WanaJF
Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.
Umesema kupanga ni kuchagua. Tanzania ina zaidi ya wakaazi milioni 45. Zaidi ya milioni 20 kati ya hao wanaishi mijini, au pembezoni mwa miji na kati ya hao, zaidi ya 90% wanaishi maeneo ambayo hayana mipango miji wala makazi yao hayajapimwa.
Ni aibu kwa nchi yenye viongozi na wasomi kuwa wanaongelea Kigamboni miaka nenda rudi, eneo ambalo halitaishi zaidi ya watu laki tano. Hivi inagharimu bilioni ngapi kutengeza karamani kama hako ulikoweka kwenye picha?
Ramani ya Kigambini ipo, na hata kama haitajengwa leo, tunajua kuwa itajengwa tu, hata miaka 50 ijayo.
Mh Waziri nakuomba kwa heshima na taadhima, angalau kwa muda uliobaki nao kuongoza wizara hiyo, tutengenezee mipango miji ya miji hata 20 tu hapa Tanzania. Najua hii nchi ina zaidi ya 'miji' 100, lakini naomba angalau target miji 20. Hizo ramani ziwepo mahali fulani, ili hata baadae wakija viongozi wengine wakute kuna "kazi" ya kufanya. Hii nchi hadi sasa haina dira, na kila kiongozi akija anafanya anavyojisikia kwa sababu haina master plans.
Kwenye hizi nchi zilizoendelea, si ajabu ukakutana na 'pori', kumbe sio pori, ni mji mkubwa tu 'uliojengwa' miaka 40 iliyopita, ila ujenzi wake bado upo katika stage ya kwenye 'karatasi'. Hapo hata aje kiongozi 'nabii', hawezi kubadilisha; ama anajenga, au anapaacha palivyo.
Ingawa kwa sasa pengine hatuna hela za kujenga, lakini hata za kupanga na kuchora hatuna?!!!