Maswali 14 ya Padri Privatus Karugendo - Raia Mwema.

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
BUSANDA: Nauliza, naomba kujibiwa!

Padri Privatus Karugendo - Raia Mwema

1. Nauliza: Tumewaona mawaziri wa serikali ya awamu ya nne wakipiga kampeni kule Busanda. Walifanya hivyo kwa vile wao ni wanachama wa CCM au kwa vile wao ni watumishi wa umma? Kama walikwenda kama wanachama wa CCM, je walikuwa kwenye likizo? Tunaweza kuhakikishiwa bila mashaka yoyote kwamba walikuwa kwenye likizo?
Kama walikwenda huko kama watumishi wa umma, je ni hatua gani imechukuliwa dhidi yao? Ni sahihi kwa mtumishi wa umma kutumia muda wa kutoa huduma kwa wananchi ili kufanya kampeni zenye manufaa kwa chama chake?
Je, maadili ya utumishi wa umma yanamruhusu mtumishi wake kuacha majukumu yake kufanya mambo mengine kama vile ya chama chake na familia yake? Leo hii wamefanya kampeni za chama chao, kesho wanaweza kutakiwa kuendesha shughuli za familia, ukoo au kabila lao. Mipaka iko wapi ya mtu wa umma kufanya kazi zake na kufanya kazi za Umma?
Kama mawaziri hawa – John Magufuli (Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo), William Ngeleja (Nishati na Madini), Laurence Masha (Mambo ya Ndani), Sophia Simba (Utawala Bora), walikwenda huko kama watumishi wa umma, je ni fedha za walipakodi zilizotumika kuwalipia usafiri, malazi na posho?
Hili linaweza kuonekana kama swali la kijinga, lakini uwajibikaji unaanzia hapo. Ni ipi mipaka ya mtumishi wa umma, ni lini yuko huru kufanya mambo yake na ni lini anaweza kufanya mambo yake binafsi?
2. Nauliza: Busanda walijiandikisha wapiga kura zaidi ya 100,000 lakini waliopiga kura ni 55,000 hawa wengine zaidi ya 50,000 wamepotelea wapi? Kwa nini hawakupiga kura? Hii ni idadi kubwa sana. Haiwezaekani kwamba hawakupiga kura kwa sababu ya ugonjwa- vinginevyo tungetangaziwa kwenye radio ugonjwa huo ulioikumba Busanda.
Hatukusikia kwamba hali ya hewa ilikuwa mbaya kule Busanda kiasi cha kuwazuia watu kupiga kura. Hili ni swali la uchokozi, lakini ni la muhimu sana. Kila mtu makini ni lazima ajiulize swali hili. Ilitokea Kiteto, zaidi ya nusu ya wapiga kura hawakujitokeza. Hadi kesho hakuna maelezo. Ilitokea Mbeya Vijijini, nusu ya wapiga kura hawakujitokeza. Kuna nini? Ni lazima tupate maelezo.
3. Nauliza: Mtu anayepinga ufisadi, kama tunavyosikia kwenye vyombo vya habari, anaweza vipi kushiriki zoezi chafu na la kishenzi kama kununua shahada za wapiga kura? Kuna watu wanaoheshimika kwa kupambana na ufisadi, hata bila ya kuwataja majina tunawafahamu na wengine walikuwa Busanda wakipiga kampeni.
Tunaposikia habari kwamba baadhi ya kada wa CCM walikamatwa wakiendesha zoezi la kununua shahada, mashujaa wetu wa kupambana na ufisadi walikuwa wapi? Kama walishindwa kukemea tabia hii na kuiruhusu iendelea kiasi cha zaidi ya watu 50,000 kushindwa kupiga kura, basi nao ni mafisadi! Kununua shahada ya mtu ili kumzuia kutumia uhuru wake kumchagua mwakilishi anayemtaka ni ufisadi wa kishenzi.
4. Nauliza: Wale kada wa CCM waliokamatwa wakinunua shahada za wapiga kura kule Busanda wamechukuliwa hatua gani? Tulisikia kwenye vyombo vya habari kwamba walitumwa na viongozi wa juu wa CCM – kama ni kweli, je viongozi hawa wamechukuliwa hatua gani? Ni lazima tuambiwe!
5. Nauliza: Je, ilikuwa ni lazima kulikomboa jimbo la Busanda kwa gharama zozote? Ilikuwa ni lazima kutumia fedha zote hizo zilizotumika Busanda? Je kama jimbo hili lingeangukia kwenye mikono ya CHADEMA, CUF AU UDP, lingekuwa limekwenda kwenye mikono ya Waganda, Wakenya, Wanyarwanda au Warundi? Je vyama hivi si vya Watanzania?
Kama lengo letu ni moja la kuijenga Tanzania kwa Watanzania, kwa nini pajitokeza watu wenye wasiwasi kwamba uongozi wa nchi hii ni lazima uwe mikononi mwa chama kimoja?
6. Nauliza: Fedha za kumwaga kule Busanda zilitoka wapi? Kwa nini ionekane Serikali haina fedha, lakini chama kina fedha? Kwa nini fedha hizi zisitumike kujenga barabara, shule, hospitali na kusambaza umeme na maji vijijini kuanxzia Busanda yenyewe?
7. Nauliza: Kwa nini kule Busanda wananchi wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kuwapatia umeme kwa kipindi chote cha Uhuru wetu kinachoelekea miaka 48, wamelalamikia maji, barabara na huduma nyingine muhimu. Badala yake wamepata t-shirts, kofia na fedha za kununua shahada.?
8. Nauliza: Kwa nini Chama tawala cha CCM kimeamua kutumia mfumo huu wa kununua shahada za wapiga kura, mfumo unaojenga utamaduni wa "kishenzi", utamaduni unaowanyanyasa wanyonge na kuwafungia haki yao ya kupiga kura; utamaduni wa kununua ushindi; utamaduni wa kuwaruhusu wenye fedha kuendesha nchi wanavyotaka?
9. Nauliza: Muhimu ni chama cha siasa au ni Taifa? Tushughulikie nini, kuendeleza vyama vya kisiasa au kuliendeleza Taifa letu la Tanzania? Wenye mawazo yanayofanana, mfano kwa suala la ufisadi, kwa nini wasiungane na kuwa na sauti moja hata kama wanatoka vyama tofauti?
Tunashuhudia kwamba baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani wana mawazo yanayofanana juu ya ufisadi. Lakini saa ikiwadia, vyama vinakuwa na nguvu zaidi ya utaifa.
10. Nauliza: Ni nani anatupumbaza na kutuaminisha kwamba Tanzania ni nchi masikini? Wimbo uliozoeleka kwenye masikio ya kila Mtanzania ni kwamba Serikali yetu haina fedha: Shule hazijengwi kwa vile serikali haina fedha, mahospitali hayajengwi kwa vile serikali yetu haina fedha, dawa hazipatikani kwa sababu serikali haina fedha, barabara hazitengenezwi kwa vile serikali yetu haina fedha, watu kule vijijini hawana huduma ya umeme kwa vile serikali haina fedha, hakuna huduma ya maji kwa vile serikali haina fedha!
Kila ikisomwa bajeti, maelezo yanayofuata ni kwamba Serikali haina fedha hivyo haiwezi kutekeleza kila lengo na tegemeo la wananchi. Kwa ufupi ni kwamba serikali yetu haina fedha, ni serikali masikini inayotegemea misaada kutoka nchi za nje. Ni kweli Tanzania ni masikini? Naomba jibu!
11. Nauliza: Je si kweli kwamba wimbo huu wa serikali haina fedha umetufikisha mahali pa baadhi ya watumishi wa serikali (kama walimu) kutolipwa mishahara na mafao yao, wastaafu kutolipwa kwa wakati, serikali kushidwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, serikali kukwepa wajibu wake wa kutoa huduma kwa wananchi kwa kisingizio cha ubinafsishaji na ushirikishwaji wa wadau katika maendeleo.
Serikali imeaanza kukimbia wajibu wake wa kutoa elimu kwa umma, wajibu wake wa kutoa matibabu kwa umma, wajibu wake wa kutoa na kusimamia usafiri wa umma, wajibu wake wa kusimamia na kuendeleza kilimo, wajibu wake wa kuanzisha na kuvisimamia viwanda, wajibu wake wa kutoa elimu ya uraia na kulinda haki za wanaonyanyaswa kama vile watoto, wanawake, walemavu na wasiojiweza kama vile yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
12. Nauliza: Swali langu ni juu ya ukweli huu kwamba serikali yetu haina fedha. Hivi ni kweli au ni matatizo yaliyo kwenye vichwa vyetu? Iwe vipi nchi tajiri kama Tanzania; ardhi kubwa ya kilimo na ufugaji, maziwa, mito na bahari yenye wingi wa samaki, misitu yenye mbao na wanyama wa kila aina na madini mengi, iwe masikini?
Umasikini huu unatoka wapi? Nani anayaweka mawazo haya ndani ya vichwa vyetu? Nani huyu anayetaka kutuaminisha kwamba sisi ni masikini, hatujiwezi, ili afanye mbinu za kutuibia kila kitu?
13. Nauliza: Inakuwa vipi serikali masikini, isiyokuwa na fedha za kuendesha huduma kwa watu wake, iwe na magari ya kifahari, iwe na uwezo wa kuwatibu wakubwa Ulaya, iwe na uwezo wa kununua ndege ya rais, iwe na uwezo wa kuwasafirisha watendaji wake daraja la kwanza kwenye ndege, iwe na uwezo wa kuwatunza watendaji wake kifahari?
Mbona matumizi ya serikali hayaonyeshi umasikini wa aina yoyote ile? Kwa nini tuendelee kuomba kufikia hatua ya kupoteza heshima yetu kama binadamu?
14. Nauliza: Kwanini Serikali haina fedha, lakini Chama tawala kina fedha? Mipango ya Serikali inakwama, huduma kwa wananchi zinakwama, lakini mipango ya chama haikwami na huduma kwa wanachama wa CCM hazikwami?
Ni imani yangu kwamba kila Mtanzania mwenye uchungu na taifa letu ni lazima ajiulize maswali kama ninayojiuliza mimi. Nani anaendesha dola? Serikali au chama?

