Masoud Kipanya Uhuru Umezidi Mipaka


Na hilo ndo jukumu la katuni. Kukufanya ufikirie. Sasa kwa akili yako wewe umefikiria hivyo. Kwa nini mnafanya mambo kwa hisia? Yaani you are so insecure! WE ARE ALL ALLOWED TO THINK DIFFERENTLY.
 
Uchaguzi ulishaisha sasa tunachapa kazi ni kipindi cha kusupport ILANI ya CCM hadi 2020
 
Una watoto hapo nyumbani wa darasa la tano wape wafupishe hyo katuni. Ninachotaka ujue ni kwamba hiyo katuni haijakaa vizuri kama ww unavyoenda direct kusema UKM
Sina mtoto wa Primary school,
Oh, pole sana, yawezekana najibishana na walosoma Memkwa!
 
kipanya amezinguaa...
Jinsi swali alivyoweka ndo tatizo... Angeuliza tu "JINA LA MAANDAMANO YA UVCCM" na sio kifupi.
 
Tuweni wakeli kabisa toka mioyoni mwetu, tusi liko wapi hapo? Tusiongozwe na hisia mbaya na za kichochezi kwa maslahi ya kujipendekeza tu. Yeye kauliza swali, na hata kama asingeuliza bado kusingekua na tusi, tuacheni kuchonganisha watu. kama huna cha kuandika kaa kimya
 
Njaga kikwetu ni mtu anaevuta bangi. Huyu Njaga aseme yeye maneno hayo yana maana gani. Mbona sioni tatizo.
 
ujinga sio tusi, mleta mada kuna jambo linakusumbua.wacha tafsili za kijinga.
 
Kufanyaje mbona hatukuelewi mleta uzi ?! Au unamlisha maneno
Yeye mbona aewalisha maneno UVCCM?Ni wapi UVCCM walisema maandamano yao yataitwa kwa neno hilo?wale wengine wanaongea kwa vinywa vyao kwamba neno ni UKUTA.
Mkuu acha kutetea mambo ya hovyo hovyo,wachora katuni mahiri huzingatia kuelimisha na kuburudisha bila kuleta confussion na unnecessary misunderstanding,kwa yeyote mwenye akili timamu hapa jina la mheshimiwa Rais limedhalilishwa na ndio sababu watu wanakosoa,nae kama ni muungwana na mwenye kujitambua ni vyema aombe radhi kwa hilo.
 
Kwani lazima iwe na kifupisho? Yale yale ya M4C ya chadema, CCM wakaibadili maana ya vifupisho.
 
mbona kuna mwana ccm mmoja alimuuliza mwana chadema et na wewe umeshikishwa UKUTA?
 
Umoja. Kumpongeza. Magufuli. Kifupi chake ni ukakasi kukitamka!!. Hasa ukiamua kuchukua herefi mbili za mwanzo kwa kila neno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…