Msaada kilimo cha hoho

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO

Jina la kitalaamu la PILI PILI HOHO ni Capsicum annum. Asili ya zao hili ni bara la Amerika ya Kusini. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Iringa, Tanga (Lushoto), Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha. Kilimo hiki kinaendeshwa na wakulima wadogo katika maeneo yenye ukubwa wa kati ya hekta 0.2-0.4 pia kuna maeneo ya wakulima wakubwa wenye hekta kati ya 2-20. Wakulima hao hujishughulisha na kilimo cha zao hilo kwa njia ya mkataba na kampuni hiyo.

Hoho hutumika katika kutengeneza rangi za asili za vyakula ambazo kwa sasa hupendwa zaidi kuliko zile zinazotokana na kemikali na pia huongeza ladha na harufu katika vyakula. Hivyo hutumika katika viwanda vya kusindika vyakula, kwa mapishi ya nyumbani na hata katika viwanda vya vipodozi kama rangi ya mdomo, uso n.k. Ina virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kama madini ya chuma, vitamin A na C.


hoho.bmp


2.0 TABIA YA MMEA
Hoho ni zao la jamii ya pilipili isiyo kali, tunda lake ni nene kiasi la duara pia linaweza kuwa lililochongoka,.

3.0 ENEO NA HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO
Hoho hustawi vema katika maeneo ya usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 2,000 yenye mvua ya wastani wa mm.600-1,250 na wastani wa joto la nyuzi za sentigredi 21 hadi 24. Udongo wa tifitifu wenye rutuba, usiotuamisha maji na wenye hali ya uchachu (pH) kati ya 5.0-6.5 hufaa zaidi. Umwagiliaji ni muhimu pale mvua inapokuwa chache.

4.0 UZALISHAJI
4.1 UTAYARISHAJI WA KITALU

Chagua eneo katika ardhi isiyo na mtelemko mkali na yenye rutuba ya kutosha. Ardhi iwe imepumzishwa bila kuoteshwa mazao ya jamii ya pilipili, biringanya, nyanya, n.k. ili kuepukana na mashambulizi ya wadudu na magonjwa.
Tayarisha kitalu kabla ya msimu wa mvua. Andaa vizuri matuta manne yenye urefu wa wastani wa mita 10 kila moja na upana wa mita moja (1) ili kustawisha miche inayotosha ekari moja.

Acha njia ya nusu mita kati ya tuta na tuta. Mwagilia maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu na endelea kunyweshea kulingana na hali ya hewa na hali ya udongo. Sia mbegu kwenye, mstari, nafasi kati ya mstari na mstari ni sm 10 na kina cha sm1. Kiasi cha mbegu cha nusu kilo kinatosha eneo la hekta moja. Weka matandazo kwenye kitalu au tumia nailoni nyeusi ili kuhifadhi unyevunyevu na kuzuia uotaji wa magugu.

4.2 UTAYARISHAJI WA SHAMBA
Shamba lilimwe vizuri na kuweka matuta ili kuhifadhi unyevunyevu na kurahisisha umwagiliaji. Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili na matuta madogo hupandwa mstari mmoja.


hoho%2Bnyekundu.bmp


4.3 UPATIKANAJI WA MBEGU
Mbegu ambazo hutumika ni chotara ambazo huuzwa kwenye maduka ya pembejeo za kilimo nchi nzima. Haishauriwi kutumia mbegu kutoka zao la msimu uliopita kwani ubora wa paprika utaharibika na hivyo kuharibu soko unashauriwa kununua mbegu bora.

4.4 UPANDAJI
Mbegu huoteshwa na kukuzwa kitaluni kwa muda wa wiki 6-8 na miche hupandikizwa shambani ikiwa na urefu wa sm.6-10. Mwagilia maji kitaluni kabla ya kuhamisha miche. Panda shambani kwa nafasi ya sm.75-90 kati ya miche kwa sm.90-105 kati ya mistari, wastani wa miche 12,500 itapatikana kwa hekta. Weka samadi shambani tani 25-37 kwa hekta wiki 1-2 kabla ya kupandikiza miche, au kilo 560-670 za NPK (mbolea ya viwandani) kwa hekta kwa uwiano wa 4:7:7 katika udongo usio na rutuba ya kutosha.

ITALIAN PAPRIKA

italian%2Bpaprika.bmp

5.0 KUHUDUMIA SHAMBA
Palizi ifanyike mara magugu yanapotokea shambani. Umwagiliaji maji ufanyike kama ilivyo kwa mazao mengine kama nyanya. Tumia mbolea kiasi cha kilo 140 za SA au CAN kwa hekta hasa wakati mmea inapotoa matunda ili kupata matunda makubwa na kuvuna kwa muda mrefu (hadi miezi 10).