Naomba moja kati ya wafuatao wampe jibu
Padri Privatus Karugendo ?

1. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi - Judge L. Makame
2. Msajili wa vyama vya siasa - Tendwa
3. Spika wa Bunge - Mh. Samwel Sita.
4. Mkuu wa Polisi - IGP Saidi Mwema.
5. Waziri wa Urawala bora - Sophia Simba.
6. Mkuu wa Takukuru - Hoseah.
7. Waziri Mkuu - Mh. Mizengo Pinda.
8. Raisi wa JMT na Mwenyekiti wa CCM - Mh. Jakaya Kikwete.

Je, kwa hali kama hii kuna haja kweli ya vyama vingine mbali ya CCM kushiriki katika Uchaguzi Mkuu mwakani ? Na kama vitaamua kushiriki, tutegemee nini kama CCM ndiyo inatunga sheria za uchaguzi, inazisimamia na inaamua nani mshindi ? Kaazi kweli kweli....
 
Tanzania ni nchi tajiri kupita kiasi tatizo letu ni hao mapapa na manyangumi wanaotutawala,hao wamejifanya miungu wadogo kuwataabisha walio wengi.
 
1. Kwa nchi kama Tz- do we need Uchaguzi Mdogo after all?????

2. Copy and paste hadi lini? Hatuna mawazo mapya?
 
1. Kwa nchi kama Tz- do we need Uchaguzi Mdogo after all?????

Hasa inapokumbukwa kwamba uchaguzi mkuu utafanyika labda miezi kumi nasita ijayo!

Tunahitaji kutumia hela mingi kumchagua mtu atakaeongoza kipindi hicho kifupi?halafu tutumie hela nyingine nyingi kwa mgombea huyo huyo kwenye uchaguzi mkuu?
 
Nikweli kabisa mkuu!, zile hela zinazotumika zingeweza kuwasaidia wananchi ktk jmbo husika! Kuliko kuzitapanya ovyo wala bila sababu! Sijui tukoje sisi!!?
 
Hasa inapokumbukwa kwamba uchaguzi mkuu utafanyika labda miezi kumi nasita ijayo!

Tunahitaji kutumia hela mingi kumchagua mtu atakaeongoza kipindi hicho kifupi?halafu tutumie hela nyingine nyingi kwa mgombea huyo huyo kwenye uchaguzi mkuu?

Huyu padri naye kadata mbona maswali haya hakuyauliza baada ya uchaguzi mdogo wa Tarime??
 
Hicho ulichosema ndicho cha muhimu kuliko maswali yake?! au upadri wake ndiyo tatizo lako mzee?

upadre wake sio tatizo kwangu tatizo kwangu kwanini hayo maswali hakuyauliza baada ya uchaguzi wa Tarime.? hilo ndilo tatizo.Maana kama ni gharama kwani haoni gharama za CHADEMA na CHOPA??

Na kingine ambacho sikielewi labda unisaidie Hivi wakati wa kampeni huwa hakuna serikali? yani wakati huo huwa hakuna Rais wala mawaziri? maana huwa wamechukuwa likizo na nafasi zao nani huwa anazikaimu wakati huo.?
 
tatizo la kunyweshwa maji ya mtera....wajinga ndiyo waliwao

Mkuu kwa hiyo wewe ni mwelevu ama mjinga?? kama ni mtanzania kutokana na msemo wako basi utakuwa moja wa mjinga maana mafisadi bado wanatukula tena kwa kasi ya ajabu .

sasa wewe fenomenani yako iko iko nje?
 
BUSANDA: Nauliza, naomba kujibiwa!

Padri Privatus Karugendo - Raia Mwema

10. Nauliza: Ni nani anatupumbaza na kutuaminisha kwamba Tanzania ni nchi masikini? Wimbo uliozoeleka kwenye masikio ya kila Mtanzania ni kwamba Serikali yetu haina fedha: Shule hazijengwi kwa vile serikali haina fedha, mahospitali hayajengwi kwa vile serikali yetu haina fedha, dawa hazipatikani kwa sababu serikali haina fedha, barabara hazitengenezwi kwa vile serikali yetu haina fedha, watu kule vijijini hawana huduma ya umeme kwa vile serikali haina fedha, hakuna huduma ya maji kwa vile serikali haina fedha!
Kila ikisomwa bajeti, maelezo yanayofuata ni kwamba Serikali haina fedha hivyo haiwezi kutekeleza kila lengo na tegemeo la wananchi. Kwa ufupi ni kwamba serikali yetu haina fedha, ni serikali masikini inayotegemea misaada kutoka nchi za nje. Ni kweli Tanzania ni masikini? Naomba jibu!

Nchi hii ni tajiri sana,na kunasiku viongozi wa serikali ya CCM wataadhibiwa na mwenyezi mungu kwa kuhakikisha wanatoa mianya ya kuwanufaisha watu wa mataifa mengine raslimali za taifa na kuwafanya wawe matajiri wakati watanzania wamebaki ni maskini wa kutupwa.

kila jambo lina wakati wake wananchi wanchezewa katika kipindi hiku kuna siku kutakuja mapinduzi ya fikra ambampo watanzania wengi watakuja kukataa kata kunyimwa haki zao za msingi ikiwemo ile ya kuwa na kiongozi wanayemtaka,wananchi wengi tunaamini Busanda CCM haikushinda

Ifike sasa hoja ya wapinzani na watanzania kwa ujumla iwe kukataa kabisa kubuluzwa katika chaguzi mbalimbali kwa mfano kama kuna wezi wa haki za msingi za uchaguzi wezi hao wabururwe kwenye mahakama za kimataifa
 
Maswali ya padri ni valid na wahusika wawajibike kuyajibu.
Wasipoyajibu ( tunajua hawawezi) wajue kuwa fukuto la mwamko wa mambo yaliyopelekea padri kuuliza maswali hayo linawaka kwenye nafsi za watanzania wengi. Hakuna kisichokuwa na tamati. Ni uamuzi wetu wenyewe jinsi gani hiyo tamati iwe!!
 
