- Hebu na wewe tuambie kwa nini mnamdaka Kafulila juu kwa juu wakati hii ishu ilikuwa inachunguzwa na PCCB na CAG ambazo ni taasisi za serikali? Ripoti za hawa jamaa ziko wapi (japo ni serikali hii hii na viongozi wake ndiyo wanaotuhumiwa kwa ufisadi huu) maana ingalau kwa ripoti ya Hosea na Utouh na timu zao (hata kama imechakachuliwa) tunaweza kupata pa kuanzia ili kujua mbivu na mbichi na kisha kumhukumu Kafulila? Au bado wanaendelea na uchunguzi? If so, mbona mnakuja kwa kasi hivi kuutetea huu ufisadi katika mitandao ya kijamii? Kuna nini hapa?..............Tumesikia hawa jamaa wameshatoa ripoti zao na kuna ushahidi wa kutosha kuwa kuna baadhi ya vigogo waaandamizi wa serikali hii ya JK (mawaziri) wamehusika katika deal hili la kifisadi, je ni kweli? Na Je, ni kweli pia eti Cabinet (Baraza la Mawaziri) wanakaa several times Ikulu kujadili hili ili kuona namna watakavyozuia na kuiokoa serikali hii isije ikaanguka kwa mara nyingine tena kutokana na scandal hii?
- Unazikumbuka scandals za EPA na Richmond namna zilivyoanza huku dhihaka kama hizi zinavyoendelea leo kwa walioziibua? Unaukumbuka mwisho wa scandal hizo? Kama umesahau, basi tukupe hiyo kumbukumbu japo ni mbaya kwenu CCM lakini ndiyo hali halisi na ndiyo nature ya serikali ya CCM ya wizi na ufisadi wa mali ya umma!!.......Mara zote walionekana kama anavyoonekana Kafulila leo, walishinda na ukweli ulidhihiri na mwisho wa siku serikali iliangukia pua!!
FionaMushi, kwa level hii ya propaganda mnayoifanyia serikali hii eti tu katika kujaribu kuikoa, bado hamjaweza kufikia kiwango cha kuwa fool watanzania hata waweze kunyamaza ktk hili.
Na nikuambie kitu ndugu yangu? Hakuna wakati mwingine mbaya kama huu ambapo serikali hii ya CCM imekabwa koo kila kona hata iweze kujinasua kwani ikigeuka huku inakutana na sokomoko la Katiba mpya, ikigeukia kule inakutana na kashfa ya ESCROW/IPTL Account vs TANESCO na zingine kibao zitakuja, wewe subiri tu tunapoelekea katika General Election ya 2015. Utabiri wa ujenzi wa mnara wa babel na kusambaratika kwa utawala huu ndiyoooooo huo kwa kasi sana unatimia sasa maana mtaongea kwa lugha ambayo hakuna atakayemwelewa mwenzake na mnara utaporomoka puuuuuh!!
Na haya yatawavuruga na kuwasambaratisha kuanzia ndani ya chama chenu hadi kuivuruga na kuisambaratisha Serikali yote. Wewe chunguza tu utalibaini hili mara moja kwani kuna kauli na matendo ya ajabuajabu sana yanafanywa na vongozi wa serikali hii hata inafikia watu wenye akili timamu wanashindwa kuelewa na kuamini iwapo hili limesemwa au limeagizwa na kiongozi wa serikali kweli au mlevi fulani ktk bar!!??
Washauri wakubwa zako, ripoti za uchunguzi wa sakata hili ziwekwe wazi ili public ijue kwani tutaelewa na kutambua mara moja kuwa,
aaah, kumbe ni kweli fedha hizo hazikuwa za umma bali zilikuwa za akina Tibaijuka,(Rwegamurula?) au Sethi Singasinga na IPTL yao............Otherwise,hakuna propaganda itakayobadilisha ukweli huu ya kuwa fedha ni zetu na tumeibiwa tu na Kafulila na wengine wote walio kinyume na hili watasimama kama heroes!!