Master J naye alamba Uteuzi BASATA

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,789
218,420
Hii ni baada ya kuteuliwa na Waziri Damas Ndumbaro kuwa Mjumbe wa Basata.
---
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo , Dkt. Damas Daniel Ndumbaro amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) baada ya Rais wa wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kumteua Prof. Saudin Jacob Mwakaje kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo, uteuzi huo ni kwa mujibu wa Sheria ya Baraza Na. 23 ya mwaka 1984 Sura 204.

Wajumbe walioteuliwa ni Joachim Marunda Kimaryo (Master J), Single Mohamed Mtambalike (Richie Richie), Jessica Julius Mshama, Dkt. Gervas Andrew Kasiga (Chuma), Felista Steven Lelo na Mgunga Attilio Mwamnyenyerwa (Baba Watoto).

Aidha, kufuatia uteuzi huu Waziri Dkt. Ndumbaro ametengua uteuzi wa Wajumbe wa Baraza hilo walioteuliwa hapo awali.

Screenshot_2023-10-03-16-51-04-1.png
 
Hivi vyeo vingine ni uchuro tu.

Sasa mtu unateuliwa kuwa mjumbe wa baraza la sanaa (BASATA!) ili ukafanye nini huko?

Ukazuie nyimbo ya Ney wa mitego inayokosoa watawala?

Ningekuwa mimi ni Master J ningekataa huo uteuzi wa kishirikina na kiftina tu.

Sorry nimesahau, kumbe Master J ni kada wa Chama cha Mambuzi (CCM), hicho cheo kimtamfaa faa kimtindo!
 
Kumbe Master J ni Kada wa Ccm
 
BASATA yenyewe ipo hoi
 
Back
Top Bottom