Tatizo la nchi yetu hakuna atakayejibu, siyo serikali na taasisi zake wala chama tawala. Kwa nchi zingine serikali ilipaswa kujibu na kuwaeleza kwa undani wananchi wake nini wamekifanya, wamekwama wapi na wanafanya nini ili kuyakabili. Kwa hapa bongo mhhhh........, jibu ni zidumu fikra za mwenyekiti wa ccm, na jk ni mgombea pekee wa urais 2010,
 
BUSANDA: Nauliza, naomba kujibiwa!

Padri Privatus Karugendo - Raia Mwema

1. Nauliza: Tumewaona mawaziri wa serikali ya awamu ya nne wakipiga kampeni kule Busanda. Walifanya hivyo kwa vile wao ni wanachama wa CCM au kwa vile wao ni watumishi wa umma? Kama walikwenda kama wanachama wa CCM, je walikuwa kwenye likizo? Tunaweza kuhakikishiwa bila mashaka yoyote kwamba walikuwa kwenye likizo?
Kama walikwenda huko kama watumishi wa umma, je ni hatua gani imechukuliwa dhidi yao? Ni sahihi kwa mtumishi wa umma kutumia muda wa kutoa huduma kwa wananchi ili kufanya kampeni zenye manufaa kwa chama chake?
Je, maadili ya utumishi wa umma yanamruhusu mtumishi wake kuacha majukumu yake kufanya mambo mengine kama vile ya chama chake na familia yake? Leo hii wamefanya kampeni za chama chao, kesho wanaweza kutakiwa kuendesha shughuli za familia, ukoo au kabila lao. Mipaka iko wapi ya mtu wa umma kufanya kazi zake na kufanya kazi za Umma?
Kama mawaziri hawa – John Magufuli (Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo), William Ngeleja (Nishati na Madini), Laurence Masha (Mambo ya Ndani), Sophia Simba (Utawala Bora), walikwenda huko kama watumishi wa umma, je ni fedha za walipakodi zilizotumika kuwalipia usafiri, malazi na posho?
Hili linaweza kuonekana kama swali la kijinga, lakini uwajibikaji unaanzia hapo. Ni ipi mipaka ya mtumishi wa umma, ni lini yuko huru kufanya mambo yake na ni lini anaweza kufanya mambo yake binafsi?
2. Nauliza: Busanda walijiandikisha wapiga kura zaidi ya 100,000 lakini waliopiga kura ni 55,000 hawa wengine zaidi ya 50,000 wamepotelea wapi? Kwa nini hawakupiga kura? Hii ni idadi kubwa sana. Haiwezaekani kwamba hawakupiga kura kwa sababu ya ugonjwa- vinginevyo tungetangaziwa kwenye radio ugonjwa huo ulioikumba Busanda.
Hatukusikia kwamba hali ya hewa ilikuwa mbaya kule Busanda kiasi cha kuwazuia watu kupiga kura. Hili ni swali la uchokozi, lakini ni la muhimu sana. Kila mtu makini ni lazima ajiulize swali hili. Ilitokea Kiteto, zaidi ya nusu ya wapiga kura hawakujitokeza. Hadi kesho hakuna maelezo. Ilitokea Mbeya Vijijini, nusu ya wapiga kura hawakujitokeza. Kuna nini? Ni lazima tupate maelezo.
3. Nauliza: Mtu anayepinga ufisadi, kama tunavyosikia kwenye vyombo vya habari, anaweza vipi kushiriki zoezi chafu na la kishenzi kama kununua shahada za wapiga kura? Kuna watu wanaoheshimika kwa kupambana na ufisadi, hata bila ya kuwataja majina tunawafahamu na wengine walikuwa Busanda wakipiga kampeni.
Tunaposikia habari kwamba baadhi ya kada wa CCM walikamatwa wakiendesha zoezi la kununua shahada, mashujaa wetu wa kupambana na ufisadi walikuwa wapi? Kama walishindwa kukemea tabia hii na kuiruhusu iendelea kiasi cha zaidi ya watu 50,000 kushindwa kupiga kura, basi nao ni mafisadi! Kununua shahada ya mtu ili kumzuia kutumia uhuru wake kumchagua mwakilishi anayemtaka ni ufisadi wa kishenzi.
