Maswali 21 kwa Zitto Kabwe

Maswali 21 kwa Zitto Kabwe

Kweli kawashika pabaya cdm,mtaulza hata maswal 100 lakn jamaa anawatesa.

Teh Teh nawasubiri Bavicha wengine waulize ana suruali ngapi na shati ngapi maana Bavicha ni futuhi
 
Umeuliza maswali yako Kishabiki kwa lengo la kuchafua haiba ya Zitto,yafuatayo ni majawabu ya maswali yako


Swali la kwanza kuhusu usaliti.
Dhana ya usaliti ni kufanya kinyume na makubaliano.

Katika chama alichokuwepo Zitto walikubaliana kutopokea posho lkn ni Zitto pekee alietekeleza kwa vitendo,waliobaki hawakuacha kuchukua...hivyo ili Zitto asipate hadhi inayoendana na maamuzi yake ,wenzake wakamwita Msaliti na kutumia Fedha nyingi kuwaaminisha kuwa ni Msaliti,pamoja na hilo Maamuzi ya Zitto kugombea Uenyeliti bila ridhaa ya Mzee Mtei ni usaliti kwa Familia ya Mtei,hivyo hizo porojo za usaliti hata Mbowe kashindwa kuzithibitisha bali ni mwendelezo wa siasa za maji taka.

Ukitala kumuua Mbwa,unampa jina baya ili kuhalalisha mauaji yake hivyo kuwepo na watu wanaosema kuwa Zitto ni Msaliti hakuhalalishi hayo bali sisi tunampima kwa umahiri wake katika Kazi za Kibunge.

2.Swali la Pili kuwa kwanini Zitto anapendwa na kushabikiwa na wana ccm?

Ukweli ni kuwa Zitto ni mwanasiasa aina ya Mutharika wa Malawi.

Kutokana na umahiri katika ujenzi wa hoja amefanikiwa kupenya ngome zote. Mfano ni pale alipotaka kumg'oa Waziri mkuu,miongono mwa waliomuunga mkono ni pamoja na Nimrod Mkono alisaini kumg'oa waziri mkuu na hatimae mawaziri nane wakafukuzwa kazi.

Pamoja na hayo,Mzee warioba alishatuambia kuwa kuna ccm asili na ccm Maslahi.
Hivyo wapo wana ccm wanaoyajua maovu ya ccm lkn wanakosa ujasiri wa kupinga hadharani ,hivyo wanaamua kuvujisha siri kwa mtu ambae ataweza kuzisimamia bila woga.

Wanapoangalia mtu anaekubalika kwa wengi ni Zitto Kabwe.

Hivyo wanaendelea kumuunga mkono kutokana na kuheshimu mchango wake kwa taifa(Siasa sio vita kama unavyotaka kuuaminisha umma)

Pia tambua wabunge kama vile Msigwa,Wenje,Kiwia na Mdee waliungwa mkono na wana ccm ambao wagombea wao walichakachuliwa,Mbona hukuuliza kwanini wana ccm wamewapigia kura wana chadema?

Zitto anashangiliwa na kuungwa mkono na wote,yaani baadhi ya wana ccm na wanamabadiliko mimi nikiwa mmoja wa wana mabadiliko wanao muunga mkono.

3.Kuhusu kuungwa Mkono na vyombo vya habari kama Uhuru,Clouds,,na Mitandao kama Jamiiforums.

Kwanza ni kweli kuwa hivyi vyombo huwa vinaripoti taarifa ya Zitto,kama vimavyoripoti vyombo vingine vya habari.

Watu wa vyombo vya habari wanapenda sana watu ambao wakiandika habari zao watauza magazeti au kusikilizwa.

Habari za Zitto zinauza kuliko habari za mwanasiasa yeyote Tanzania.

Si vyombo hivyo tu ulivyovitaja bali hata ITV ndio walioruka hewani siku ya uzinduzi wa chama,Pia mara kadhaa magazeti ya Tanzania Daima na Mawio nao wamekuwa wakiropoti taarifa za Zitto.

Hivyo hilo si swali la Zitto eti kwanini anaandikwa na kutangazwa,Zitto hana uwezo wa kuwazuia wasiandike habari zake,atakuwa ameingilia uhuru wa habari ambao amekuwa akiupigania katika utumishi wake wa Kibunge.

4.Kwanini Zitto hakujituma sana akiwa chadema kuliko anavyofanya sasa.

Kwanza si kweli kuwa Zitto hakujituma akiwa chadema,Ni jitihada ambazo Zitto alizifanya Zilizowasaidia Chadema kuongeza majimbo.

Wabunge vijana wote wa chadema ni Matunda ya Kazi nzuri ya Zitto.

Kama Zitto angefanya vibaya kwenye Bunge la 2005-2010 angetuharibia vijana kuaminiwa na wananchi.

Pia Oparatio sangara iliyokiimarisha chama ilifanyika huku Zitto akiwa Mstari wa Mbele katika mapambano.

Hata mwaka Juzi kabla ya Mgogoro Zitto alifanya Ziara ya Chama mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara)

Akaendelea na Ziara Mikoa ya Katavi,Tabora ambako aliutaja hadharani Mshahara wa Rais na Waziri Mkuu.

Zitto hakushiriki Oparation ya M4C kutokana na imani yake kuwa hakukuwa na haja ya kuanzisha oparation nyingine wakati hata Oparation Sangara ilikuwa haijaelewaeka vizuri kwa Umma.

Vivyo kiu yake ilikuwa kuona Oparation Sangara Inawafikia watanzamia wote kabla ya kurukia Oparation Nyingine.

Lkn cha kuudhi zaidi Wenye chama waliamua kulazimisha Oparation M4C Kwa lengo la kumsaidia Lema ulaji ambae kipindi kile Ubunge wake ulikuwa umesitishwa na Mahakama.

Baada ta Lema kushinda rufaa yake,Oparation nayo ilikufa na ikaibuka oparation Nyingine Oparation Chadema ni Msingi,ambayo nayo hatujui ilikoishia.

5.Kuhusu ACT-Wazalendo kutopewa ruzuku lkn wanafedha nyingi kufanikisha Uzinduzi na sasa Oparation Sambaza Uzalendo.

Ni kweli Chama hakina ruzuku ,lkn chama kina wanachama na Mashabiki.

Watu tunatoa michango kila siku kukichangia Chama,tunayo Orodha ya wabunge zaidi ya 50 watakao jiunga na chama ambao nao wanatuchangia ili kukiimarisha zaidi ili watakapohamia, wahamie chama imara.

Tunapata Misaada toka vyama rafiki ,vyama hivi awali vilitoa fedha Chadema lkn baada ya kugundua kuwa hazifanyi kazi kama walivyolenga ,wameamua kukata Misaada chadema na sasa Chama kinaendeshwa kwa ruzuku na Michango ya wabunge.

Wame channel Misaada kuja ACT-Wazalendo kutokana na imani kubwa waliyonayo kwa Zitto ambae ndie akiwaunganisha na Chadema.

Wafanya biashara na wajasiliamali wanakichangia chama kama sehemu ya kuwa wanamabadiliko.

Pia Kupitia Ring back tone wana ACT tuliounganishwa kwenye mitandao ya simu tunakichangia chama chetu.

6.Kuhusu Kutoisema vibaya serikali ya ccm.

Kwanza kabisa ACT-Wazalendo haiamini katika siasa nyepesi za kushambulia haiba za watu na chama,badala yake tumejikita kufanya siasa za Maswala (Agenda )ili kutafuta suluhisho la umaskini na matatizo ya wananchi.

Zitto akiwa Morogoro aliibua tuhuma kubwa kuwahi kutokea serikalini kuhusu Watuhumiwa wa Esrow kupewa tenda Kinyemela ya tajriban Bil 54,Gazeti lako pendwa la Tanzania Daima la Juzi tarehe 14-04-2015 limeandika huku likiipa kicha cha habari"Zitto atunishiana misuli na Rugemarila"

Hivyo si kweli kuwa serikali haisemwi pale inapokosea,

7.Kihusu watu wengi kuongea hakafu akasikika yeye tu,ni kutokana na Rekodi aliyojijengea,Pia tambua kuwa vyombo vya habari vya Tanzania vinaangalia soko,hivyo hii challenge kwa vyombo vyetu kuacha bias....maana hata Mawio au Tanzania Daima wanaandika watu wanne tu Chadema,Yaani Mbowe,Slaa,Mnyika na Lissu,ni madra sana kuikuta habari ya Prof Kahigi au Machemli japo ni wabunge wa Chadema

8.Kuhusu Mauzo ya kadi kuwa hafifu na kupita bila kambi.

