wakisimama mmoja mmoja hawataweza ufisadi wa CCM!wapunguze sana nafasi zao Bungeni wakipata zaidi ya nusu......fitna kwisha wataweka Spika wao,watapitisha mambo yao na mengi ya msingi!!waanzie kwa mstaafu Tendwa anaetaka kufia akiwa kazini...wabadilishe sheria ya vyama kuungana bila masharti wkaikubaliana tu iwe imetosha!
 
tatizo wanazani wale wadanganyika wa 2005 wanaendelea kuwa na influence katika jamii ya kizazi hiki?
 
Wapinzani waungane...kwneye chaguzi za ubunge na urais hapo ndipo patakuwa nafuu yao wakisimama mmoja mmoja hawataweza ufisadi wa CCM!wapunguze sana nafasi zao Bungeni wakipata zaidi ya nusu......fitna kwisha wataweka Spika wao,watapitisha mambo yao na mengi ya msingi!!waanzie kwa mstaafu Tendwa anaetaka kufia akiwa kazini...wabadilishe sheria ya vyama kuungana bila masharti wkaikubaliana tu iwe imetosha!
yani uungane na wale wanaosifiwa na Kinana,hakuna kitu kama hicho....either with us or with the enemy!!tuache unafiki.
 
Cuf ni kutojijua au wako kwenye mtanziko na mhemuko wa ndoa (ushirika) vinginevyo kama CUF kingekuwa chama makini kilitakiwa kukikaba koo ccm waeleze kinaga ubaga kuhusu ugaidi wao na lile kontena la visu na majambia kabla ya kukubali ndoa na ccm.

Ukienda mbali zaidi na kukuna kichwa maana yake ni kwamba ccm wamefunga ndoa ya ushirika na chama kilicho ingiza kontena la visu na majambia, kwa maana hiyo ilikuwa shida kwa visu na majambia ya cuf kabla ya ndoa lakini baada ya ndoa wanandoa hao waliingia vyumbani na kusamehena!

Na je, Vipi ile sheria ya ugaidi inayo sema kikao cha magaidi lazima kiwe na watu kuanzia watatu na kuendelea? Na vipi kuhusu mantiki ya anaye wasiliana na gaidi naye ni gaidi?!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hivi kati ya wewe Sumu na muandishi wa makala mchumia tumbo ni nani?! Kama kuandika ukweli ni uchumia tumbo basi wewe unaye andika uwongo ni mchumia dhambi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Mkuu, kwa kum quote kwako huyo Kinaja umemuongezea Bonus leo Lumumba
 
HUo ni unafiq mbona hamkuwasaidia wakati wanachafuliwa kipindi kile na mahita?.kwahiyo mliwasaliti?kwanini?
 
Kuonesha mapanga na kusema CUF ni chama cha waislam ni CCM kuuzalilisha uislam. Nashangaa waislam wanaoshabikia CCM
 
huyo Ansebert Ngurumo ni mnafiki,
alikuwa wapi kuhoji haya.Anaitumia cuf kujibia hoja za cdm.
Tunajua kwamba cuf ilikuwa ni propaganda na sote tulishabikia cuf ife.
Sasa leo mnataka kuonesha cuf ilionewa ili iwe hoja hata kwa cdm inaonewa.
cdm ni kweli inashiriki matukio ya kigaidi mf lwakatare
Mtasema mnasingiziwa na ccm lakini si kweli cdm ni ugaidi na ukristo full stop
 
Back
Top Bottom