4. Nauliza: Wale kada wa CCM waliokamatwa wakinunua shahada za wapiga kura kule Busanda wamechukuliwa hatua gani? Tulisikia kwenye vyombo vya habari kwamba walitumwa na viongozi wa juu wa CCM – kama ni kweli, je viongozi hawa wamechukuliwa hatua gani? Ni lazima tuambiwe!
5. Nauliza: Je, ilikuwa ni lazima kulikomboa jimbo la Busanda kwa gharama zozote? Ilikuwa ni lazima kutumia fedha zote hizo zilizotumika Busanda? Je kama jimbo hili lingeangukia kwenye mikono ya CHADEMA, CUF AU UDP, lingekuwa limekwenda kwenye mikono ya Waganda, Wakenya, Wanyarwanda au Warundi? Je vyama hivi si vya Watanzania?
Kama lengo letu ni moja la kuijenga Tanzania kwa Watanzania, kwa nini pajitokeza watu wenye wasiwasi kwamba uongozi wa nchi hii ni lazima uwe mikononi mwa chama kimoja?
6. Nauliza: Fedha za kumwaga kule Busanda zilitoka wapi? Kwa nini ionekane Serikali haina fedha, lakini chama kina fedha? Kwa nini fedha hizi zisitumike kujenga barabara, shule, hospitali na kusambaza umeme na maji vijijini kuanxzia Busanda yenyewe?
7. Nauliza: Kwa nini kule Busanda wananchi wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kuwapatia umeme kwa kipindi chote cha Uhuru wetu kinachoelekea miaka 48, wamelalamikia maji, barabara na huduma nyingine muhimu. Badala yake wamepata t-shirts, kofia na fedha za kununua shahada.?
8. Nauliza: Kwa nini Chama tawala cha CCM kimeamua kutumia mfumo huu wa kununua shahada za wapiga kura, mfumo unaojenga utamaduni wa "kishenzi", utamaduni unaowanyanyasa wanyonge na kuwafungia haki yao ya kupiga kura; utamaduni wa kununua ushindi; utamaduni wa kuwaruhusu wenye fedha kuendesha nchi wanavyotaka?
9. Nauliza: Muhimu ni chama cha siasa au ni Taifa? Tushughulikie nini, kuendeleza vyama vya kisiasa au kuliendeleza Taifa letu la Tanzania? Wenye mawazo yanayofanana, mfano kwa suala la ufisadi, kwa nini wasiungane na kuwa na sauti moja hata kama wanatoka vyama tofauti?
Tunashuhudia kwamba baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani wana mawazo yanayofanana juu ya ufisadi. Lakini saa ikiwadia, vyama vinakuwa na nguvu zaidi ya utaifa.
10. Nauliza: Ni nani anatupumbaza na kutuaminisha kwamba Tanzania ni nchi masikini? Wimbo uliozoeleka kwenye masikio ya kila Mtanzania ni kwamba Serikali yetu haina fedha: Shule hazijengwi kwa vile serikali haina fedha, mahospitali hayajengwi kwa vile serikali yetu haina fedha, dawa hazipatikani kwa sababu serikali haina fedha, barabara hazitengenezwi kwa vile serikali yetu haina fedha, watu kule vijijini hawana huduma ya umeme kwa vile serikali haina fedha, hakuna huduma ya maji kwa vile serikali haina fedha!
Kila ikisomwa bajeti, maelezo yanayofuata ni kwamba Serikali haina fedha hivyo haiwezi kutekeleza kila lengo na tegemeo la wananchi. Kwa ufupi ni kwamba serikali yetu haina fedha, ni serikali masikini inayotegemea misaada kutoka nchi za nje. Ni kweli Tanzania ni masikini? Naomba jibu!
