Maswali kwa Mbunge wangu: MH WENJE

Maswali kwa Mbunge wangu: MH WENJE

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,314
Mimi ni mwanchama wa chadema na ni mkaa wa mwanza,kuna mambo nimekuwa nikijiuliza,
1.mbele ya pamba police post kuna ujenzi unaendelea pale yapata miezi 8 na kwa muonekano ujenzi na vifaa wanavyotumia havina kiwango kabisa japo mimi sio injinia.
2.stand kuu zinakoingilia daladala za airport na kutokea kuna mashimo makubwa sana yana miezi kadhaa pale.
3,kuna ujenzi unaendelea mlango mmoja ambao wanaziba shimo week karibia 2 sasa hauna kiwango pia.
3.kupaki gari mjini tunaambiwa tulipie kwa kutwa sh 900 toka 500 kuna uhalali wowote?
Naomba kupata ufafanuzi najua ukiwa kama mbunge hutoi pesa mfukoni ila una jukumu la kufutilia .
 
mkuu na hapo nadhani hujamaliza,
maeneo ya VOIL kipo kipande cha mita kumii karibu na reli, sasa mwezi wa tatu huu,
na buzuruga - nyasaka - pasiansi/kilimahewa huu ni mwaka wa pili
Tenda zote hizi amepewa Nyanza Road Works - anaitwa mwekezaji wa ndani
Mwisho wa siku ndo anashindwa kumaliza project, budget kila mwaka inazidi kupaa, kazi inaharibika
 
Kupaki gari kwa kutwa Sh900? Kwa mwezi Sh27,000 kwa mwaka Sh324,000...Meya Chadema, Mbunge Chadema, Madiwani wengi ni wa Chadema.
 
Ki ukweli hapa panahitaji majibu,rafiki yangu Wenje si uzi wa kudharau,tunakuomba ujitokeze utupatie majibu mkishirikiana na Kiwia kwa barabara la Buzuruga hadi Pasiansi.
 
Kupaki gari kwa kutwa Sh900? Kwa mwezi Sh27,000 kwa mwaka Sh324,000...Meya Chadema, Mbunge Chadema, Madiwani wengi ni wa Chadema.
Hayakuhusu, funga bakuli lako chafu!
 
Kipande cha pale voil kiko chini ya taroads ambacho kinawekewa zege lenye nondo na kufanya kazi ya pale kuwa ngumu kutokana na kutokuwa na diversion hivyo kuradhimisha mkandarasi kufanya nusu upande ilikuweza kuruhusu flow ya traffic na curing pia,mradi wa k/hewa buzuruga ambao contractor ni nyaza unategemea fedha za european unioun kwa hiyo wanaendesha mradi kotokana na flow ya pesa.
 
Mimi ni mwanchama wa chadema na ni mkaa wa mwanza,kuna mambo nimekuwa nikijiuliza,
1.mbele ya pamba police post kuna ujenzi unaendelea pale yapata miezi 8 na kwa muonekano ujenzi na vifaa wanavyotumia havina kiwango kabisa japo mimi sio injinia.
2.stand kuu zinakoingilia daladala za airport na kutokea kuna mashimo makubwa sana yana miezi kadhaa pale.
3,kuna ujenzi unaendelea mlango mmoja ambao wanaziba shimo week karibia 2 sasa hauna kiwango pia.
3.kupaki gari mjini tunaambiwa tulipie kwa kutwa sh 900 toka 500 kuna uhalali wowote?
Naomba kupata ufafanuzi najua ukiwa kama mbunge hutoi pesa mfukoni ila una jukumu la kufutilia .

mkuu pole sana kwa changamoto hizo,
lakini mbona uhulizii kuhusu MAISHA BORA KWA KILA MTANZANZANIA? Maana hili nalo ni la muhimu sana kwani huu ni mwaka wa 7 sasa hakuna kitu.
 