6.0 MAGONJWA NA WADUDU

Wadudu

• Funza wa vitumba
• Vidukari
• Kidomozi (Leaf miner)

Kudhibiti: Tumia dawa aina ya permethrin
Magonjwa
• Kuoza mizizi
• Mnyauko wa majani
• Batobato
Kudhibiti: Choma nyasi kwenye kitalu kabla ya kusia mbegu.
Badilisha mazao yasiyo ya jamii ya pilipili.

7.0 UVUNAJI
Matunda ya kwanza huwa tayari kuvunwa kuanzia miezi 2-3 baada ya kupandikizwa; matunda yaliyokomaa vizuri na kuwa na rangi nyekundu ndiyo huvunwa. Matunda 30-80 hupatikana kwa mmea mmoja.

Ubora wa hoho huongezeka kutegemeana na kiwango cha rangi yake ikiwa ni nyekundu njano au kijani. Mazao kiasi cha tani 3.5 kwa hekta hupatikana. Baada ya kuvuna mwagilia maji, piga dawa (kama ni muhimu) na weka mbolea kuongeza uzalishaji unaofuata.

8.0 USINDIKAJI

Hoho huuzwa ikiwa bado fresh tofauti na jamii nyingine za pilipili ambazo zinaweza kukaushwa na kusindikwa kasha kuuzwa baadae.


hoho%2Bua.bmp

9.0 SOKO LA PAPRIKA
Soko la hoho lipo nchi nzima kwenya masoko makubwa na hata magengeni, hoho hutumiwa zaidi kama kiungo cha kupikia mapishi mbali mbali au kutia kwenye kachumbari. Tatizo kubwa wanalokabiliana nalo wakulima ni kutokuwa na soko la uhakika ndani na nje ya nchi, mazao huweza kuoza shambani au njiani kutokana na tabu ya usafiri hasa vijijini ambapo mvua zikinyesha barabara hazipitiki kwa urahisi

Kuna aina ya pilipili isiyo kali kama hoho lakini ni ndefu kama pilipili za kawaida ijulikanayo kama PAPRIKA ambayo ina soko kubwa nje ya nchi. Zao hili kwa sasa huzalishwa kwa msukumo wa kampuni ya kigeni ya Hispania inayoitwa Tanzania Spices Ltd iliyopo mkoani Iringa


hoho%2Bkijani.bmp

10.0 GHARAMA YA UZALISHAJI WA HEKTA MOJA:
Mbegu Tshs. 24,000 /-
Vibarua 200,000/-
Mbolea(mboji/samadi) 300,000/-
Madawa 100,000/-
Jumla 624,000/-

MAPATO:
Kilo 3,500/- X 800/- 2,800,000/-
 
Habari wana waungwana? Naomba muongozo wa kilimo cha pilipili hoho kwa wenye uzoefu.

Asanteni
 
Wakuu nawasalimu sana, please naomba aliewahi kufanya hiki kilimo anisaidie nijue A-Z yake, mchakato mzima wa kukifanya, risk zake, mauzo/soko, mapato nk. Natanguliza shukrani za dhati.
 
Eagerly waiting for the reply. Utakaetoa somo usisahau kuweka gharama kwa ekari,aina ya udongo znapositawi vizur,mahitaj ya madawa, mambo muhimu ya kuzngatia tokea mche ukiwa kitaluni,mapato kwa ekari iliyotunzwa vizur na mwisho kabsa bei yake sokoni kwa ujazo wa kiasi fulani.
 
Eagerly waiting for the reply. Utakaetoa somo usisahau kuweka gharama kwa ekari, aina ya udongo znapositawi vizur,mahitaj ya madawa,mambo muhimu ya kuzngatia tokea mche ukiwa kitaluni, mapato kwa ekari iliyotunzwa vizur na mwisho kabsa bei yake sokon kwa ujazo wa kiasi fulani.

Asante kwa kufafanua zaidi, naendelea kusubiri majibu.
 
Thanks sana kaka hii kitu swafi sana maelezo nimeyakubali. Embu tupe mchanganuo wa kitunguu na dawa zake kuanzia kupanda mpaka kuvuna .Inaelekea uko vizuri sana kwenye agriculture wengine tumevamia fan mradi ni biashara
 
Ndugu baraka unaweza kushare nasi mahali unapolimia,soko lako unalipatia wap au wanunuzi wakubwa wako wap,kipindi cha mwaka ambapo bei inakuwa nzuri,uzoefu wako na mapato kwa ekari pamoja na ufungaji wa bidhaa kwenda sokoni.
 
Wanaukumbi

Naomba mawazo yenu nipo najiandaa kulima PILIPILI HOHO maeneo ya kigamboni katika OPEN FIELD heka 1 natumia umwagiliaji wa drip

Naomba msaada wa soko la pilipili hoho pamoja na mbegu ambayo inafaa kwa kilimo hiki
 
Hoho zipo aina 3: nyekundu, njano na kijani. Sokoni tumezoea kuona hoho za kijani ila njano na nyekundu zina soko kubwa sana ndani na nje ya nchi. Hoho za kijani hulimwa popote meaning unaweza lima ndani ya greenhouse au nje ya kitalu nyumba.

Ila njano na nyekundu kutokana na rangi zake kuwa exceptional hazipaswi kukutana na jua kali hivyo basi hulimwa mara nyingi ndani ya greenhouse. Ni zao la muda mfupi kwa maana ya tangu unapanda hadi unaanza kuvuna ni miezi minne.

KilimoJoint tunatoa ushauri wa bure kabisa kwenye simu na ukitaka tukutembelee shambani tunaweza katika gharama ndogo kulingana na shamba lilipo.

Habari hii nimetoa katika kurasa ya KilimoJoint huko Facebook na nikaona si vibaya nikawapa wadau mlioko interested na kilimo cha mboga mboga mka jifunze.

1436325355549.jpg
 
Green capsicum is dorminant in big food stores almost everywhere! Hata Tz sidhani km hizo yellow & red zina soko sana.

Ni km water melons, hizi common ndio zipo kibaoo lakin honey wm ama rock wm sijawahi hata ziona tz zaid ya Nairobi. For the case of business unaweza jaribu😳
 
Jerrymsigwa kweli za njano na nyekundu sio common sana hapa kwetu ila gharama yake iko juu zaidi. Kama mara tatu au nne zaidi ya bei ya hoho za kijani kama sikosei. Mtu akipata tenda kwenye supermarket lazima apate hela ya maana.
 
Last edited by a moderator:
Nilitaka kuliam hizo mda si mrefu nimeshukuru kujua kumbr haziitaji jua kama unaamua kulima nje.. ahsante kiongozi
 
Wakuu nawasalimu sana, please naomba aliewahi kufanya hiki kilimo anisaidie nijue A-Z yake, mchakato mzima wa kukifanya, risk zake, mauzo/soko, mapato nk. Natanguliza shukrani za dhati.
Mkuu hili zao mimi nalima tena sana tu kwnza kwa hiyo bajeti aliyoiweka ni ndogo sana mbegu tu kama unapanda mbegu chotara mf tycoon kwa hk 1 ni sh 250000 kukodisha shamba inategemea kiwango cha chini kbs ni 100000 kulimwa trekta tsh45000 kupiga halo tsh 40000 kulima matuta tsh 80000 mbolea ya kupandia kg100 =140000 vibarua wa kupanda tsh 50000 madawa ukungu+sumu=250000 mbolea kuumwa kg100 =tsh120000 mbolea kuzalishia kg100 =100000 ghalama za umwagiliaji namaanisha petrol tsh120000 palizi tsh100000 boy shamba tsh200000 ziada tsh 200000 soko inategemea na msimu kunakipindi gunia mmoja ni 80000-150000 kwa hk moja ukiitunza vizuri wastani wa maroba 20-30 kwa wiki pilipili hoho inavunwa kwa wastani wa miezi 3-6 inategemea na hali ya hewa
 
Mkuu hili zao mimi nalima tena sana tu kwnza kwa hiyo bajeti aliyoiweka ni ndogo sana mbegu tu kama unapanda mbegu chotara mf tycoon kwa hk 1 ni sh 250000 kukodisha shamba inategemea kiwango cha chini kbs ni 100000 kulimwa trekta tsh45000 kupiga halo tsh 40000 kulima matuta tsh 80000 mbolea ya kupandia kg100 =140000 vibarua wa kupanda tsh 50000 madawa ukungu+sumu=250000 mbolea kuumwa kg100 =tsh120000 mbolea kuzalishia kg100 =100000 ghalama za umwagiliaji namaanisha petrol tsh120000 palizi tsh100000 boy shamba tsh200000 ziada tsh 200000 soko inategemea na msimu kunakipindi gunia mmoja ni 80000-150000 kwa hk moja ukiitunza vizuri wastani wa maroba 20-30 kwa wiki pilipili hoho inavunwa kwa wastani wa miezi 3-6 inategemea na hali ya hewa
Ahsante mkuu were unalima wapi? mimi nataka kuanza kufanya hiki kilimo dar
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom