Master plan ya Lowassa ni ipi?

Master plan ya Lowassa ni ipi?

Rasm ya pili ya katiba mpya ambayo Lowasa na chadema wana ahidi kuifufua si tu inafanya mabadiriko Bali pia kufagia uchafu wote ulioletwa na ccm ndani ya nchi hii.haya huyaoni kwa Kuwa akili yako ipo likizo.hapa unatumia akili ya magufuli,ulofa,upumbavu na tumbo lako
Hata uwe na katiba bora kiasi gani kama hakuna busara na weledi na utashi wa kutekeleza yaliyomo itakuwa kazi bure.
Pia katika hali ya kawaida katiba haiwezi ikawa bora na ikasimamia kila kitu kwa matakwa ya kila mtu au kila kikundi. Hivyo katiba iliyopendekezwa na tume ya katiba sio SULUHISHO la matatizo yetu bali ni mwanzo mwingine.
Itakiwa yeyote anayesema atairudisha katiba au rasimu hiyo atueleze ni kitu gani atakachosimamia na kutekeleza.
 
Mabadiliko yepi hayo, yaani uchukue nguo chafu uifue kwenye maji machafu alafu uwaambie watu utapata nguo safi? dawa ya uchafu ni sabuni, Lowasss ni mchafu hawezi kutumikà kama sabuni kuifanya nguo iwe safi zaidi zaidi anaongeza uchafu
 
mkuu master plan ya nchi imeshaandaliwa na watanzania wenyewe kupitia rasim ya pili ya katiba mpya.kazi ya lowasa ni kuirudisha na kuipeleka kwa wananchi waipe mamlaka.basi.

Kazi ya pili ni kuwa empower watanzania ili wajenge nchi yao baada ya serikali kuongozwa na malofa wa akili for 54 years,malofa wanaoamini nchi hii itaendelea kwa kushinda ulaya na marekani kuomba omba
sasa mbona lowassa huyu huyu alikua anapinga rasimu mpya ya katiba, au alipokatwa ccm akaona inafaa?
 
unataka master plan kwani unataka kucopy kitu gani mkuu.
Jiulize tumekuwa na master plan ngapi tangu uhuru. Je tunasonga ama tunatudi?
Usikute hhata hata master yaafamiliamyako yako.
sitaki kukopi chochote nataka nione alafu nipime ndio nijue nitampigia kura nani kwenye urais
 
Lowassa akiwa Morogoro
😃😃😂😂😂👇🏿

"tutaimarisha reli kwa kiwango cha lami"...

☝🏿☝🏿☝🏿😃🙌🏿
 
elimu..elimu..elimu..kilimo..afya..mawasiliano..na kama hauna uccm kwa sasa tanzania tunahitaji vitu kama hivyo..itasaidia vijana kujitambua na kuacha kuongea pumba humu jf ili akapate buku 5 pale lumumba..
ok, elimu, elimu, elimu.. Mbona hajaelezea elimu itaiboreshaje sasa, tuna wahitimu ambao hawawezi kuajiriwa kwenye nchi yao ila wanaletwa wageni kisa wazawa hawaaminiki na elimu yao mr lowassa atalifanyaje hili?
 
rasm ya pili ya katiba mpya ambayo lowasa na chadema wana ahidi kuifufua si tu inafanya mabadiriko bali pia kufagia uchafu wote ulioletwa na ccm ndani ya nchi hii.haya huyaoni kwa kuwa akili yako ipo likizo.hapa unatumia akili ya magufuli,ulofa,upumbavu na tumbo lako
kwanza kabisa haina haja ya kutukana tunajadiliana ili tujue rais bora ni yupi, pili kuhusu katiba mpya lowassa alikua hana mpango kabisa na rasimu ya warioba hadi alipokatwa ccm ndio akaenda ukawa ambayo tayari ilikua na ilani yake
 
lowassa anahaidi uboreshaji na siyo mabadiliko. Nasema uboreshaji kwa kua kila anachoahidi ni kiko kwenye utekelezaji wa ccm au ahadi za ccm na hii mfano suala la elimu anasema elimu bure badala ya kuahidi mfano kutumia lugha mama kiswahili hadi chuo au kiingereza toka darasa la kwanza n.k kwa hiyo underpinnings za elimu zibaki vile vile yeye lowassa mabadikiko yake ni ubure hii tunaita cosmetic make up na siyo mabadiliko.

Kwenye suala la katiba lowassa mwenyewe hajahaidi kama rasimu ya warrioba italetwa kwa wananchi kupigiwa kura ya maoni ndani ya muda let say mwaka au miezi mi3 au siku 100 za kwanza za utawala wake,kuhusu tatizo ufisadi hajaongea kama ataanzisha mahakama au time ya kujadili na kurudisha rasilimali zikizoibiwa katika kipindi fulani chini ya ccm mfano wa buhari kule nigeria ambapo aliahidi kufanya hivyo kama mojawapo ya ahadi za mabadiliko nigeria na kuua ufisadi nchini humo na mpaka sasa nigeria na buhari wanefanikiwa kurudisha kwa umma $50b zikizokwapuliwa na walafi wachache .

Kwa mantiki hii hapa tunaona huyu llwassa asiyeamini mabadiliko ni mtu mbinafsi anayetaka tu kutimiza ndoto binafsi awe rais wa tanzania basi.

Mabadiliko uwa hayawi vuguvugu mabadiliko ni moto mabadiliko siyo kuboresha mabadikiko ni kufutilia mbali yaliyopo sasa, mabadiliko uwa na ahadi zinazopimika ndani ya muda unaopimika na siyo ahadi tu zisizopimika, na muhimu mabadiliko hufanywa na wale ambao hawakua mpaka hivi punde tu hawaamini kwenye hayo mabadiliko na walikua ni sehemu kubwa ya tatizo lenyewe in the first place hadi tukatamani hayo mabadiliko.
nashukuru kwa kujibu bila kejeli au matusi,jf inatakiwa kuwa hivi sio kama genge la wahuni
 
1. Atafuta tozo zote kwa mazao ya wakulima na wafugaji. Hawa ni 90% ya watz wote. Kufuta tozo ni kuongeza kipato kwa mkulima huko ni kuuchukia umasikini.
2. Elimu bure kwa ngazi zote nchini.
Kwa mkakati upi?.
Kupunguza matumuzi ya anasa na kwa kukusanya kodi zote.
shukrani kwa mchango wako
 
unadai umefuatilia ila ulivyoandika inaonyesha kabisa hujafuatilia
imejaribu ila sijaona kama wewe unajua zaidi yangu tuelimishane lengo langu sio ushabiki
 
Lowassa anahaidi uboreshaji na siyo mabadiliko. Nasema uboreshaji kwa kua kila anachoahidi ni kiko kwenye utekelezaji wa CCM au ahadi za CCM na hii Mfano suala la elimu anasema elimu bure badala ya kuahidi Mfano kutumia lugha mama kiswahili hadi chuo au kiingereza toka darasa la kwanza n.k kwa hiyo underpinnings za elimu zibaki vile vile yeye lowassa mabadikiko yake ni ubure hii tunaita cosmetic make up na siyo mabadiliko.

Kwenye suala la Katiba lowassa mwenyewe hajahaidi kama rasimu ya warrioba italetwa kwa wananchi kupigiwa kura ya maoni ndani ya muda let say mwaka au miezi mi3 au Siku 100 za kwanza za utawala wake,kuhusu tatizo ufisadi hajaongea kama ataanzisha mahakama au time ya kujadili na kurudisha rasilimali zikizoibiwa katika kipindi fulani chini ya CCM Mfano wa Buhari kule Nigeria ambapo aliahidi kufanya hivyo kama mojawapo ya ahadi za mabadiliko Nigeria na kuua ufisadi nchini humo na mpaka sasa Nigeria na buhari wanefanikiwa kurudisha kwa umma $50b zikizokwapuliwa na walafi wachache .

Kwa mantiki hii hapa tunaona huyu lLwassa asiyeamini mabadiliko ni mtu mbinafsi anayetaka tu kutimiza ndoto binafsi awe rais wa Tanzania basi.

Mabadiliko uwa hayawi vuguvugu mabadiliko ni moto mabadiliko siyo kuboresha mabadikiko ni kufutilia mbali yaliyopo sasa, mabadiliko uwa na ahadi zinazopimika ndani ya muda unaopimika na siyo ahadi tu zisizopimika, na muhimu mabadiliko hufanywa na wale ambao hawakua mpaka hivi punde tu hawaamini kwenye hayo mabadiliko na walikua ni sehemu kubwa ya tatizo lenyewe in the first place hadi tukatamani hayo mabadiliko.

Ukweli Lowasa anahitaji kutoa ahadi inayoeleweka jinsi ya namna atakavyoshughulikia katiba. Sijamsikia akizungumzia jambo hili ambalo kimsingi ndio roho ya Tanzania yetu.
 
Back
Top Bottom