Maswali 7 ya Jaji Joseph Sinde Warioba


Mm nimekuelewa ukwel cna hata mda wa kusikiliza mbili Wala tatu moja ndo mpango cuzz zote mbili na tatu ukitizama kiundan zina matatizo au zitaleta matatizo baadae
 

haya ni mawe..
 
Muheshimiwa Kinana, Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi; tusaidie kujibu maswali haya kwa niaba ya chama cha mapinduzi.

Q1. Kwa nini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?

Q2. Wapeni majibu wananchi kwa nini Tanganyika imevaa koti la Muungano?

Q3. Elezeni kwa nini Katiba imevunjwa, madaraka ya Rais kuchukuliwa na marais wawili katika nchi moja?

Q4. Tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi na kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?

Q5. Kwa nini mnamtuhumu Jaji Warioba na Joseph Butiku kuwa walikuwa wajumbe wa Tume za Kisanga na Nyalali zilizopendekeza serikali tatu?

Q6. Kwa nini hamtaki kuzungumzia yaliyomo katika rasimu bali wanadai imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba?

Q7. Waelezeni wananchi kwa nini mnadai Tume imeingiza maoni yake, wakati iliyakusanya kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?


Chanzo;
Mwananchi
 

majibu mengi ya haya maswali swali yanapatikana katika haya mahojiano yaliyofanyika May mwanzoni. Bofya link hapo chini

"Mahojiano na Wasira - Tuambie TBC1" on YouTube - Mahojiano na Wasira - Tuambie TBC1: Mahojiano na Wasira - Tuambie TBC1 - YouTube
 

Source ya taarifa inatia shaka kwa sababu gazeti la mwananchi linakuwa na asili ya uichochezi.
Pili-Jaji Warioba alishafanyakazi yake na ilishafikia tamati yake .Sheria haisemi kuwa bunge la katiba ni lazima lipitishe rasimu ya tume ya katiba.BUNGE LINAWEZA AMA KUKATAA RASIMU KUHUSU MUUNDO WA MUNGANO AU KUKUBALIANA NA MAPENDEKEZO YA TUME NA KUIFANYA NCHI KUWANA SERIKALI TATU KWA UAMUZI WO WOTE UTAKUWA SAWA.
Kinachoonekana machoni pa watu ni kwamba Jaji anataka kuwaaminisha Watanzania kwamba Ameandika BIBLIA MPYA AU KORANI MPYA ambavyo havitakiwi kupingwa au kujadiliwa.Lazima tujadili ama sekali mbili au tatu huo ni uhuru ambao Jaji hawezi kutunyang'anya.
Kwangu naona hili ndilo kosa kubwa la Jaji kutaka kujibizana na BUNGE LA KATIBA kwa kutaka kipitishwe kile tu alichoandika yeye kwenye rasmu.
.Akae kimya asasi zingine nazo zifanye kazi.SIO KOSA NA SI DHAMBI KUIKATAA RASMU JUU YA MUUNDO WA SERIKALI.
Historia itakuja kumhukumu,awapo alifanya vema au aliboronga.
 
Muheshimiwa Kinana, Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi; tusaidie kujibu maswali haya kwa niaba ya chama cha mapinduzi.

Q1. Kwa nini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?

Q2. Wapeni majibu wananchi kwa nini Tanganyika imevaa koti la Muungano?

Q3. Elezeni kwa nini Katiba imevunjwa, madaraka ya Rais kuchukuliwa na marais wawili katika nchi moja?

Q4. Tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi na kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?

Q5. Kwa nini mnamtuhumu Jaji Warioba na Joseph Butiku kuwa walikuwa wajumbe wa Tume za Kisanga na Nyalali zilizopendekeza serikali tatu?

Q6. Kwa nini hamtaki kuzungumzia yaliyomo katika rasimu bali wanadai imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba?

Q7. Waelezeni wananchi kwa nini mnadai Tume imeingiza maoni yake, wakati iliyakusanya kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…