Mastercard ya bank ipi ni nzuri au visa card

Mr Kazembe

JF-Expert Member
Mar 24, 2019
374
483
Ningependa kujua naweza kuanzisha mastercard au visa card kwa papo hapo au lazima niwe na account kwanza na je bank ipi ni nzuri kwa mastercard.....

images%20(1).jpg
 
-Kwa bank lazima uwe na account.
-Kwa mobile money lazima uwe na namba ya simu registered na mobile money.
-Equity bank kwa visa card wapo vizuri na NMB master card wapo vizuri ila wazinguzi kinoma kwenye kujiunga unaweza kumaliza mwaka hujaungwa. au Jaribu Exim na wapo fresh sana.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
BancAbc sio lazima uwe na Account ukifika unajaza fomu unapewa kadi papo hapo, sema kuwa makini sana jamaa wana hidden fees kila transaction inapofeli wanaweka -2000 hivyo kwa muda fulani card isipokuwa na hela na kuna website sumbufu sumbufu inayojaribu kufanya transaction unaweza pata deni kubwa sana.

Njia rahisi kwa sasa tunayotumia ni Mastercard ya mpesa ama Airtel money, hizi ni rahisi zaidi.
 
Ningependa kujua naweza kuanzisha mastercard au visa card kwa papo hapo au lazima niwe na account kwanza na je bank ipi ni nzuri kwa mastercard.....

View attachment 1573111
Siyo lazima uwe na kadi hata mpesa na airtel master card ziko poa tu, au Bank ABC pia wanatoa card bila account, ukitaka ya bank bora equity maana hawa crdb na nmb wazinguaji
 
Mkuu hizi master card na visa za taasisi za kifedha za kibongo zina kigugumizi sana kama unakua na mishe nyingi na card hizi na haswa transactions za online nk

Labda ungekuwa specific unataitaka kwa sababu zipi?
Maana kila taasisi ina ubora wake kwenye kipengele fulani fulani
 
Mimi nina Visa card NBC na CRDB ziko vizuri sana,cha muhimu uwe na account kwenye hizo bank baada ya hapo unaserereka tu...
 
E Q U I T Y bank wako vizuri sana sana.... Waaminifu,
Ile umefungua tu account inakuwa tsyari imeunganishwa Online purchasing...
Hauna haja ya kwenda tena kufanya Maombi ya Ku activate Mambo ya Online.
 
BancAbc sio lazima uwe na Account ukifika unajaza fomu unapewa kadi papo hapo, sema kuwa makini sana jamaa wana hidden fees kila transaction inapofeli wanaweka -2000 hivyo kwa muda fulani card isipokuwa na hela na kuna website sumbufu sumbufu inayojaribu kufanya transaction unaweza pata deni kubwa sana.

Njia rahisi kwa sasa tunayotumia ni Mastercard ya mpesa ama Airtel money, hizi ni rahisi zaidi.

Very true , nina Accout na nina Card tuu ya BankABC nadhani ni bank no 1 kwa huduma ya VISA , pia katika huduma bora VISA wanahuduna bora zaidi ya MasterCard. Kuhusu hii charges naona kama siku za karibu haipo sijajua wametoa au laah tuliwalalamikia sana .
 
Stanbic bank ni poa sana,visa card unarudi nayo siku hiyo hiyo,pia makato ni nafuu zaid kuzidi wengine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom