Masopakyindi Travels: -Hapa ni wapi wajameni?

Masopakyindi Travels: -Hapa ni wapi wajameni?

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,897
Reaction score
15,125
View attachment 109201

Katika pita pita zangu huko nji nyingine , nimekuta ingalau barabara safi, hakuna mashimo, tena ni two-way-two-lane.
Nikabaki kujisikikia miye.
Naomba anayeweza kuniambia hapa ni wapi nimpe huo mji.
 
Hiyo mbona kama ni barabara ya "kawawa road" pale junction ya makutano na Mwali kabakwa..
 
picha yenyewe ukiifungua imeandikwa south african trip halafu bado unauliza swali
Kweli mkuu lakini sauzi kubwa na ndio mana nikatoa changamoto.......kama ni chemsha bongo ushapata kengele!!!!
 
Vipi masopyakindi ulipeleka mzigo nini, manake punda sio wasanii tu!!

Aah Mkuu, acha hizo. Sie tutajuaje hapo ni wapi kabisa, maana magari yanatembea. Hata hivyo, uki zoom hiyo picha utaona hizo gari mbili zina namba zifuatazo: CH 43RB GP na TLB 598 GP

Sasa ninavyoelewa mimi Bondeni wana namba za magari za majimbo, na GP kwenye hizo namba inasimamia "Gauteng Province" ambako ndiko mji wa Johannesburg upo. Kwa mantiki hiyo basi lazima hapo ni Johannesburg.

Na pia utaona huo mtaa unaitwa Christian Dube. Hivyo hapo ni Soweto, karibu na Mmesi Park.

Ila Mkuu, kwa kuwa hii picha imepigwa toka ndani ya gari, naona ulitaka tu kutufahamisha kwamba ulikuwa Bondeni au bado uko Bondeni. Unatafuta nini Soweto? Sema tu Mkuu, sie hatuna hiana, ili mradi usiwe kwenye kale ka biashara kanakomsumbua Mwakyembe!
 
Bosi wewe kweli umepatia kwa asilimia mia moja!!!
Nimefika bondeni wiki iliyopita katika safari zangu.
Nilyoyaona huko yalinishangaza kidogo, maana hapo kweli ni SOWETO(South West Township).
Sehemu ambayo mzngu au kaburu hagusi huko au hatakiwi.
Nimeonyesha picha hii kuelezea barabara zilivyo murua ndani ya jiji la Soweto, tofauti na mawazo niliyokuwa nayo nikifikiri sawa na Manzese kwa Mfuga Mbwa!!

Kuna sehemu za Soweto ni bomba sana, ingawaje kuna sehemu kubwa zenye vijumba vilivyo jengwa na makaburu, kwa ajili ya waafrika.
Vile vile nilifika kuhiji nyumbani kwake Kholithatha Madiba, kona ya 8115 Orlando/Vilakazi Street.
Hapo nina picha murua ambayo ni zawadi kwa watani zangu wa jadi CHADEMA, nitaiposti siku zijazo.
 
Hongera sana kwa kwenda Bondeni Vp Masogange hajambo?
Maana wabongo kwa kujifanya mna akili kuliko wenzenu mko juu.
 
Hongera sana kwa kwenda Bondeni Vp Masogange hajambo?
Maana wabongo kwa kujifanya mna akili kuliko wenzenu mko juu.

Mkuu inaelekea wewe ni mmoja wa watanzania waliojizoeza kujifutika futika hivyo kuwa na upeo finyu wa dunia.
Usiwe mwepesi wa kupiga domo tu ukijiwa na wageni, wafuate huko waliko- na uone kwa nini wakija wanabeba kazi zote na rasilmali kwa vile sisi tunazidiwa ufahamu.
Safiri uone.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom