Secret Star
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,720
- 1,639
Nimeshashikia mara nyingi kutoka kwa watu mbalimbali kuwa Wazungu wametutengenezea virusi vya Ukimwi ili vituue tupungue, sababu tumekuwa wengi mno, Swali hapa linalonipa utata ni hili, Je kama hiyo hoja ni ya msingi iweje imekuwa kinyume,! Watu wanaongezeka badala ya kupungua!! Tunajua kwamba kipindi virusi vya HIV kipindi vilipotangazwa Tanzania tulikuwa Mil 18, na sasa hivi tumeshakuwa Mil 50 mbali na vifo na magonjwa yote na HIV ikihusishwa, hii ina maana kuwa watu wanafanya ngono zembe sana zaidi ya ifikiliwavyo sana!! Swali je Ni kweli Ukimwi umewekwa utupunguze!!?
Swali la pili Kwanini asilimia kubwa ya familia, yaani mke na mme waliopimwa HIV, imeonekana ni mwanandoa mmoja tu ndiye mwenye maambukizi, na inawezekana kuwa asilimia ndogo sana ya familia ndiyo wameonekana wote ni waathirika?
Swali la tatu, kwanini Watumiaji wengi wa ARV's hawafi kwa Maralia, au Homa, Wengi wanaugua magonjwa kama Saratani mbali mbali kwa wanaume na wanawake, BP, kisukari, na mengineyo,
Kipi kinachoendelea ina maana gonjwa hili ni la miujiza!!?