WAZO BINAFSI:
Kwa ufupi hili ni suala gumu kulijadili kwa sababu kuna pande mbili zinapingana: Kidini/Maadili, na Haki za binadamu.
Kidini, kama tungelikuwa tunafuata maamrisho ya dini zetu, wala kusingelikuwepo na tatizo hili. Lakini kwa kukiuka dini na maadili, ndio maana utoaji mimba upo na unazidi kila uchao.
Kwa kuwa tumewacha mafundisho na maadili, kwa sabau ya usasa wetu wa "haki za binadamu", tunafuata matakwa yetu kuliko maadili hayo, matokeo yake ni mimba zisizo tarajiwa na watoto wasiotakiwa.
Kwa tulipofika njia ni mbili tu: Ama turudi katika maadili yetu au tukubali ukweli. Ukweli uliopo sasa ni kuwa utoaji mimba upo. Tukiuharamisha mimba zitatolewa, tukiuhalalisha mimba zitatolewa. Madhara ya kuuharamisha ni kutolewa mimba kisirisiri, pengine na watu wasio wataalamu na waganga wa kienyeji. Inasikitisha kuwa baadhi ya wanaotoa mimba hufariki, wanaopona hubakiwa na madhara ya kudumu, kimwili na kisaikolojia.
Pengine ni bora kuuhalalisha huku kukiwa na sheria za kudhibiti hii hali, kwa mfano, mwisho wa umri wa ujauzito kutolewa, na sababu za kutolewa. Pia hii itapunguza machinjio bila ya utaalamu.
Mimi ninabakia na wazo la mchangiaji mmoja: Kinga ni bora kuliko tiba.