Kupaki gari kwa kutwa Sh900? Kwa mwezi Sh27,000 kwa mwaka Sh324,000...Meya Chadema, Mbunge Chadema, Madiwani wengi ni wa Chadema.
rais thithiem,waziri mkuu thithiem,madam spika thithiem katibu mkuu kiongozi thithiem,mfumo wote serikari thithiem.migomo kula kukicha.hushangai hilo.
 
Mkuu kwa hiyo Chadema nao wanapata Excuse ya kufanya ufisadi sasa kwa nini mnawadanganya wananchi kuwa mnataka kuwakomboa.
 
Kwa kuwa halimashauri ipo chini ya cdm wao ndio wanakusanya ushuru na kuna kero ndogondogo wanaweza kuzitatua bila kuhangaika na serekali ya sisiem,kama wanavyojitahidi kwenye usafi.ni vizuri tukosoane kuliko kukosolewa
 
Mkuu kwa hiyo Chadema nao wanapata Excuse ya kufanya ufisadi sasa kwa nini mnawadanganya wananchi kuwa mnataka kuwakomboa.
Nani alikwambia kuwa hizo hela zinaingia kwenye mifuko ya Chadema?
 
Mimi ni mwanchama wa chadema na ni mkaa wa mwanza,kuna mambo nimekuwa nikijiuliza,
1.mbele ya pamba police post kuna ujenzi unaendelea pale yapata miezi 8 na kwa muonekano ujenzi na vifaa wanavyotumia havina kiwango kabisa japo mimi sio injinia.
2.stand kuu zinakoingilia daladala za airport na kutokea kuna mashimo makubwa sana yana miezi kadhaa pale.
3,kuna ujenzi unaendelea mlango mmoja ambao wanaziba shimo week karibia 2 sasa hauna kiwango pia.
3.kupaki gari mjini tunaambiwa tulipie kwa kutwa sh 900 toka 500 kuna uhalali wowote?
Naomba kupata ufafanuzi najua ukiwa kama mbunge hutoi pesa mfukoni ila una jukumu la kufutilia .

Mimi pia ni mkazi wa mwanza na nipo mwanza, sijaridhika kabisa na utendaji wa halmashauri inayosimamiwa na Chadema kama ilivyokuwa kwa CCM mambo ni yaleyale, kumbe hapa tatizo sio chama ni watu.
 
Nani alikwambia kuwa hizo hela zinaingia kwenye mifuko ya Chadema?

Jasusi, hizo pesa ndio zimefanya Meya wa Jiji la Mwanza (Chadema) kupigwa chini kwa ufisadi...ebu tuambie sheria za Jiji zinatungwa na nani?
 
Last edited by a moderator:
Unajua hawa jamii ya kina Wenje na chama chao hawakujiandaa kuongoza hizi halmashauri kama ambavyo hawajajiandaa kuongoza nchi yetu.budget ya halmashauri wanapitisha wao chini ya mayor wa chadema sasa kwa nini wapandishe tozo la parking kwa asilimia karibu mia moja
.Ukumbuke hata Moshi ilitokea hivyo kwa dala dala na mabasi mpaka waligoma.kuendesha nchi is not like sipping mbege my dears.
 
Mh Wenje na Mh Mnyika mnalaumiwa sana na wananchi wenu
 
Madiwani wa Chadema ndio wengi katika halmashauri ya Jiji la Mwanza na ndio wametoa Meya wamepitisha sheria ya Jiji kupaki magari kwa kutwa ni Sh900 wastani wa magari 500 kwa mwezi wanakusanya 13,500,000 kwa mwaka wanakusanya kiasi cha 162,000,000 kwa gari 500 tu...hizi pesa zinakwenda wapi? Wenje wasaidie wakazi wa Mwanza.
 
Ulizia hayo matrilioni yaliyokutwa huko uswisi kwanza mkuu !!!!!!
 
Pro-Chadema bana kwa hiyo wewe kujadili mambo ya CCM, CUF, Chadema, ruksa mie siruhusiwi kujadili mambo ya Chadema.
Jadili ya wezi wenzako CCM na mikakati yenu ya kifedhuri ya kuwakandamiza watanzania kwa masilahi yenu!
 
Back
Top Bottom