11. Nauliza: Je si kweli kwamba wimbo huu wa serikali haina fedha umetufikisha mahali pa baadhi ya watumishi wa serikali (kama walimu) kutolipwa mishahara na mafao yao, wastaafu kutolipwa kwa wakati, serikali kushidwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, serikali kukwepa wajibu wake wa kutoa huduma kwa wananchi kwa kisingizio cha ubinafsishaji na ushirikishwaji wa wadau katika maendeleo.
Serikali imeaanza kukimbia wajibu wake wa kutoa elimu kwa umma, wajibu wake wa kutoa matibabu kwa umma, wajibu wake wa kutoa na kusimamia usafiri wa umma, wajibu wake wa kusimamia na kuendeleza kilimo, wajibu wake wa kuanzisha na kuvisimamia viwanda, wajibu wake wa kutoa elimu ya uraia na kulinda haki za wanaonyanyaswa kama vile watoto, wanawake, walemavu na wasiojiweza kama vile yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
12. Nauliza: Swali langu ni juu ya ukweli huu kwamba serikali yetu haina fedha. Hivi ni kweli au ni matatizo yaliyo kwenye vichwa vyetu? Iwe vipi nchi tajiri kama Tanzania; ardhi kubwa ya kilimo na ufugaji, maziwa, mito na bahari yenye wingi wa samaki, misitu yenye mbao na wanyama wa kila aina na madini mengi, iwe masikini?
Umasikini huu unatoka wapi? Nani anayaweka mawazo haya ndani ya vichwa vyetu? Nani huyu anayetaka kutuaminisha kwamba sisi ni masikini, hatujiwezi, ili afanye mbinu za kutuibia kila kitu?
13. Nauliza: Inakuwa vipi serikali masikini, isiyokuwa na fedha za kuendesha huduma kwa watu wake, iwe na magari ya kifahari, iwe na uwezo wa kuwatibu wakubwa Ulaya, iwe na uwezo wa kununua ndege ya rais, iwe na uwezo wa kuwasafirisha watendaji wake daraja la kwanza kwenye ndege, iwe na uwezo wa kuwatunza watendaji wake kifahari?
Mbona matumizi ya serikali hayaonyeshi umasikini wa aina yoyote ile? Kwa nini tuendelee kuomba kufikia hatua ya kupoteza heshima yetu kama binadamu?
14. Nauliza: Kwanini Serikali haina fedha, lakini Chama tawala kina fedha? Mipango ya Serikali inakwama, huduma kwa wananchi zinakwama, lakini mipango ya chama haikwami na huduma kwa wanachama wa CCM hazikwami?
Ni imani yangu kwamba kila Mtanzania mwenye uchungu na taifa letu ni lazima ajiulize maswali kama ninayojiuliza mimi. Nani anaendesha dola? Serikali au chama?

Naomba moja kati ya wafuatao wampe jibu
Padri Privatus Karugendo ?

1. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi - Judge L. Makame
2. Msajili wa vyama vya siasa - Tendwa
3. Spika wa Bunge - Mh. Samwel Sita.
4. Mkuu wa Polisi - IGP Saidi Mwema.
5. Waziri wa Urawala bora - Sophia Simba.
6. Mkuu wa Takukuru - Hoseah.
7. Waziri Mkuu - Mh. Mizengo Pinda.
8. Raisi wa JMT na Mwenyekiti wa CCM - Mh. Jakaya Kikwete.

Je, kwa hali kama hii kuna haja kweli ya vyama vingine mbali ya CCM kushiriki katika Uchaguzi Mkuu mwakani ? Na kama vitaamua kushiriki, tutegemee nini kama CCM ndiyo inatunga sheria za uchaguzi, inazisimamia na inaamua nani mshindi ? Kaazi kweli kweli....
Anna kilango malecela na mumewe sio WAPINGA UFISADI BALI WASAIDIZI WA KARIBU WA UFISADIIII???

HAO NI VINARA WA UFISADI WA BUSANDAAAA......
 
Back
Top Bottom