Kwanza nikujulishe kuwa watu wanaojiunga na ACT-Wazalendo ni wengi kuliko unavyojifikiri.
Wapo wanaoomba kadi kwa njia ya Mitandao,wapo wanaochukua pale kwenye mikutano na wapo wanaofuata Ofisini.

Baada ya ziara kumalizika Chama kitafanya tathmini na kuutangazia Umma idadi ya kadi Zilizouzwa kwa Kipindi cha ziara ya viongozi wa kitaifa.

Kuhusu kupita bila Kambi,ni kuwa ACT-Wazalendo kimeshafanya uchaguzi wa viongozi hivi karibuni kuanzia ngazi ya Tawi ,Kata,Jimbo,Mkoa na Taifa,hivyo usilazimishe kila kazi ya Chama kufanywa na viongozi wa Kitaifa,sisi tunaamini katika kugawana Majukumu na kuaminiana katika kazi,hivyo Ni viongozi wa Mkoa husika watahaoendelea kutimiza wajibu wao kitatua kero za wanachama pamoja na kukieneza Chama.

9.Kwani Afande Sele anaitukana Chadema lkn Zitto hatukani.

Kila mtu anakikomo chake cha uvumilivu.

Zitto amekomaa katika siasa hivyo si rahisi kutukana.

Kuhusu viongozi wengine ,hakuna mkutano wowote ambao chadema imetukanwa ,kama ilitajwa wakati wa kufafanua jambo ka kweli umapaswa kuwa mvumilivu maana Vitu vya ukweli haviitwi matusi,tutaendelea kufanya siasa safi na si siasa za maji taka.

10.Zitto sio Mtei ama Mbowe ambae anadiriki hata kuwachagulia marafiki watu wazima wenye familia Zao,Kila Mbunge anamaono yake kuhusu maisha,hivyo mipaka ya Zitto ni kusimamia katiba ya ACT-Wazalendo ,hivyo swala la Mafao ya wabunge si moja kati ya misingi ya kuasisiwa kwa ACT-Wazalendo.

11.Kuhusu wabunge wanaovujisha Nyaraka ndio wanaotajwa kuja ACT kama Leticia Nyerere.

ACT-Wazalendo ni kama timu ya taifa,inaishi kwa kujikita kwenye misingi hivyo swaka la utu,usawa vinatukataza kumbagua mtu yeyote.

Kuhusu kuvujisha Nyaraka ,hayo ni maneno ya kutunga,kwani Leticia anawadhifa gani kwenye chama kiasia cha kushikilia Nyaraka Muhimu za Chama.

Kila asiekubali kushikiwa akili hubambikwa usaliti na kuvujisha Nyaraka ili kuhalalisha ubaguzi.

Pamoja na hayo ACT-Wazazendo haikutaja majina ya wabunge watakaojiunga na ACT hivyo subiri muda ufike
12.Kuhusu Mchange na Mtemelwa.

Kwanza usipotoshe Umma kuwa Msafiri Mtemelwa alifukuzwa Chadema,aliondoka kwa hiari baada ya Slaa kuandikiwa barua kustaafu rasmi kuitumikia Chadema

Kuhusu Mchange na Mtemelwa,ni vema ukajiandaa vema kisaikolojia kuwa si wana chadema tena,kwa sasa wanajenga Chama kipya na hutawasikia tena wakijiita Chadema.

Swala ka kuhama chama ni swala la utashi wa mtu na sheria za nchi zinaruhusu,wao si wakwanza kuhama na kuwa wajumbe wa kamati kuu,Slaa alikuwa ccm kwa umri wa ujana wake,akahama na sasa ni Katibu wa kamati kuu.

Lema alikuwa TLP akahamia Chadema na sasa ni mjumbe wa kamati kuu

Lissu alikuwa NCCR akahamia chadema na sasa ni mjumbe wa kamati kuu

Benson Kigaila alikuwa UDP akahamia Chadema na sasa ni mjumbe wa kamati kuu.

Hivyo walichokifanya Mchange na Mtemelwa hakitofautiani na kilichofanywa na Slaa,Lema,Lissu na Kigaila.

13.Kwanini Zitto anajiita Mjamaa wakati ana mali.

Kwanza Ujamaa sio umaskini bali ujamaa ni mfumo wa uzalishaji ambao hupunguza pengo kati ya wenye nacho na wasionacho.

Ujamaa unaozungumziwa na ACT-Wazalendo ni ule ujamaa wa Kidemokrasia.

Hivyo unatambua juhudi za mtu binafsi na jitihada za mtu kumiliki mali.

Hoja ya ujamaa tunayoipigania ni rasilimali za wote Zinufaishe wote,kupata fursa sawa katika matumizi ya rasilimali hizo.

Tunaposema furasa sawa hatumannashi kulingana fedha au Nyumba za kuishi.

Bali tuna maanisha kuwa Kama ni Elimu basi Mtoto wa Kabwela na Mtoto wa tajiri wasome shule mojs ili kama mtu anashindwa ashindwe mwenyewe na si kushindwa kwa sababu ya miundombinu duni na uhaba wa walimu.

Kama ni huduma za Afya basi hispital za umma ziboreshwe ili Maskini na tajiri wote waweze kutibiwa kwa gharama zinazolipika na si mmoja kumuacha na Hospital yenye paracetamol na mwingine anatibiwa hospital binafsi kwa bei ghali.

Hivyo Zitto au mtu yeyoye kumiliki mali ya halali hakupingani na sera ya Ujamaa wa Kidemokrasia.

14.Ramadhani Dau ni mtu mwenye uziefu na mtu mchapa kazi ambae kila mtu anatamani kujifunza kutoka kwake.

Ramadhani Dau ni kama Mzee wa Zitto hivyo Zitto anajifunza mengi kutoka kwake.

15.kuhusu mahusiano ya Zitto na Dau.

Mnapofanya kazi ya ujenzi wa taifa ni lazima mfanye kazi kwa pamoja(team work)ilimradi nyote muwe na dhamira safi.

Dau ni Moja ya wakurugenzi wenye mafanikio miongoni mwa wakurugenzi wa mifuko ya hifadhi ya jamii

Hivyo hakuna sababu ya kuamini katika uadui badala ya ushirikiano.

16.Kuhusu kushindana na John Cheyo kugombea uenyekiti wa PAC.

Asiekubali kushinda si mshindani,kati ya Cheyo na Zitto Mmoja ilikuwa ni lazima ashinde.

Zitto alistahili kuiongoza PAC kutokana na uelewa wake katika maswala ya fedha.

Kamati ya PAC inavitu vigumu ambavyo vinahitaji mtu mwenye uelewa wa kiwango cha juu.

Matunda ya Zitto kuchaguliwa tuliyaona kwenye Sakata la Escrow ambapo hata wabunge wengi walionyesha kupwaya kwa kushindwa kuekewa hata dhana ya Capacity charge.

Ili bidi Zitto ageuke Mwalimu wa Bunge Zima ili kuwaondoa uvulivuli wabunge ambao walikuwa wanachangia mambo wasiyoyajua.

Hivyo Kila mtu mwenye mapenzi ya kweli hawezi kujutia Zitto kuiongoza PAC.

kuhusu kuwa alisaidiwa na Kikwete,huu ni mwendelezo wa kufanya Ubunilizi badala ya kujenga hoja.

Ushawishi wa Zitto kwa wabunge ni Mkubwa sana ukilinganisha na Mzee Cheyo.

Wakati PAC inaongozwa na Cheyo na Zitto anaongoza POAC wengi hatukujua kama kuna kamati inaitwa PAC,tulikuwa tunaifahamu POAC lkn baada ya kushikwa na Mzalendo huyu kamati imekuwa machinjio ya viongozi wasiowajibika na wale wanaoliibia taifa.

Hayo ndiyo majawabu kwa maswali yako 16.

ZITTO KABWE HUYU HAPA.naomna amalizie majibu ya maswali yangu.
 
Ama Kweli Watanzania Tuna Kazi Juu Ya Siasa
 
Back
Top Bottom